Liwale: Mkuu wa shule na matroni ambayo binti alizalia shule wavuliwa madaraka

Walimu nao ni wapumbavu (samahani) ukuu wa shule wameugeuza mgodi


Ifike pahala na wao wajue hicho kiti siku hizi ni cha moto,

Bajeti yenyewe haieleweki na uhakika nao wa mtumishi uko hatihati.
 
Shida ipo kweli,do you see now mkuu kavulishwa madaraka kwa uzembe wa wakubwa wake
Na wa kumtetea hamna maskin. Sema kwa hali ilivyo saiv ukijifanya mjuaji ndo wanakuzima kabsa,bora uwe tu mnyonge ukubali matokeo unless una "konekshen"
 
Kosa la uzembe wa uwajibikaji na kutokutimiza wajibu wao.

Shule za bweni za wasichana, upo utaratibu wa kuwapima mimba wanafunzi.

Haiwezekani kipindi chote cha miezi 9 mwanafunzi asigundulike na huo ujauzito.

Kama ni uzembe tuacheni utetezi, mwalimu anabeba dhamana ya mzazi, pindi mtoto anapokuwa chini ya uangalizi wake wa moja kwa moja.
Kwamba mwanafunzi kupata mimba ni kosa la mwalimu? Au sijaelewa vzur point yako mkuu
 
Kwamba mwanafunzi kupata mimba ni kosa la mwalimu? Au sijaelewa vzur point yako mkuu
Point ya uwajibikaji hapo ni kule kutokuwafanyia medical checkups wanafunzi kama ilivyo ada.

Angeligundua tatizo hilo mapema kwa mwanafunzi huyo na kuchukua hatua za kinidhamu, wala asingelipata madhila aliyokumbana nayo.
 
Point ya uwajibikaji hapo ni kule kutokuwafanyia medical checkups wanafunzi kama ilivyo ada.

Angeligundua tatizo hilo mapema kwa mwanafunzi huyo na kuchukua hatua za kinidhamu, wala asingelipata madhila aliyokumbana nayo.
Yeah you are right,majuto ni mjukuu
 
Haya matamko yanashida sana.

Yaani mkuu wa wilaya anakurupuka tu na kumvua madaraka mkuu washule?Je imebainika kuwa yeye ndiye aliyempa mimba huyo mtoto?

Mkuu wa shule yuko pale kutokana na taaluma yake na si kwamba aliwekwa pale kuwa kunyooshewa kidole(Kuteuliwa)

Kwa mawazoyangu, matron ndiye anapaswa achukuliwe hatua maana inawezekana hao wanafunzi walikuwa hawapimwi mimba, na kama walikuwa wanapimwa, basi alijua akapiga kimya.
Zoezi la upimaji linapaswa kufanyika walau mara moja kila miezi miwili
 
Imagine huyo mkuu wa Wilaya naye alikuwa mwalimu amenifundisha chuo.Mwalimu akipanda cheo huwa ana "deal" na Waalimu wenzake,hii kada ina shida kubwa
 
Back
Top Bottom