Liwale: Mkuu wa shule na matroni ambayo binti alizalia shule wavuliwa madaraka

Na bado kuna wapuuzi wataendelea kumdefend mtoto mjinga aliyekubali kurubunika kisa chipsi yai na akapewa mimba, huku vibarua vya watu vikiota nyasi.
 
Awamu hii ina vituko sana ndio madhara ya oda kutoka kwa fulani, mwalimu wamemuonea sana
 
Ni sahihi huo ni uzembe wa hali ya huku,zamani enzi zetu kila baada ya miezi mitatu wanafunzi wote wa kike walikua wanapimwa ujauzito,wangefanya hivyo lazima wangefahamu mapema.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kiangara pamoja Na Matron wa shule hiyo wamechukuliwa hatua za kinidhamu kwa kile kinachodaiwa wameshindwa kuwajibika ipasavyo kwenye upande wa malezi hadi kupelekea Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo ya bweni ajifungulie shuleni.

Mwanafunzi huyo anadai mwanzoni hakuwa anajifahamu kama ni mjamzito mpaka siku alipojifungua na hata Walimu na Matron nao kwa kipindi chote hawakugundua kuwa Mwanafunzi huyo ana mimba.

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba amesema Mkuu wa Shule na Matron wamevuliwa Madaraka, na bado Polisi wanaendelea kumtafuta Kijana aliyempa mimba mwanafunzi huyo na kisha kutoroka.


Nb huu ni uonevu kwa walimu

Pia Soma
 
Ila kweli aisee mimba hadi inafika miezi tisa watu hawajui
Nimewahi kushuhudia pia mwanafunzi alijifungua bwenini na hakuna mtu aliyekuwa akijua kama alikuwa ni mjamzito, ila yeye alikuwa ni chibonge na muda mwingi alikuwa akivaa sweta
 
Halafu Wakuu
Mbona msichana akipata mimba halaumiwi Wala vyombo vya kisheria havimgusi ?
Mwalimu Mkuu anavuliwa madaraka.
Matron anavuliwa madaraka pia.
Kijana mtia mimba anatafutwa ili afungwe miaka mingi.
Msichana mwenye mimba haguswi kabisa yaani Kama alilazimishwa kuvuliwa nguo na kutendwa.
Msichana anaheshimiwa kana kwamba hakuhusika na chochote.
Ivi huu ni uungwana kweli?
Hii Ni haki kweli?
Wakati huyo msichana ndio chanzo Cha yote kwakuwa ndiye aliyekubali kwa hiari yake.
Vischana wakati huu vinajimanua tu vikijua havitachukuliwa hatua yoyote Ile ?
Hivi ndo vikitakiwa viwe vya kwanza kuchukuliwa hatua.
Acheni hizo
 
Sasa hapo Mwalimu kosa hulioni?
Miezi 9 kweli hujawahi kuwapima watoto mimba. Hata akitapika hukumuona.
Maana yake wewe uko mbali sana na wanafunzi wako

Kasome uzi alionitagi, Kuna zaidi ya hayo.
Achana na mwalimu km umeishi kitaa mtoto wako anaweza kuficha mimba mpk miezi 6 usijui itakuwa walimu.
Ambao kazi yao Ina shida lukuki
 
Back
Top Bottom