Liyumba arejeshwa tena rumande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Liyumba arejeshwa tena rumande

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,434
  Likes Received: 5,691
  Trophy Points: 280
  ate::6/1/2009
  Liyumba arejeshwa tena rumande vivuli vya hati vyakataliwa kortini
  Na Nora Damian

  KAMA ni balaa, basi ni hili linalomwandama kigogo wa zamani wa Benki Kuu (BoT), Amatus Liyumba ambaye jana alilazimika kurejea rumande baada ya mahakama kukataa kupokea vivuli vya hati za mali alizowasilisha kwa ajili ya kupata dhamana.

  Lakini kuwekewa pingamizi kwa dhamana ya Liyumba jana kulisababisha upande wa utetezi kudiriki kusema kuwa upande wa mashtaka una hila dhidi ya mkurugenzi huyo wa zamani wa utumishi na utawala wa BoT na hivyo kuzua malumbano ya kisheria.

  Pamoja na kukwama kwa dhamana yake jana, hali imezidi kuwa tete kwa Liyumba baada ya mahakama kuelezwa jana kuwa kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka yaliyoisababishia serikali hasara ya Sh221 bilioni, limeitishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kupitiwa.

  Jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, mmoja wa mawakili wanaomtetea mshtakiwa huyo, Majura Magafu aliwasilisha vivuli vya nyaraka kadhaa, ikiwemo hati ya kusafiria, hati ya nyumba ya Liyumba na ripoti ya uthamini wa nyumba hiyo ili mteja wake apate dhamana.

  “Tunaomba mahakama kama itaridhia, ipokee copy (vivuli) za nyaraka hizi kwa sababu nyaraka original (halisi) zilishatolewa hapa mahakamani katika kesi nyingine ya mteja wetu ambayo ilifutwa,” alidai Magafu.

  Lakini wakili wa serikali, Justus Mulokozi alijibu ombi hilo kwa kudai kuwa hawana uhakika kama nyaraka halisi bado ziko mahakamani kwa sababu zilikuwa katika kesi ya awali ambayo ilifutwa baada ya mahakama kubaini upungufu katika hati ya mashtaka.

  Pia alidai kuwa Ijumaa iliyopita walipewa hati nyingine na upande wa utetezi kwa ajili ya kuipitia, lakini imewaweka katika mkanganyiko.


  “Hatujapata majibu rasmi ya maandishi kutoka Wizara ya Ardhi, lakini tulipata taarifa zisizo rasmi kwamba uhalali wa hati hiyo haukuweza kuthibitika moja kwa moja,” alidai Mulokozi.

  Hoja hiyo ya upande wa mashtaka ilizua malumbano ya kisheria baada ya Wakili Magafu kudai kuwa upande wa mashtaka una hila za kutaka kumkwamisha mteja wake kupata dhamana.

  Kauli hiyo ya Magafu ilisababisha Wakili Mulokozi kusimama na kumwambia Magafu ale kiapo kwanza kwa anayotaka kuyasema.

  Magafu aligoma kula kiapo, hali iliyomlazimu Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba kuingilia kati na kumuonya Magafu kutumia lugha nzuri mahakamani.

  “Ninachokisema ni ukweli na wala sili kiapo sisi tunahisi kuna kitu katika kesi hii kwa sababu kesi ya awali ilipofutwa na mshtakiwa akaletwa tena mahakamani hakuna nyaraka zozote zilizorudishwa kwa mshtakiwa,” alidai Magafu.

  “Tunaheshimu na tunaiamini mahakama kwamba kitu kikiwa chini ya mahakama kinakuwa katika ulinzi, kama upande wa mashtaka hauna nia mbaya na mshtakiwa, tunaomba haki itendeke ili aweze kupata dhamana,” alisema.

  Alidai kuwa kifungu namba 148, vifungu vidogo vya (6) na (7) vinatoa masharti ya dhamana na mahakama inatakiwa kuhakikisha yanatekelezwa na si upande wa mashtaka.

  Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Mwaseba alisema kuwa hataweza kutoa dhamana kwa mshtakiwa huyo kwa kutumia vivuli vya nyaraka na kwamba endapo upande wa utetezi utatimiza masharti hayo waombe hati ya kumleta mteja wao mahakamani kwa ajili ya dhamana.

  “Mahakama inatakiwa ijiridhishe kwa sababu nyaraka hizo sikuzipitia mimi, alizipitia hakimu mwingine na kesi ya Liyumba ilishaendeshwa na mahakimu wengine wawili hivyo siwezi kujua wao waliamua nini,” alisema Hakimu Mwaseba.

  Pia hakimu huyo aliuagiza upande wa mashtaka kwenda kukagua anwani za wadhamini wawili waliotajwa na upande wa utetezi kwamba wanafanya kazi BoT ili waweze kujiridhisha.

  Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 15 mwaka huu itakapotajwa, lakini aliushauri upande wa utetezi kama ukitimiza masharti ya dhamana waombe kibali cha kumpeleka mshtakiwa mahakamani kwa ajili ya kukamilisha dhamana.

  Kukataliwa kwa dhamana ya Liyumba mwendelezo wa vikwazo vya kisheria ambavyo kigogo huyo wa zamani wa BoT amekuwa akikabiliana navyo tangu alipopata dhamana kwa mara ya kwanza Februari 17 na baadaye dhamana yake kubatilishwa kutokana na kubainika mapungufu mengi kwenye hati alizowasilisha, ikiwemo hati iliyoisha muda ya kusafiria.

  Wiki iliyopita mawakili wake walishinda hoja ya kupinga masharti ya dhamana yanayotaka mshtakiwa atoe fedha au hati za mali zenye thamani ya nusu ya fedha anazodaiwa kuiba.

  Alitakiwa atoe Sh55 bilioni au hati za mali zisizohamishika zenye thamani hiyo, lakini mahakama ikakubaliana na hoja kuwa masharti hayo ni kwa washtakiwa wanaotuhumiwa kuiba kesi, wakati kesi ya Liyumba ni ya matumizi mabaya ya madaraka.

  Kwa mantiki hiyo, Hakimu Mwaseba aliweka masharti ya kumtaka atoe fedha taslimu Sh300 milioni au hati za mali yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa; awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh 50 milioni kila mmoja; asisafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuwasilisha hati yake ya kusafiria polisi.

  Kabla ya kupandishwa tena kizimbani, Liyumba aliachiwa Jumatano wiki iliyopita baada ya mahakama hiyo kubaini kuwa hati ya mashtaka ina makosa ya kisheria.

  Liyumba alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Januari 27 mwaka huu na kushtakiwa pamoja na meneja mradi wa BoT, Deograthias Kweka kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yaliyoisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 221 bilioni.

  Februari 17 aliachiwa kwa dhamana ya Sh882 milioni, lakini Februari 24 dhamana hiyo ilifutwa baada ya hati 10 alizowasilisha mahakamani hapo kubainika kuwa na mapungufu na kwamba mshtakiwa huyo alikuwa na hati nyingine ya kusafiria ambayo hakuitoa mahakamani.

  Machi 13 Hakimu Hadija Msongo, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo awali, alijitoa baada ya mahakama kulaumiwa kuwa dhamana ya Liyumba ilikuwa na utata.

  HUYU HATOKI MPAKA AOMBE RADHI KWA KULA CHAKULA CA MNUKULU
   
 2. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  “Mahakama inatakiwa ijiridhishe kwa sababu nyaraka hizo sikuzipitia mimi, alizipitia hakimu mwingine na kesi ya Liyumba ilishaendeshwa na mahakimu wengine wawili hivyo siwezi kujua wao waliamua nini,” alisema Hakimu Mwaseba.

  Kama ni kweli hayo yaliyoandikwa kwenye hilo gazeti hayakunukuliwa vibaya, basi sababu za Hakimu Mwaseba hazijaegemea katika katika picha ya kutaka kumtendea haki mtuhumiwa.

  Hakimu Mwaseba akiwa na ufahamu mzuri kuwa nyaraka zilikwishatolewa katika kesi ambayo iliendeshwa kwenye mahakama hiyo, je hii kauli ya kutaka mahakama ijiridhishe si sahihi, labda angedai kuwa yeye hakimu Mwaseba ndiyo anataka kujiridhisha, kwahiyo alitakiwa aseme ni kwa namna gani atajiridhisha na sio kuutupia mzigo upande wa utetezi as if kesi ya kwanza ilikuwa katika mahakama ambayo si Tanzania.

  Haya mambo ya umangi meza katika vyombo vyetu vya sheria huwaumiza watu wengi hasa wananchi wa kawaida ambao kwamba hata mashauri yao haya ripotiwi kama ambavyo yalivyo mashauri ya watu maarufu.

  Ninatoa wito kwa Msajili wa mahakama kanda ya Dar es Salaam afuatile kwa karibu utendaji wa mahakama zetu hasa Kisutu kwa baadhi ya mahakimu.
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  vick Kamata aanausikaje hapo?
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu leta ushahidi wa kutosha kuhusu kuingiliana kwa Mkulu na Liyumba kwenye totoz, kinyume na hapo usilete porojo za uzushi jamvini!

  Mwaga dataz, au omba wadau wenye nyeti za jamaa wamwage jamvini!!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh, hata mimi nilidhani labda nimeamka na hang-over, maana nilikuwa naona maluweluwe tu.
   
 6. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mama Mia

  Usituchanganye hapa.......kichwa cha Habari kina sema MAMBO YA VICK KAMATA................ukisoma habari humo ndani haihusiani na Vicky Kamata.

  Vicky Kamata anahusikaje hapo?
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hizi ni gossipps!
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ooh!thank u mods kwa kubadilisha title
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Wanamuonea....tuuu kwani ni yeye peke yake alieidhinisha.....kwa kweli wanamuonea....
   
 10. M

  Mkora JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwani Vicky peke yake mbona Raya wa Derby hamumtaji aliyekuwa demu
   
  Last edited: Jun 2, 2009
Loading...