Live Updates: Morocco Vs Tanzania leo, 8 June 2013 uwanja wa Stade de Marrakech

Live Updates: Morocco Vs Tanzania leo, 8 June 2013 uwanja wa Stade de Marrakech

Hili game sio la kukosa kuliona. Hivi kwanini TBC ya tangu alipoondoka Tido haitujali kabisa sisi walipa kodi tunaopenda michezo? Hili suala huwa linaniuma sana
 
Wenzetu Congo ya Brazaville wana uhakika wa kwenda Brazil. Maajabu ya soka hayo, si lazima kila siku Nigeria, Ghana..... Hata sisi tunaweza enda Brazil.
 
kila la kheri stars, ingawa jana inasemekana walikatiwa umeme kwa muda wakati wanafanya mazoezi usiku uwanjani.
Na sisi tulivyo "wakarimu" ingekuwa moroco bdae wanakuja tz,tungewapa ulinzi wa ajabu,na kukataza hata mashabiki kuwapa presha ya mchezo tu!
 
Nimependa sana strategies za technical bench la Taifa Stars kuelekea mchezo wa leo.

Mwalimu ameamua kutumia mfumo wa kushambulia ili tupate goli la mapema na kupunguza kasi ya wao kucheza na kutushambulia.

Mwalimu atatumia mfumo wa 4-3-3 kwa kuwapanga kwa pamoja kule mbele Ngassa, Ulimwengu, Sama Goal wakati Viungo watakuwepo Damayo, Sure Boy na Kiemba. Nyuma kama kawaida Juma K Juma, Nyoni, Kapombe, Yondani na Agrey.

Kwahivo leo tutarajie ushindi, tuna kila sababu ya kushinda ugenini kutokana na maandalizi mazuri ya timu yetu!
 
Back
Top Bottom