Young Africans leo inashuka katika
dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam kucheza na maafande wa
jeshi la kujenga Taifa nchini timu ya
JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ikiwa
ni muendelezo wa michezo ya Ligi
Kuu ya Vodacom mzunguko wa 12.
Mara baada ya ushindi wa pili
mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya
Rhino Rangers na Mgambo Shooting
kikosi cha mholanzi Ernie Brandts
kimeendelea kuimarika na safu ya
ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo
kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Mpaka sasa Young Africans inashika
nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi
1 nyuma ya timu zinaongoza mbili za
Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na
pointi 23 zikitofautiana kwa mabao
ya kufunga na kufungwa.
Young Africans inahitaji pointi tatu
muhimu katika mchezo huo wa
kesho dhidi ya JKT Ruvu ili iweze
kujikita kileleni na kukalia kiti cha
uongozi wa Ligi Kuu kwa kufikisha
pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa
na timu mbili tu za Azam FC na Mbeya
City ambazo zitachezwa mwishoni
mwa wiki.
Timu iliingia kambini jana jioni
katika hostel zilizopo makao makuu
ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani
kujiandaa na mchezo huo ambao ni
muhimu kwa vijana wa Jagwani
kuhakikisha wanaendeleza wimbi la
ushindi na kupata pointi tatu
muhimu.
Katika mchezo wa kesho Young
Africans itakosa huduma ya
wachezaji wake David Luhende na
Nizar Khalfani ambao ni majeruhi
huku kiungo Haruna Niyonzima
akiukosa mchezo huo kutokana na
kuwa nchini Rwanda alipokwenda
kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Wapenzi, washabiki na wanchama
wa Young Africans kesho
wanaombwa kujitokeza kwa wingi
kuja kuwashangilia vijana katika
mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.
dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam kucheza na maafande wa
jeshi la kujenga Taifa nchini timu ya
JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani ikiwa
ni muendelezo wa michezo ya Ligi
Kuu ya Vodacom mzunguko wa 12.
Mara baada ya ushindi wa pili
mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya
Rhino Rangers na Mgambo Shooting
kikosi cha mholanzi Ernie Brandts
kimeendelea kuimarika na safu ya
ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo
kuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Mpaka sasa Young Africans inashika
nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi
1 nyuma ya timu zinaongoza mbili za
Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na
pointi 23 zikitofautiana kwa mabao
ya kufunga na kufungwa.
Young Africans inahitaji pointi tatu
muhimu katika mchezo huo wa
kesho dhidi ya JKT Ruvu ili iweze
kujikita kileleni na kukalia kiti cha
uongozi wa Ligi Kuu kwa kufikisha
pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa
na timu mbili tu za Azam FC na Mbeya
City ambazo zitachezwa mwishoni
mwa wiki.
Timu iliingia kambini jana jioni
katika hostel zilizopo makao makuu
ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani
kujiandaa na mchezo huo ambao ni
muhimu kwa vijana wa Jagwani
kuhakikisha wanaendeleza wimbi la
ushindi na kupata pointi tatu
muhimu.
Katika mchezo wa kesho Young
Africans itakosa huduma ya
wachezaji wake David Luhende na
Nizar Khalfani ambao ni majeruhi
huku kiungo Haruna Niyonzima
akiukosa mchezo huo kutokana na
kuwa nchini Rwanda alipokwenda
kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Wapenzi, washabiki na wanchama
wa Young Africans kesho
wanaombwa kujitokeza kwa wingi
kuja kuwashangilia vijana katika
mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.