Liyumba Azidi Kubanwa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
MKURUGENZI wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Julius Andrew amesema malipo mengi makubwa yaliyofanywa katika ujenzi wa majengo mapacha ya benki hiyo yaliidhinishwa bila idhini ya bodi na aliyekuwa Gavana, marehemu Daud Balali.

Shahidi huyo watatu kwa upande wa mashitaka alidai hayo jana alipokuwa akitoa ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Jopo la mahakimu watatu linaloongozwa na Bw. Edson Mkasimwongwa.

Akiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Bw. Ben Linkolin shahidi alidai Julai 11 mwaka 2006 alikuwa miongoni mwa waliohudhuria kikao cha Bodi ya Wakurugenzi.

Alidai ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya BoT ambapo menejimenti iliwasilisha.

Bw. Andrew alidai baada ya kuwasilisha taarifa hiyo bodi ilikemea matumizi yaliyofanyika nje ya bajeti iliyopangwa na kuidhishwa.

Shahidi alidai malipo mengi makubwa yaliyokemewa na bodi yaliidhinishwa na marehemu Balali na mshitakiwa Liyumba aliidhinisha malipo madogo madogo kulingana na utaratibu wa benki hiyo bila baraka za bodi.

Alidai maoni na mapendekezo ya kufanyika kwa malipo hayo nje ya bajeti yalitoka kwa Meneja wa Mradi Bw. Deogratius Kweka, yakapitia kwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi, Bw. Amatus Liyumba na kumalizia kwa Gavana wa BoT wakati huo, marehemu Balali.

Alidai malipo hayo yalifanyika bila kupata baraka za bodi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo gharama za kodi ya vifaa vya ujenzi na sababu zingine za kitaalamu.

Akiendelea na ushaidi alikubaliana na Wakili wa Utetezi, Bw. Majura Magafu wakati akimuhoji kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu ujenzi wa majengo hayo ni wa bodi na mshitakiwa Liyumba hakuwa na uwezo wa kutoa uamuzi.

Badaa ya ushahidi huo upande wa mashitaka uliomba kuahirisha kesi hadi Jumatatu na kwamba watawasilisha maombi ya kuongeza idadi ya mashahidi badala ya 10 waliotaja awali.

Mahakimu walikubali maombi yao na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Jumatatu. Mshitakiwa katika kesi hiyo, Bw. Amatus Liyumba anakabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya ofisi yake na kusababisha hasara ya sh. bilioni 221.1 kutokana na kuidhinisha malipo ya mradi huo bila idhini ya bodi ya wakurugenzi.

SOURCE: http://www.majira.co.tz/index.php?o...i-kubanwa&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57
 
Wadau wa JF ambao ni wafuatiliaji wa kesi hii naomba hoja zenu juu ya kesi hii kama zipo!
 
Huu uandishi huu, ona hapa chini, hii ndio lead paragraph

MKURUGENZI wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Julius Andrew amesema malipo mengi makubwa yaliyofanywa katika ujenzi wa majengo mapacha ya benki hiyo yaliidhinishwa bila idhini ya bodi na aliyekuwa Gavana, marehemu Daud Balali.

then:

Alidai malipo hayo yalifanyika bila kupata baraka za bodi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo gharama za kodi ya vifaa vya ujenzi na sababu zingine za kitaalamu.

Akiendelea na ushaidi alikubaliana na Wakili wa Utetezi, Bw. Majura Magafu wakati akimuhoji kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu ujenzi wa majengo hayo ni wa bodi na mshitakiwa Liyumba hakuwa na uwezo wa kutoa uamuzi.

halafu linganisha na headline
 
Habari hii inasema kwenye Gazeti la Tanzania Daima kwamba "shahidi amsafisha Liyumba!" Hongereni sana waandishi wetu wa habari!
 
Mwananchi: Shahidi mwingine amtetea Liyumba

Jambo leo:Shahidi adai Liyumba cha mtoto, aliyesaini fedha nyingi balali

Nipashe: mkurugenzi BOT amtetea Liyumba

Mtanzania: Bodi BOT ilikemea matumizi makubwa aliyoidhinisha Balali

Daily News: Ballali approved payments in twin tower project
 
Liyumba lazima ashinde, hakuna kitakachomzuia na serikali ijiandae kumlipa fidia. Hapo ndo utagundua kwamba system zetu ni mbovu sana
 
Mwananchi: Shahidi mwingine amtetea Liyumba

Jambo leo:Shahidi adai Liyumba cha mtoto, aliyesaini fedha nyingi balali

Nipashe: mkurugenzi BOT amtetea Liyumba

Mtanzania: Bodi BOT ilikemea matumizi makubwa aliyoidhinisha Balali

Daily News: Ballali approved payments in twin tower project

Hapa Liyumba lazima atoke kama mambo ndio hayo, yaani shahidi upande wa mashtaka anamtetea mshtakiwa? Prosecution, wake up please, the battle isn't on your side!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom