live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

live: Mkutano wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga

MCHONGANISHI

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2011
Posts
372
Reaction score
364
Leo kuna mkutano wa hadhara wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga katika viwanja vya mahakama nguzo 8 Majengo. Mgeni rasmi ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mh. Freeman Mbowe.

Sasa tunasubiri mkutano uanze huku tukiburudishwa na gwaride la Red Brigade.

Wakuu.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kamanda Freeman Mbowe, akiongozana na viongozi kutoka makao makuu pamoja na wabunge wa Kanda ya Ziwa Mashariki, punde wanaelekea kwenda kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Shinyanga, eneo la Nguzo nane, Mahakama ya Mwanzo, ni baada ya kikao cha ndani kilichomalizika muda mfupi uliopita.

Ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha kanda hiyo ambayo ni kati ya ngome kubwa za CHADEMA.

UPDATES:

»• Meshack Opulukwa: kama kuna mikoa inaombea na ina hamu kubwa uchaguzi mkuu ufike haraka wafanye mabadiliko makubwa kuiondoa CCM ni Shinyanga na Simiyu. Wananchi wameshachoka na kushindwa kwa CCM!

• Chombo chochote kikitumika sana kinaingia uchakavu. CCM imeshaingia uchakavu, haiwezi tena kutumika kuleta ukombozi wa maendeleo. Kwa kauli ya Pinda maana yake ni kwamba mihimili 3 haina maana kwa serikali ya CCM. Anasema chama cha magamba, chama cha wezi kimeamua kuwateketeza na kuwatelekeza wakulima wa pamba. Haiwezi tena kuwatetea. Kazi hiyo inafanza na CHADEMA, waiunge mkono.

» • Heche: mkutano mkubwa kama huu, CCM wanatumia miezi 2 kuuandaa kwa kusomba watu kutoka maeneo mbalimbali. Anazungumzia simcard tax. Anasema sasa maskini kabisa wa Tanzania atatozwa sawasawa na tajiri mkubwa kabisa wa Tanzania.

• Kwa mwaka atalipa sh. 12,000, kiasi kikubwa kuliko wakati wa kodi ya kichwa iliyoanza kufutwa Hai na Karatu, kwa sababu ya uongozi wa CHADEMA maeneo hayo kisha ikafuata nchi nzima.

• Majuzi baada ya wabunge wenu wa CHADEMA, kwenda Arusha kuomboleza na kuzika, watu wa CCM kwanza hawakujali, wakaendelea na shughuli, tofauti kbs na kawaida ya bunge, kisha wakapitisha hiyo kodi! Ndiyo maana kila siku nawaambia watanzania wenzangu, tushukuru kuwepo kwa CHADEMA na viongozi wake makini, la sivyo Watanzania wote tutauzwa!

»• Sasa kapanda Mwenyekiti. Anazungumzia kwanza, anawapatia hongera wale wote walioko kwenye mfungo wa ramadhan wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za imani yao. Anaelezea tukio la Arusha na matukio yote yaliyotokea uchaguzi wa kata 26

Updates combination chini ya Tumaini Makene itawajuza.

----------------------------

View attachment 103240

---------------------

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

Kwa hisani ya mpiga picha Pukudu na Tumaini Makene Shinyanga huko.
 
Leo kuna mkutano wa hadhara wa chadema mkoa wa shinyanga katika viwanja vya mahakama nguzo 8 majengo. Mgeni rasmi ni mwenyekiti wa CDM Taifa mh. Freeman Mbowe... Sasa tunasubiri mkutano uanze huku tukiburudishwa na gwaride la red brigade

Rushia na picha makamanda huwa wanao ushahidi na vielelezo.
 
Si ni juzi tu huyo Mbowe alikuwa Songea akifanya mkutano wa hadhara, sasa leo tena yuko Shinyanga!! Huyo jamaa huwa hachoki tu?
 
Kazi njema, na ulinzi uimarishwe. Mwenyekiti wa cdm ni zaid ya mwenyekiti
 
Kikao cha ndani ndio kinamalizika ktk hotel ya Karena afu viongoz waende uwanjani. Ntawaletea pichs ingawa chaji nehi coz kuanzia asubuhhi hakuna umeme ila najua makamanda tuko wengi
 
safi sana mboye tembea nchi nzima usichoke kabisa zunguka hata maeneo ambayo huna wabunge na madiwani na viongozi wote watembee kila mahali kutoe elimu kwa wananchi waache kulala sasa
 
Si ni juzi tu huyo Mbowe alikuwa Songea akifanya mkutano wa hadhra, sasa leo tena yuko Shinyanga!! Huyo jamaa huwa hachoki tu?

Ukombozi wa Mkoloni ambaye ni Mwafrika Unagharama hautafutwi kwa kuweka vidole na miguu juu. Ni kwa bidii na nguvu kama afanyavyo huyo kamanda.
 
mh. MboWe, Kasulumbay, Opurukwa na Heche watakuwepo ndio wanaingia. Hivi kwenye Nokia E63 unaupload picha vipi??
 
Mwenyekiti wa chadema taifa pamoja na wabunge wa kanda ya ziwa leo wanafanya uzinduzi wa kanda ya ziwa mashariki katika viwanja vya mahakama ya mwanzo vilivyopo shinyanga mjini.
 
unafikiri huyo ni gamba? Magamba yakifanya ata kikao huwa wanaomba likizo eti wanaenda kupumzika wamechoka sana
Haaaah!! Imebidi nicheke sana. Hata mwenyekiti wetu wa CCM huwa anafanya vikao (mikutano!!) vingi sana bila kuchoka bahati mbaya sana anafanya hayo akiwa ughaibuni wakati wa ziara zake za nchi za nje.
 
Wakuu.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kamanda Freeman Mbowe, akiongozana na viongozi kutoka makao makuu pamoja na wabunge wa Kanda ya Ziwa Mashariki, punde wanaelekea kwenda kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Shinyanga, eneo la Nguzo nane, Mahakama ya Mwanzo, ni baada ya kikao cha ndani kilichomalizika muda mfupi uliopita.

Ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha kanda hiyo ambayo ni kati ya ngome kubwa za CHADEMA.

UPDATES:

»• Meshack Opulukwa: kama kuna mikoa inaombea na ina hamu kubwa uchaguzi mkuu ufike haraka wafanye mabadiliko makubwa kuiondoa CCM ni Shinyanga na Simiyu. Wananchi wameshachoka na kushindwa kwa CCM!

• Chombo chochote kikitumika sana kinaingia uchakavu. CCM imeshaingia uchakavu, haiwezi tena kutumika kuleta ukombozi wa maendeleo. Kwa kauli ya Pinda maana yake ni kwamba mihimili 3 haina maana kwa serikali ya CCM. Anasema chama cha magamba, chama cha wezi kimeamua kuwateketeza na kuwatelekeza wakulima wa pamba. Haiwezi tena kuwatetea. Kazi hiyo inafanza na CHADEMA, waiunge mkono.

» • Heche: mkutano mkubwa kama huu, CCM wanatumia miezi 2 kuuandaa kwa kusomba watu kutoka maeneo mbalimbali. Anazungumzia simcard tax. Anasema sasa maskini kabisa wa Tanzania atatozwa sawasawa na tajiri mkubwa kabisa wa Tanzania.

• Kwa mwaka atalipa sh. 12,000, kiasi kikubwa kuliko wakati wa kodi ya kichwa iliyoanza kufutwa Hai na Karatu, kwa sababu ya uongozi wa CHADEMA maeneo hayo kisha ikafuata nchi nzima.

• Majuzi baada ya wabunge wenu wa CHADEMA, kwenda Arusha kuomboleza na kuzika, watu wa CCM kwanza hawakujali, wakaendelea na shughuli, tofauti kbs na kawaida ya bunge, kisha wakapitisha hiyo kodi! Ndiyo maana kila siku nawaambia watanzania wenzangu, tushukuru kuwepo kwa CHADEMA na viongozi wake makini, la sivyo Watanzania wote tutauzwa!

»• Sasa kapanda Mwenyekiti. Anazungumzia kwanza, anawapatia hongera wale wote walioko kwenye mfungo wa ramadhan wakitekeleza moja ya nguzo muhimu za imani yao. Anaelezea tukio la Arusha na matukio yote yaliyotokea uchaguzi wa kata 26

Updates combination chini ya Tumaini Makene itawajuza.
 
Last edited by a moderator:
Watz wawe makini na tindikali huko
Wewe na CCM wenzio endeleeni kushangaa shangaa huoni kuwa hiyo MOVIE ya Tindikali imeshindwa? Muulize Mwigu pamoja na kutembea na na yule jamaa mlomwalibu uso Igunga ni nini kimeitokea CCM Arusha? Makamanda wako kazini Leo Mbowe Shinyanga kesho Mnyika Dr Slaa Lisu nk Wako Mabibo SaharaDar wanawasha moto. Godless Lema Sugu Msigwa na Sirinde kesho wanaunguruma Mbeya Mtajutaaaaaa!
 
Back
Top Bottom