Wakuu.
Leo majira ya saa 9, M/kiti wa CHADEMA Taifa, kamanda Freeman Mbowe akiandamana na viongozi kutoka Makao Makuu na wabunge wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, atakuwa na mkutano wa hadhara mjini Songea, Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya ukamilishaji wa uzinduzi wa Kanda ya Kusini (Mtwara, Ruvuma na Lindi).
Mapokezi makubwa (maandamano)yataanzia eneo la Bomba mbili. Mbali ya ku-set agenda za masuala mbalimbali, kisiasa, kijamii na kiuchumi, ambayo CHADEMA inasimamia kwa ajili ya Watanzania, pia atazungumzia masuala kadhaa, zikiwemo kauli za Mzee/Viongozi Wastaafu (ref. Mwananchi ya leo) kuwa wanapaswa kuwa statesmen, hasa katika kushauri taifa kushughulikia primary contradictions kwa ajili ya kutatua matatizo yanayoikabili nchi na Watanzania, badala ya (wao) kutumika kufanya propaganda kwa kuzungumzia secondary contradictions (mfano suala la amani linafanyiwa propaganda sana), huku taifa likiangamizwa na CCM.
Updates combination
Tumaini Makene na
Mohamedi Mtoi itakujuza kila linalo jiri.