Henge
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 6,933
- 1,514
mkapa yupo!Mkapa yupo? manake ashapiga chini hizi sherehe!
mkapa yupo!Mkapa yupo? manake ashapiga chini hizi sherehe!
mkuu isijekuwa na ushabiki umeingia kwenye hili jambo!Ukijaribu kufanya analysis utatambua kwa ujumla serikali na wananchi hawakuwa na muamko au uchangamfu ukilinganisha na sherehe zilizopita.
Kikwete hakuwa na raha kabisa labda aliogopa hata kuandaa speech akidhani CDM wangeweza kuja uwanjani na kufanya kama yale ya Dodoma.Ama inawezekana alikuwa anawaza ni kiasi gani wafadhili watachangia katika budget hasa baada ya mkulo kuchakachua.
Viongozi wengine walikuwa wapowapo tu,mfano seif na Bilal hawakuonekana kama ni mara yao ya kwanza kuhudhuria sherehe hizi kama makamu wa marais.
Kwa upande wa vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa wamepoa kabisa,uchapaji wa miguu ulikuwa legelege ukilinganisha na mwaka jana au hapo kabla.washashtuka kama serikali haina heshima ya nini iheshimiwe(hii ni hatari sana).
Vikundi vya halaiki vilijaribu bila mafanikio kutumbuiza sherehe hizi.wale watoto wapatao 700 walionekana kama walikunywa chai kikombe kimoja na ka slesi cha mkate,yaani morali nguvu na sauti vilikuwa chini kabisa.
Watangazaji wa T.V ndio walikuwa hoi kabisa utadhani wanatangaza msiba wa kitaifa,hawakujua nini cha kuongea. sijui hawakuhadiwa kifuta jasho?
Wana JF,wengi wao hawakuonekana kuchangia hapa jamvini inaelekea wengi waliamka na "Hangover" ya safari au castle.
Na hii ndio analysis ya kilichojiri kwenye sherehe zetu tukufu.TAFAKARI CHUKUA HATUA.
wapi ndugu yangu wewe, HAKUNA KITU KAMA HICHO NCHI HII!Hata mimi hizi sherehe cha maana kilichoniongezea ni siku moja ya kupmzika nyumbani. Ningefurahi kama watanzania hasa watoa habari kwa umma na viongozi wangetumia fursa hii kutuelezea wapi taifa limetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea.
Kwa nini tupo tulipo na je tumeridhishwa?
kama ndiyo, tufanyeje tuendelee kubaki tulipo?
Kama sivyo, tilifanya nini kilichotuweka hapa tulipo?
Na tufanyeje ili tutoke tulipo?
Jamani, nchi yetu ina matatizo mengi zaidi ya kwenda kushangilia risasi na gwaride. I agree, it is part of the celebration kupata uhuru kutoka kwa wakoloni. But the way we celebrated it 40 years ago should not be the same as the way we celebrate it now. walau basi, tuonyeshwe silaha wanajeshi wetu wametengeneza, mbinu mpya walizokuja nazo, etc.
It is a time to display what we have achieved so far, and discuss on what is yet to be done.
Please, tubadilikeni...
la sivyo nchi hii itafia mikononi mwetu na itakuwa aibu kubwa kwetu...