Live Updates VPL: Simba Sc Vs Biashara Utd,Mkapa Stadium

Sijawahi kumkubali kabisa, anafanya makosa mengi sana uwanjan anakuja kubahatisha kigoli kimoja ambacho kimahesabu kinakuwa hakina faida kulinganisha na Mchango wake uwanjani
Wewe Mzamiru anajua sana mpira na sasa hivi kiwango Chake kiko juu sana. Kawafunga Yanga goli la Nne, Kawafunga Mtibwa lile goli moja Wakati yeye sio mfungaji ni kiungo mshambuliaji. Na sio kiungo mkabaji kama Mkude.
Kocha anamwona mazoezini ndio maana Anampanga.
 
Nimependa sana alichokifanya Ndemla Leo.Kaupiga mwingi sana .
Naona kocha kaanza kumuamini now.
Hana namna zaidi ya kujituma, Ndemla na Ajibu walijisahau sana muda mrefu, walijiona kuwa wameshajua, walipokuja wageni na kucheza mpira mkubwa nao wameanza kucheza soka ya kiwango Chao.
Kwa sasa wote wanacheza vizuri waongeze bidii wataanza kikosi Cha kwanza.
 
Ila wanaoendesha website ya Simba wamezubaa, hamna updates yoyote wameshindwa hata kueleza tatizo la Fraga ni nini na litachukua muda gani wakati wao wapo karibu na timu kuliko chombo chochote cha habari
 
Back
Top Bottom