Maswali yanaendelea.................
9. Elizabeti Mashawa, Loyola High School, Form V: Enzi za zamani ilikuwa ni rare kwa watu kufa njaa, Je, kama Nyerere alifanya watu wakajitegemea, viongozi wetu wanatumiaje mikakati ya Nyerere ili kujitegemea kuliko kutegemea nchi za nje?
10. Mwalimu aliondoka lakini hakuondoka na mambo yake, wapo watu ambao alifanya kazi nao wapo mpaka sasa. Katika Azimio Arusha kuna mambo yaliyotiliwa mkazo, km kujitegemea. Wale ambao walikuwa wanafanya kazi na Mwalimu inawezekana kwamba waliomzika waliweka jiwe kubwa ili kama angefufuka basi afufukie baharini na sio Tanzania. Sasa hivi kuna migogoro ya ardhi mahali mbalimbali lakini wazee hawafanyi chochote. Wasomi ndio wanaoiangamiza Tanzania ijayo maana ukimuuliza msomi sasa hivi ukimaliza masomo ataenda kufanya nini atakwambia kwamba ataenda kujikusanyia maana kila mtu anachukua chake mapema. Tuache ngonjera kupambana na rushwa.
11. Christopher Ole Sendeka, Mfugaji, Mwakilishi wa Wananchi Jimbo la Simanjiro: Katika Ilani za Uchaguzi tumekuwa tunaweka mambo mbalimbali ya kuyatekeleza. Tukichukua suala la Ardhi, maelfu ya ekari kupitia mambo ya madini na kilimo, kupitia wageni. Hoja iliyopo ni kuangalia yaliyo mbele yetu. Mwalimu hakuwa vuguvugu, kama kuna jambo lililohitaji kuwa na ujasiri alisimama imara. Naomba kupata mawazo kutoka kwa Prof Shivji na Kingunge mnachukua hatua gani...
12. Joseph Emanuel: Tukae kimya kwa dk moja kumkumbuka Mwalimu (wote wakakaa kimya). Katika nchi ya Tanzania tulitakiwa tuishi kijamaa, taifa lenye misingi ya kupendana, lakini viongozi wa Serikali wanaongea bila kuangalia tufuate misingi ipi. Mwalimu alisema kwamba ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Sasa hivi hakuna uongozi bora. Tunaposema KILIMO KWANZA, An Agriculture Revolution is not an overnight event, tukae na wananchi tuwaulize kwamba wanahitaji nini...