Live kutoka bungeni; Kingwangwala aitisha resolute

Live kutoka bungeni; Kingwangwala aitisha resolute

canaan

Member
Joined
Mar 1, 2008
Posts
46
Reaction score
6
Anasema serikali isipochukua hatua wananchi wa nzega watafunga mgodi
 
Anasema ni wezi wanaiibia nchi, nibora tubaki na madini ardhini kuliko tuwaachie watu watuibie
 
Anasema mkataba kati ya mgodi na serikali unamadudu mengi
 
Atafungwa bakuli kesho tu.....ubunge wenyewe amepewa 4 grant
 
Anaiomba serikali isitishe uwekezaji kwenye madini
 
Anasema ripoti za kina Tundu lisu kuhusu migodi zinatisha, hakuna uzalendo kwa viongozi wa nchi hii
 
Ameongea mambo mengi ambayo hayako organised ndio maana ameshindwa kiconclude mchango wake!
 
Ila ameongea point, japokuwa amechakachua matokeo. Anabifu na ngeleja nin? Mbona amemsema sana.
 
Tumpe sifa wakuu amewaongelea watanzania angalau kwa leo.
 
Anasema serikali isipochukua hatua wananchi wa nzega watafunga mgodi
Sio kila upuuzi lazima utuwekee thread hapa!!Huyu mnafiki tumesha mjadili sana hapa kwenye forum. Juzi hapa alikuwa anawatetea Wawekezaji kisa mbunge wa Cdm kaongea leo anawaponda nani atamwelewa.
 
Nashangaa sasa hivi, anapinga alichounga mkono juzi na last week alipopitisha budget! Si yeye tu Ole Sendeka na Komba naye kapinga mashangingi.

Swali, je nao wanatafuta umaarufu, au wameanza kuguswa na matatizo ya nchi hii?
 
Nafikiri ameona jinsi gani anavyopoteza nafasi ya kurudi bungeni!
 
Anasema ripoti za kina Tundu lissu kuhusu migodi zinatisha, hakuna uzalendo kwa viongozi wa nchi hii
Huyu bwana nashindwa kumuelewa, siku Tundu Lisu aliposimama kidedea kupinga mikataba mibovu ya madini yeye alikuwa anampinga kiushabiki hadi zile hoja mbovu zikapita kwa "ndiooooooooo ........sioooooo". Leo anaongea huku akitaka hata kulia akirejelea yale yale aliyokuwa naongea Lissu. Mimi bado najiuli: hivi huyu bwana alikuwa anampinga Lissu kwa ushabiki tu wa CCM au alipinga kwa kutojua.
 
Jibu alilompa T.Lissu siku ile alipounga mkono hoja ya msamaha wa kodi kwa wawekezaji nililipenda sana. Mnafiki tu huyu!
 
Back
Top Bottom