LIVE: Nape ndani ya Wapo Radio

LIVE: Nape ndani ya Wapo Radio

Naona Nape anatoa data. Naona ameanza kukomaa siyo kama wakati ule anapewa uenezi.

Watoto wa wakubwa kwenye NEC hawafiki kumi - Nape Nnauye
 
mimi riziwani na mtoto wa mwinyi tu ndo tupo kwenye nec yenye watu 385. sasa hao watoto wametoka wapi? je mimi kuzaliwa kwa nauye ni dhambi?. dr ngoma watoto wake karibia wote ni madaktari. dhambi ni kubeba mtu asiye na sifa. mbona mtoto wa malecela alishindwa uchaguzi na wamwinyi pia alishindwa? anasema nape. mia
 
Mtoto wa mkunga akirithi kazi ya ukunga, si tatizo; lakini mtoto wa mwanasiasa akiingia kwenye siasa ni TATIZO
 
anaulizwa serikali ya ccm kutekeleza hadi ishinikizwe hiyo ni kweli? rais kukosa kura moja kwanini alisikitika? maandamano ya mtwara kuna gari ilikua na bendera mbona ya ccm hatukuiona? hii ya kurudisha imaani kwa wananchi si janja ya mamba kukaa mdomo wazi kitu kikiingia anabana?. mia
 
nape anajibu;
nikiwa mkuu wa wilaya ya masasi watu walikua wanasema dc utulipe sababu uchaguzi ni keshokutwa. sikuwalipa hadi uchaguzi ulipo isha. sio lazima tushinikizwe. mbona hatujashinikizwa ujenzi wa barabara za lami na mashule?. si kweli kwamba rais alikasirika kukosa kura mbili. bendera haikuwepo sababu kuna mambo haya fanywi kwa maaandamano. mkishaandamana ndo gas haitatoka mtwara?. watani zetu walitoka nje wakizani watasitisha marekebisho ya katiba. lakini hawakufanikiwa. mia
 
asante ndugu nime tune namsikiliza kama kawaida kuisifia ccm. anataka mambo ya gesi wangetuma watu wakae waongee sio kuandamana anasisitiza serikali iwahusishe wananchi kwanini manufaa ya gesi kusafirishwa na chanzo cha maandamano ni kwamba wananchi hawakuelewa vizuri mchakato wa gesi , anawaponda chadema walivyotoka bungeni kumtokumtambua rais baada ya uchaguzi,
 
nape anasema, inawezekana vyama vya siasa vilidandia tu. mimi ndo nliuliza mawaziri kwanini gas ya wanamtwara inapelekwa dar es salaam?. chanzo cha maandamano ni wananchi kutokujua na kuto kuelewa sera za gas na chama tuliwambia serikali warudi kuwaeleza lakini bado hawajaenda.
sisi tumeangalia tukaona hatuko sasa. kujikosoa na kujirekebisha ndo siraha ya mapinduzi. mwalimu alisema ccm imekuwa kama kokolo. so uchafu tuutoe. biblia inasema kama jicho lako linakusumbua litoe. kambona sif hamad kambona. mia
 
nape anasema. ccm tulianza kufukuza watovu wa nidhamu zamani. tulimfukuza mrema, kambona, seif hamad na wengine wengi hata kabla ya hawa watani zetu chadema. so sisi ndo wakwanza. mia
 
asante ndugu nime tune namsikiliza kama kawaida kuisifia ccm. anataka mambo ya gesi wangetuma watu wakae waongee sio kuandamana anasisitiza serikali iwahusishe wananchi kwanini manufaa ya gesi kusafirishwa na chanzo cha maandamano ni kwamba wananchi hawakuelewa vizuri mchakato wa gesi , anawaponda chadema walivyotoka bungeni kumtokumtambua rais baada ya uchaguzi,
Aseme ukweli nape kuna siku imewahi pita maishani mwake toka amepewa cheo ccm ipite bila kuitaja CHADEMA?
 
nape anasema:
haya mambo ya kuwapeleka mahakamani kwa kukurupuka ya watu wa epa wanaweza kukushinda ukawalipa hata hela ya kununulia vidonge so ni bora kuwajibishana kisiasa. 1995 kuna watu aliwauliza "tumekupa cheo juzi leo umekua tajiri kiasi hiki". so haya mambo yameanza zamani. mia
 
Wakuu nipeni namba ya wapo radio,naona nape anaulizwa maswali yanayompa kichwa
 
Back
Top Bottom