Live Updates: Yanayojiri bungeni Dodoma, leo tarehe 17 Juni 2014

Live Updates: Yanayojiri bungeni Dodoma, leo tarehe 17 Juni 2014

Mheshimiwa Batenga
Kapiga mavitenge yake hapa safi na nywele kazichana fresh, alafu kwa nini wanawake wanaweka nywele kama wanaume?

Anamsifu Mkuya kwa kujiamini, lakini anamshauri awe msikifu, nadhani kuna dalili za huyu dada kutokuwa msikivu, mtu wa pili sasa anazungumzia hili swala.

kawasifu Mwigulu Nchemba Madelu na Malima.

Kaanza kuponda baada ya kutoa sifa kwa mawaziri

Anadi ni makosa BRN kuiacha sekta ya Afya, hivi haimo kumbe? ma - CCM Bwana, si ndo yangeweka hii yakanunua zile bajaji na kupiga bao la kisigino faster, the dying are dead.

Anataka wanawake wapigiwe saruti kwa kazi ya kuzaa.

anasema hakuna vitanda vya kutosha japo kwa wazazi,

huyu mama hana amsha amsha kabisa, yeye kang'ang'ania wanawake waonewe huruma waonewe huruma, anaongea ujinga hapa, eti wanaume wajaribu kujifungua - this woman??

Anasema hili limemkaa rohoni sana, wakati watu kibao wameisha lizungumzia, na Mheshimiwa rais alisema atarilekebisha, sasa anakaa nalo rohoni kivipi, si ndio unafki huu.

Wanajeshi sasa.
anasema kuna jeshi la akiba, wako huko wastaafu, nadhani anazungumzia wapewe mshiko, anadai pensheni ni ndogo, walipwe kama mawaziri wakuu.

Kamaliza Mheshimiwa Elizabeth Batenga
 
Last edited by a moderator:
Mwingine tena
Nywele zake kama za waarabu, sijui ni wigi, ila ni kama za waarabu.

Kaanza kusifiaaaaa
anaendelea kusifia kwa ile excise duty ya 15% luondolewa, na kuhamishiwa kwa mabank, bila kufikiria eti anasema serikali iangalie kodi hiyo isije kuhamishiwa kwa wananchi, sijui nani kamuambia mabank yataibeba yote nzima nzima

BRN Sasa, anapongeza BRN kupewa pesa, anasema tupewe tathmini za BRN, Nadhani anahisi ni kimeo kingine kama kawaida.

RELI ya Kati sasa, kuna watu wanasema haijengwi sababu hakuna pesa, kwanza pesa za kujenga lile bomba la mafuta na za kujenga hii reli zipi nyingi?

Anasema tutumia gas kama collateral tukope tujenge reli, kweli kwa nini hatufanyi hivi?? anasema debt is cheap than equity na anasema tukope tuuu.

Vitambulisho sasa, eti hatuwezi kupanua wigo wa kukusanya kodi hii issue isipokamilika mapema, anasema NIDA wapewe mshiko wapige kazi.

Uchumi utaendelezwa na sekta binafsi na sio serikali, kweli kabisa dada.

Sasa anasema kodi ndogo ndogo, alafu kumbe ni wakilimanjaro, sijui mmachame huyu?? sijamuelewa anasema nini ila kuna kitu kasifia

anaitwa Betty Eliezer Machange
 
Mjuu wa Nyerere sasa.
Anasema serikali ni oga, anasema ukihesabu matairi ya magari tu utaona fursa ya viwanda, kwamba tuwaambie wageni hatutaki bidhaa zao tunataka viwanda vyao.

Anazungumzia Mohamed Kessy, kampa kick, kampaisha na Msechu na NHC

Nyerere hajajipanga na yeye naona.

Anasema Dada za Mkuya kuhusu ajali za barabarani haziko sawa,naona anataka kuleta ile issue ileeee ya kugagua magari huko nje, anasema hakuna ufanisi.

Anasema agencies zipunguzwe zimekuwa nyingi sana, TFDA,TBS n.k

Anasema TFDA wanachukua magunia ya sukali kama sample,

duuu, eti wafungwa wanalala tu, wanakula tu, waziri wa mambo ya ndani anapaswa kuomba matrekta sio hela.

anasema serikali inaogopa kufanya biashara kivipi?

enhe kuna mtu anashikwa wizi hapa.

Biometric Mashines, wizara ya mambo ya ndani imeomba, na jamaa wa tume wa uchaguzi wameomba, kwa nini wasishee?

Wizara ziseme zinakaa vikao vingapi, na waache kwenda kwenye vikao vya ukimwi.

hajaunga mkono hoja
 
-==Ole medeye anaona punguzo la kodi asilimia moja kwenye mshahara wa mfanyakazi ni dogo mnooooo.....kodi ipungzwe hadi songle digit na anamuomba waziri atekeleze hilo sasa,
===ongezeko la nyongeza ya mshahara wa wafanyakazi ni dogo mno
===analalamikia ubovu wa miundombinu esp barabara maeneo ya vijijini
 
Chiku ambwao
===anasema kama wabunge tunakaa hapa kuipongeza serikali ni uzuzu
===kwamba kazi ya upinzani ni kukosoa na kutoa mawazo mbadala kwa nchi
===anampongeza chenge kwa mapendekezo mazuri aidha anapongeza mawaziri vivuli kwa taarifa zao
anamhurumia chenge kulalamikia kutotekelezwa maoni ya kamati ya fedha ya bunge lakini bado anaunga mkono bajeti
===anashangaa serikali kutegemea vileo km pombe,sigara, kuwa chanzo kikuu cha mapato
===anasema serikali haifanyi kazi ya kusimamia mapato esp migodini,viwandani na ktk sekra za utalii na mali asili ya nchi
 
Abwao anasema ni kiini macho kutegemea kupata maendeleo km nchi kwa kumtegemea mgeni
 
Abwao anasema amefanya ziara jimbo la isimani kuna kero kubwa sana ya maji,tatizo kubwa la huduma za afya na miundombinu ya barabara....sina ugomvi na waziri lakini tupeni huduma jamani
 
Shabiby anashauri serikali ipunguze kodi kwenye magari mapya kuliko kuongeza kodi kwenye magari chakavu
 
Anadhauri kurudisha kodi ya kunyonga wahujumunuchumibkama china
 
Mkosamali sasa
==anaanza kuwashangaa wabunge wanaolalamika kila mwaka...kwamba kiongozi si mlalamikaji bali mtatua matatizo
==anawashangaa kamati ya bajeti kula laki tano kila siku bure lakini hakuna kazi wanafanya
 
Mkosamali anakatibia kulia kwa uchungu kwa ubabaishaji wa kamati ya bajeti na wabunge kutokufanya kazi yao ipadavyo
 
Sangarara.....
hongera sana kwa updates...keep it up but ondoa hisia za kisiasa...report kinachotokea sio unachokipenda wewe coz hapa watu wanatofautiana itikadi za kisiasa.....
 
Nimefurahishwa sana na mchango mzuri wa mbunge huyu kijana. Wakati akichangia bunge la bajeti leo jioni Mkosamali amewashauri wabunge kuacha kulalamika na badala yake kufanya kazi yao kama wabunge na mhimili mmojawapo wa serikali na wenye nguvu kubwa. Kizuri zaidi kamchana Rage kwamba anapigapiga kelele wakati wananchi wake wa Tabora wanazidi kutaabika.
Kaichana kamati ya bajeti kwamba kazi yao ni kuchukua posho ya laki 5 huku wakija na hoja za kulalamikalalamika kila siku. Kudos Mheshimiwa Mkosamali.
 
na malalamiko yooooooote ya asumpter mshana, kaunga mkono hoja.
alafu huyu Naibu speaker anasema huyu mwanamke ni wa watu wa Jimbo la Kongwa, kivipi?

Sangarara ni hivi N/Spika aliposema Assumpter Mshama ni wa watu wa jimbo la Kongwa kwani huelewi? Assumpter Mbunge wa Nkenge Bukoba ameolewa na Julius Mshama wa Mtanana huko kwetu Kongwa. Mimi ni shemeji yangu na hata kampeni kule Bukoba alichukua vijana wa Mtanana kumsaidia. Hivyo Ndugai hajakosea sisi huyo ni mke wetu. Hlojina a Mshama la mumewe.
 
Nimefurahishwa sana na mchango mzuri wa mbunge huyu kijana. Wakati akichangia bunge la bajeti leo jioni Mkosamali amewashauri wabunge kuacha kulalamika na badala yake kufanya kazi yao kama wabunge na mhimili mmojawapo wa serikali na wenye nguvu kubwa. Kizuri zaidi kamchana Rage kwamba anapigapiga kelele wakati wananchi wake wa Tabora wanazidi kutaabika.
Kaichana kamati ya bajeti kwamba kazi yao ni kuchukua posho ya laki 5 huku wakija na hoja za kulalamikalalamika kila siku. Kudos Mheshimiwa Mkosamali.

Kwa kweli Rage kaaibishwa sana na Mkosamali kwa kutoa taarifa ambayo yeye mwenyewe hata hajui anachokizungumzia ila alitaka aonekane ana mkosoa mbunge wa upinzani. Mkosamali kawaambia wabunge wa CCM waache kuisemea serikali kwani Bunge na serikali ni mihimili miwili tofauti kabisa na inakazi mbili tofauti.
Kwa kweli uwasilishaji wa Mkosamali una aina fulani ya mvuto na huwa hana hofu na yeyote pia hajipendekezi yeye kama ni kumchana mtu bungeni hahofii hata kama ni PM yeye anampa tuu. Huyu kijana ni hazina


Sent from my iPad using JamiiForums
 
watanzania watu wa ajabu sana kutokana na viongoz wetu karib wote kutotekeleza wajibu wao sasa yule anayetekeleza anapewa mijisifa kemkem.inashangaza kuona hata rais anasifiwa kwa maendeleo ya barabara mbov tena za mkopo

dimond misifa kemkem dar na matuzo ya kumwaga haya alipofika kule kwa wanajua tena akiwa na promota wake JAKAYA kaleta ziro kapozwa na wal maharage kule white house ya dom.
 
Back
Top Bottom