Mchakato wa Kumtafuta Malkia Wa Jukwaa La MMU yaani "Queen Of MMU" for the Year 2011 umekamilika baada ya kupigwa kwa kura za maoni na baadaye kuwashindanisha walioteuliwa na Tume ya Uchaguzi JF.
Tafadhali Rejea katika uzi ufuatao ili kupata historia:
Tume ya Uchaguzi ya Jamiiforums JEC baada ya kupitia mchakato mzima wa uteuzi wa wagombea na upigaji wa kura imeridhika kwa kauli moja kuwa Uchaguzi ulikuwa HURU NA WA HAKI na hivyo inatangaza kuwa:
Lizzy ni: JF Queen Of MMU - 2011 - (Q-MMU 2011)
Kwa kuwa mhusika ametangazwa mshindi inampasa kuwa na maadili mema kipindi chote atakachokuwa amebeba title hii. Tume haitasita kumnyang'anya ushindi atakapokwenda kinyume na maadili ya JF na Tume.
Sambamba na hilo Members wa JF wanaopenda wanaruhusiwa kumwita kwa jina lake la heshima yaani: Q-MMU Lizzy.
Pia sambamba na hilo zawadi ya TZS 50,000 itatolewa kwa mshindi wetu huyu.
Kwa niaba ya wana JF wote tume inapenda Kumpongeza kwa dhati kwa ushindi alioupata.
Wote Mnakaribisha Kumpongeza Q-MMU Lizzy kwa Ushindi alioupata.
Hongera lizzy jamani,ngoja nilete na mahari kwenu nikuoe kabisa,nasikia umeachika kwa Nape sasa mi ntakuoa na nitakuhudumia vizuri hadi utapendeza girl wangu lizzy.