Live Updates: Azam & Simba Matches

Mbona kimya vp tena?au ndiyo tayari hapo Chamanzi na Tanga?
 
Uwanja wa Azam Complex mechi ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Azam FC na Ferroviario da Beira imeanza bado ni 0-0 ni dk ya 2
 
Kikosi cha Simba ni Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Donald Musoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Awadh Juma, Badru Ali, Amri Kiemba, Hamis Tambwe na Ramadhani Singano
 
TBC Taifa wamejiunga na Mkwakwani stadium. Mlioko Chamazi tafadhali mtuletee updates bila hila wala unazi. Tanga kuna tension sana.
 
Dua kama hili atakama huyo Mungu angekua Mjomba wako asingelikubali.
 
Last edited by a moderator:
Uwanja wa Azam Complex mechi ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Azam FC na Ferroviario da Beira imeanza bado ni 0-0 ni dk ya 2

Asante sana Mkuu, endelea kutujuza, tunawaombea mshinde.
 
Kikosi cha Simba ni Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Donald Musoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Awadh Juma, Amri Kiemba, Hamis Tambwe na Ramadhani Singano

Asante sana Mkuu, tunawaombea mfungwe, sitaki kuwa mnafiki. Mgambo timu, funga Simba wakae chini.
 
Yani mpaka sasa Simba bado tu?Rage must go now,atuachie Simba yetu.
 
Hao Ferrovirio de Nacala hata waje na AK47 hawawezi leta madhara yoyote nyumbani kwatu, tutawachapa mbele ya shangazi zao Yanga.
 

Al Ahly nao wanasubira kichapo cha wiki nzima"
 
Dak 16 zimekatika uwanjawa Azam Complex bado ni 0-0
 
Nawatakia kila la heri Azam katika mechi kwani mechi hiyo haina madhara kwa timu yangu. Naiombea Mgambo Shooting iifunge Simba au hata itoe sare ili tubaki salama pale juu.
Mungepatikana watu Kama nyinyi 3 tu basi angalau soccer letu lingetamba kimataifa.
 
Simba nanyi mbona mnatuchelewesha kufurahi.
 
Tetesi,dk14:Mgambo1-0Simba.
Wenye taarifa kamili watujuze tafadhi.
 
Dak. 25 Mgambo 0-0 Simba, hali bado ni shwari kama tunavyotaka.
 
Nawatakia kila la heri Azam katika mechi kwani mechi hiyo haina madhara kwa timu yangu. Naiombea Mgambo Shooting iifunge Simba au hata itoe sare ili tubaki salama pale juu.[/QUOTE]

hapo umenikuna sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…