Live Updates: SIMBA Sports Club vs TP Mazembe

Leo Wazembe ni wanakula 2...
Nakuunga mkono kwa ilo. Naamini Mazembe atoki salama leo! Ila kideo kilichowekwa hapo juu na Ivuga kinaonyesha Simba hasa Kaseja hawakuwa makini. Na kama wataendeleza huu ubishororo watapigwa wao mabao.
 
Matatizo ya Usimba na Uyanga yametufanya Watanzania tuendelee kufungwa kama wendawazimu.

Watanzania hatuna uzalendo inapofikia timu binafsi zinacheza kuwakilisha nchi, utakuta Yanga wanashabikia Mazembe km was******n***e vile! Mijitu na akili zao yanasahau kuwa hapo inayocheza ni Tanzania na siyo Simba, simba inakuwa ni jina tu, lakini unakuta mijitu mizima na ndevu hadi mk**** yanapiga kelele kushabikia Mazembe. Aibu kubwa na tutaendelea kufungwa daima.

na hali hii si kwa Yanga tu kuzomea Simba, bali pia Simba wana tabia hiyo hiyo ya Ki-maniac, kuwazomea Yanga wakiwa na mechi za Kimataifa.

Hii ni sawa na kumwona baba yako yuko mtupu unaanza kucheka ni laana tupu.

Mie inaniuma sana kuona Watz hatuna utaifa, hatuna umoja inapokuja ktk mslahi ya Taifa letu. na haya yamechangiwa na mengi, kwani hata viongozi wetu wako katika mkumbo huo huo. Unakuja jitu kiongozi lakini lina ushabiki wa kishenzi usio na manufaa yoyote kwa Taifa, mradi limesikika sauti tu. Hii inanikera sana tena sana, natamani hata sunami ije iwameze watu wa tabia hii wapotee kabisa. Sina hamu na watu wa hivyi natamani nikawafungie senyenge jangwani wakauke kwa kiu.

Ndio maana hata maendeleo hakuna, sababu za ushabiki usio na maslahi kwa taifa, kuanzia siasa, udini, ikabila, ufisadi, uzinzi, ufataki n.k Kwa kuendekeza mambo haya hatuwezi songa mbele hata siku moja. Tutakuwa wapiga kelele tu na kuishia kunywa pombe na kucheza ngoma.

Tuache ushabiki usio na manfufaa, tutafakari mambo kabla ya kujiweka washabiki wasio na mwelekeo.

Usimba na Uyanga tusipouua katika mechi za kimataifa tuaishia kufungwa tu kila siku hata km wachezaji wetu watajituma kwa moyo mmoja. Hamasa huwatia nguvu wachezaji na huongeza ari ya ushindi lakini siyo zomea zomea isiyo na maana.
TUBADILIKE KWANZA

Hii kitu iko dunia nzima kaka...haikwepeki.

Wee angalia England, ambako haya mambo ya patriotism wenzetu walianza kuya-practice hata kabla msamiati "uzalendo" haujagota kwenye kamusi zetu za huku.

Nakumbuka mwaka 2007 kwenye UEFA Champions League final kati ya Liverpool vs AC Milan, Alex Fergurson alimwahidi Ancelloti chupa ya whisky/wine endapo AC Milan wangeshinda...AC Milan wakashinda na huku akiwa na furaha kubwa, Ferguson akatimiza ahadi yake!

Sembuse huku uswahilini (Bongo) bwana?

Nyie Simba jipangeni kushinda gemu, period...hivi visingizio vya uzalendo vitawapotezea focus bure!
 
banka yupo benchi ila timu ni nzuri,mabeki na viungo ni wengi zaidi
 
Simba wataipiga Tp mazembe kimaneno na si kivitendo, nawatakia game njema ila msiache kutoa updates maana naona kipigo kipo pamoja nanyi
 
Kuna makosa ya kijingajinga yanayofanyika kwa upande wa simba yanayoweza kutukosti.... Samataaaaaa.....dah anakosa goli la wazi!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom