Live Updates: Yanayojiri bungeni Dodoma, leo tarehe 17 Juni 2014

Live Updates: Yanayojiri bungeni Dodoma, leo tarehe 17 Juni 2014

CHAMI SASA
Kwanza anasema anaipenda sana CCM.

Alafu anatoa hisia za wanakilimanjaro juu ya mlima kilimanjaro, kimsingi anaelezea udhaifu wa ma-CCM.

Leo ndo anasema tuwe na kitengo cha Intelligencia ya Uchumi, hajawahi kuwa kwenye baraza la Mawaziri huyu jamaa?

Sasa anazungumzia bank za maendeleo ya wananchi, kwamba Bank za wananchi ni za muhimu kuliko za biashara, na mambo ya mkutabita sijui na nini? anaongea mambo mazuri tu, ila hawa Ma-CCM kwa nini hawasikilizani hata wenyewe tuu?
 
Ohooooo zitto analipuliwa hapa na ndugai kiaina
tanapa haitpi pesa hovyo hovyo, naona wanakilimanjaro nao wanazitolea macho pesa za tanapa
 
Prince Ridhiwan.
Kaanza na kujipendekeza, anamuita Mwigulu Kaka yake wakati alimuacha chuoni.
Alafu kaomba sijui nani huko lugomba aombewe kwa sababu anaumwa sana, nadhani haelewi hali ya sekta ya afya nchini.

Kaenda kwenye Saccos, anaongea kama Baba yake.
Kwamba Nia za saccos kuwasaidia wananchi zinafail kwa sababu ya Riba huko kwa Mabank, nadhani haelewi biashara ya Fedha kiasi.

Anasema PPP ndio tiba ya miradi inayokwamba, "mi nafsi sasa umefika wakati muafaka" yaani kama baba yake 100% kwamba barabara za chalinze na bandari ya bagamoyo zitakuwa zimeende vizuri kabisa kwa sababu private sekta itakuwa imekuwa engaged.

ndo mzungumzaji anayepigiwa makofi kuliko wote leo.

sasa misamaha ya kodi,subiri, anasemaje, hakubaliani na misamaha ya kodi kuondolewa ili kuvutia wawekezaji.

Ridhiwan anasema nchi nzima hii ni mashamba, anasema arusha hakuna mashamba, ridhiwan anahoji kwaaaamba, kama kilimo kinachanga asilimia 4 basi tuna tatizo kubwa.

anasema JKT wameacha kuagiza matrekta kwa sabau pesa hamna, anaponda kilimo kwanza, anasema takwimu zimekosewa, credibity ya takwimu za serikali ziko kwenye lime light sasa.

Ridhiwan anawamaliza ma -CCM leo, au ndo unafiki wenyewe
hakubaliani na kukua kwa uchumi kwa sabau hali ya wananchi ni mbaya sana, hakubali kabisa kabisa kwa sababu maskini ni masikini sana.

Mamaaaaaaa na yeye kaunga mkono hoja.
 
Hivi hawa ma-CCM wakiwa wanaongea huwa hawajisikilizi?
 
Hii imekaaje wakuu, mbunge anapopewa nafasi ya kuchangia mjadala bungeni anaanza kwa kutoa shukrani kwa waliomuombea alipoenda kutibiwa India. Je haya ni matambo, au mikogo! Watu wanakosa huduma hapa nchini wamama hawana vifaa kwa ajili ya kuzalishiwa. Dawa hazipo. Mbunge anasema bila aibu wala huruma kwamba alienda matibabu India. Kwenye mijadala wananchi hawatetewi, isipokuwa kutetea serikari na mafanikio haya ya viongozi wetu kushindwa kutibiwa nchini kwenye hospital za kayumba. Tunasemaje?
Ulitaka awalaani? Mbona unaongea pumba hivi
 
sasa kuna mbunge anawakaanga ma-CCM
Anazungumzia zile megawati wa ka-Ngereja zileeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, megawati 300 sijui za mchuchuma, megawati 250 za wapi sijui, megawato 100 za manzese.

Kwanza kasema hazijazalishwa miezi karibia 36 toka tuelezwe ziko tayari, anauliza zimezingatiwa sasa.

Kakumbushia machungu ya wanamtwara kupelekewa wanajeshi badala ya umeme.


ma-TBC Wameondoa matangazo lakini jamaa alikuwa anaelezea namna serikali inavyodanganya wananchi.

Hayaaa, anasema serikali inafanya copy and paste, mamitambo ya TBC vipi hapa.

Amerudi
anatoa ushahidi wa rushwa,ufisadi,umbeya,ushirikina na wizi huko serikali
Kwamba kuna mtu kampigia simu kwamba kaombwa rushwa ya milioni moja huko wizara ya ardhi.

Hii, eti mkuya alisema serikali italeta vifaa vya kusimamia utekelezaji wa shughuri za maendeleo, hii serikali hii jamani kwa nini inatufanyia hivi, inataka kununua mashine tena, na Big result nao inamaana ndo wanaondoka, si ndo kazi yao hii.

muda wa jamaa umeisha
 
Kafumu Speaking
Huyu kafumu mbona hang'ai kama wenzake, Wabunge wa Tabora na Kigoma wote hawang'ai au miili yao iliishazoa shida.

tuendelee
anazungumzia kodi za majengo,
anazungumzia swala la wananchi kulipa kodi, kama yule dada mzungu, nyerere

sasa anacompare utawala wa Mkapa na Kikwete, atakosana na ma-CCM wenzake sasa hivi.
eti focus ya mkapa ilikuwa kukuza uchumi, hajaeleza focus ya sasa ni ipi, wenye akili tumeishaelewa msimao wake.

anazungumzia FDI,eti tushiriki kwenye free market, kwani model ya uchumi wetu ikoje, hawa ma-CCM vipi hawaelewi hata wanavyoendesha nchi, mbona ni majanga.

Sasa anazungumzia daraja lileeeeee la magufuri lilitaka kumpokonya ubunge, halijaisha mpaka leo sababu pesa haijaenda, anasema 2015 imeishafika walimalizie haraka,

ahaaaaaaaaaaa kumbee wanafanya kazi kwa misingi ya uchaguzi sio.

siamini masikio yangu, ameunga mkono hoja.
 
Lusinde anamalizia
anamshukuru Mungu kwa kupata fursa,sijui mungu ndio anateua wazungumzaji.

kaanza siasa, anachekacheka,anasema wanaopenda scuff wavae tu isiwe tabu, huyu jamaa kanywa pombe nini?

Nachokipenda ni hiki kwa haya majinga
-Kaanza kusema hatukusanyi kodi
-Anasema hazina hakuna waaminifu, inaonekana anamaanisha serikali itafute namna ya kuajiri watu waaminifu ili kuepukana na watumishi wasio waaminifu, hajielewi huyu jamaa, anasema mtu kaajiriwa miaka miwili tu serikalini alafu anakuwa na maendelea makubwa. kimsingi anasema ma-CCM sio waaminifu
- alaaa, alienda china na mwigulu sio.

hana flow nzuri
-Mamaaa sasa anawamaliza madaktari, kwamba manesi walipwe zaidi ya Madaktari
-Anaongea kama yuko kijiwe cha Pombe, anamkosea adamu ndesamburo hapa.

Kama Kawaida
-Anaanza kumponda Mwigulu (na hili ni bila kujijua), kwamba kama uchumi umekuwa mbona vijijini hakuna maendeleo
-anazungumzia sana swala la vijijini,namuunga mkono kwa hili,
-Mazao-Kwamba zabibu inalimwa kama matunda pori kimezarauliwa-wakulima wameachwa, sasa najiuliza wameachwa na nani?
-Anasema Madaktari wapewe bunduki.

Kaunga mkono hoja.
anachekesha sana huyu Jamaa
 
Michango kadhaa imesema ukusanyaji wa kodi hauridhishi wakimaanisha bado kuna walipa kodi ambao hawaguswi kulipa.

Je mfumo uliopo unawafanya Wabunge wenyewe na viongozi wakuu wengine wa serikali kuwa ni walipaji wa kodi wazuri?
 
Tuungane tena Jioni. kikao kimeahirishwa,

Mi-CCM Bwana, yaani ni kujipendekeza pendekeza, unafki nafki, huku yanasifia huku yanaponda, sasa mpaka mtoto wa Rais na yeye anaponda serikali ya Baba yake.
 
Michango kadhaa imesema ukusanyaji wa kodi hauridhishi wakimaanisha bado kuna walipa kodi ambao hawaguswi kulipa.

Je mfumo uliopo unawafanya Wabunge wenyewe na viongozi wakuu wengine wa serikali kuwa ni walipaji wa kodi wazuri?

Wabunge wawili, Ester Matiko na Dalali Kafumu wameelezea umuhimu wa serikali kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulipa kodi, lakini hawajaeleza umuhimu wa wao kulipa kodi.

Hii ndio inaitwa, YES,BUT NOT IN MY BACK YARD.
 
Mkuu Sangarara twashukuru kwa update za mjengon kweli ma-ccm hawajielewi nini cha kufanya wanapokuwa mjengoni maana wanaunga hoja kitu chenye mapungufu
 
Muda mchache ujao bunge litarudi hewani, updates zitaendelea kuja kama kawa wandugu.
 
Saa 10:58 TBC1 wameanza kurusha matangazo hapa, huyu jamaa anayetembea kwa kurusha miko unnecessarily ndo amemaliza kuondoa lile li dude na kaondoka vile vile kwa kurusha miko.

Ndugai amekaa na kuruhusu Katibu kufungua kikao

Ndugai kamuita DR Haji Mponda.

Safi sana, achana na wale wanaomshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapatia nafasi za kuongea, Dr Mponda kamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia afya njema.

anasema anaswali kutoka Ulanga huko
Kwamba uchumi umekuwa kwa asilimia saba, na ndio tumeongoza kwa asilimia saba, anahoji hapa kwamba bajeti yetu ni T 19, Kenya ni T 30 + Na ujanga ni zaidi ya T 19 zetu, anauliza hii inawezekana kivipi?

nadhani ameacha tu kusema anahisi takwimu zimechakachuliwa, hili swala la takwimu kuchakachuliwa naona ni la kweli hili, uzuri linaibuliwa na ma-CCM.

Mpango wa Taifa wa Maendeleo sasa, Mradi wa SAGOT Kama sikosei, nadhani ni mradi wa kilimo huu. ila anasema habari za huu mradi hasa kilombero ujenzi wa barabara umekuwa hadithi kwa muda mrefu, mwaka wa nne sasa.

Alafu kuna issue ya daraja la kilombero, muda wa kumaliza daraja zimebaki miezi saba, pesa zilizotengwa na bilioni saba wakati nakisi ni karibia bilioni 30, anaendelea kuwavua ma -CCM nguo, hivi yanajenga barabara zipi jamani?

Anasema Kilombelo na uranga hakuna mawasiliano ya usafiri.

anaanza kunichanganya sasa, eti pinda ana nia nzuri, pinda huyu huyu???

Buffer zone sijui ndio nini, ma-CCM yanamisemo mingi jamani.

Kamaliza kwa kuunga mkono hoja, na amelalamika mwanzo mwisho hapa. kahoji jambo la msingi sana mwanzoni lakini kanichanganya kuhunfga mkono hoja.

any way.
 
Back
Top Bottom