LIVE: Nape ndani ya Wapo Radio

LIVE: Nape ndani ya Wapo Radio

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,680
Reaction score
59,179
Baada ya watu kumshutumu nape kwamba amekimbia maswali aliyo kuwa akiulizwa na wasikilizaji, sasa ameamua kurudi tena kumalizia kujibu maswali yaliyo baki.

Nape alisema hataki kuulizwa maswali mengine bali anaenda kujibu vipolo vya maswali alivyo bakisha kwa mara ya mwisho alipokuwa wapo radio. Hii imekuja baada ya member wa jamii forums kulalamikia kitendo chake cha kutokujibu maswali.

So wale mlio uliza maswali kaeni mkao wa kula.

mia
 
katibu wa itikadi na uenez taifa wa chama cha mapinduzi leo saa 4 asubuh atakuwa wapo redio fm kuzungumzia mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwamo msimama wa ccm juu ya masuala ya mafuta na ges pia maon ya ccm juu ya katiba mpya.unadhan nape ana jipya?
 
Natamani kuona ccm itakavyokufa, Mungu wa Mbinguni nisaidie.

Amina
 
Solution siyo media bali serikali inapaswa kwenda kukaa meza moja na wanamtwara na watatue mgogoro wa gesi na siyo kumtuma MC wa CCM kuongea jambo zito kama hilo kwenye radio isiyofika/isiyosikika Mtwara.

Ifike wakati sasa serikali imakinike!
 
Huu ni mtego wa PANYA kwa Nape. Tuone sasa kama ATAWASALITI wananchi wa Mtwara kwaajili ya li-CCM. BTW, ninasikia ana mpango wa kugombea Jimbo mmoja la Mtwara baada ya kuona Ubungo hamuwezi Mnyika. Wana Mtwara huu ndiyo wakati wenu wa kumpina Nape.
 
Atakachokiongea ni kile kilichoko kichwani mwa kj
 
Aende mtwara akapige mkutano wa hadhara aongee utumbo kama kawaida yake aone kitakachomtokea au mbatia hakurudisha jibu?
 
Wanajamvi mda huu Nape yukop live Wapo radio akijibu maswali ya hapo kwa hapo, haya sasa wenye maswali tune Wapo radio now!
 
wamemuambia kikwete alikuja wapo radio akakimbia, na viongozi wengine wawili walikimbia. hata wewe ulipo pata dharula tukajua umekimbia!. tusamehe kwa hilo. nape anajibu ntakuwepo mpaka saa sita. mia
 
Maswali ya wapuuzi hujibiwa na wapuuzi wenzao, Nape waache hao wapuuuzi.
 
kuhusu afya elimu na rushwa vilivyo zidi inakuaje?
nape anajibu;
tatizo la rushwa lipo dunia nzima hata wakati wa mwalimu rushwa ilikuwepo. leo matukio yanaonekana ni makubwa sababu ya mabadiliko katika jamii. watu wanasema nape anaweza?..sio sawa la nape bali ni swala la kutengeneza mfumo utakao zuia watu kutoa rushwa na mifano ipo mingi. dr. mwakyembe ametoa mfano pale bandarini. walikua wanakusanya bi 40 sasa hivi wanakusanya bil 100 na kitu. mwakyembe alisema wasilipe hela cash. mia
 
nape anasema hilo la mwakyembe kutengeneza mfumo wa malipo ya bandali kufanyikia bank ni mfumo wa mwakyembe wa kupunguza rushwa. mia
 
anaulizwa kuhusu bima ya afya na ubora wa elimu.
nape nauye anajibu:
anasema tulijenga shule za secondary. tulipeleka chuo kikuu mkwawa wazalishe walimu wa haraka. safari ni hatua. ingekua serikali nyingine ingekuwa na vipaumbele vyake lakini serikali hii ya ccm ilisema tuanze kutengeneza majengo halafu tukaja kutengeneza walimu. mahitaji ya leo sio mahitaji ya kesho. mia
 
Wanajamvi mda huu Nape yupi live Wapo radio akijibu maswali ya papo kwa papo, haya sasa wenye maswali tune Wapo radio now!
 
shule1.jpg
shule2.jpg
mwambieni aache upuuzi aelezee matatizo ya watanzania na hatima yao kama anaweza vinginevyo afunge domo lake maana CCM imewafikisha kubaya watanzania miaka 51 sasa hakuna la maana zaidi ya ufisadi tu...
 
Wanajamvi mda huu Nape yupo live Wapo radio akijibu maswali ya papo kwa papo, haya sasa wenye maswali tune Wapo radio now!
 
yaani jamaa mweupe kujibu maswali...sijui sisi-emu wamemteuaje kwenye nafasi hiyo
 
Mpuuzi tu huyu! Undugu ndani ya CCM eti anaongelea CHADEMA.
 
Back
Top Bottom