Liwazo: Wale wanaohisi wana vibamia

Liwazo: Wale wanaohisi wana vibamia

Quinine Mwitu

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2014
Posts
5,530
Reaction score
6,126
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaohisi wana upungufu wa nguvu za kiume au na maumbile madogo(vibamia), hali ambayo ni hatari sana. Hatari hiyo ni kubwa kwa sababu baadaye inaweza ikapelekea kuwa ni tatizo la kisaikolojia na pia hata wanaoamini hivyo kwa kiasi kikubwa wamekuwa na tatizo la kutokujiamini kisaikolojia.

Inaweza ikawa imechangiwa na wapenzi wao baada ya kuwaambia kuwa hawawezi kuwaridhisha maana kama tunavyoambiwa ki mapenzi kasoro yoyote itakayotakwa na mpenzi wako juu ya uhusiano kingono huwa ina athari kubwa.

Labda niseme kitu kimoja kuwa haijalishi wewe una umbile gani, una postion gani kiuchumi n.k. Unaweza furahia ngono kama mtu yoyote anavyoweza kufurahia

1. Acha kutokujiamini, ni kweli huwezi mridhisha mpenzi wako kila siku kama yeye ambavyo hawezi kukuridhisha kila siku. Kwa hiyo hii haipaswi kutumia kama kigezo cha wewe kuwa na inferiority complex. Mpenzi wako akiwa akiona unajiamini, anaamini pia kuwa unajua na unaweza.

Utafiti wa haraka haraka unaonyesha wanaume wengi wakiwa wanajiandaa kufanya mapenzi, huwa wanafikiria jinsi gani watawaridhisha wapenzi wao, vipi ukitokea ameshindwa mwenzi wake atamfikiria vipi? Hali ambayo humnyima kujiamini

2. Nini unatumia kama chakula chako cha kila siku? Kula chakula kitakachokufanya uendelee kuimarika kimwili na kiakili. Vyakula vyenye mafuta mengi siku zote vimekuwa ni kikwazo kwenye masuala ya sex

3. Endelea kujifunza kila siku. Kama wanavyosema, sex is an art. Ukishamjua manzi wako anataka nini, mwanamke akifanyiwa vile anavyotaka hasa kwenye masuala ya foreplay hata unywele unatosha kufanya apagawe, nini kibamia?

4. Mazoezi. Hakuna dawa inayoweza kutatua tatizo la nguvu za kiume zaidi ya saikolojia, ulaji na mazoezi.

USIRUHUSU WOGA NA KUJISHTUKIA KUKATAWALA MAHUSIANO YAKO
 
Mna taabu vijana ondoeni hofu Mungu alivyokuumba alijua utamudu maadam utakutana na fitting muafaka. Wewe unajijua Anduche halafu unakwenda paramia tembo ; hapo utasema una kibamia au umevaa kiatu oversize?
 
hahha faraja ni kitu muhimu sana,ndizo zilimfanya kipepe ashawishike kwenda kutaka kumkamua maziwa simba
Hahahaaaa. Ila mtu anaweza jifariji akiwa peke yake ila itakapotokea ndio anakaribia kwenda kwenye ile shughuli lazima kamoyo kadunde mkuu.
 
Mna taabu vijana ondoeni hofu Mungu alivyokuumba alijua utamudu maadam utakutana na fitting muafaka. Wewe unajijua Anduche halafu unakwenda paramia tembo ; hapo utasema una kibamia au umevaa kiatu oversize?
He created you in a complete way
 
Back
Top Bottom