News Alert: Live From BOT: KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA


Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
27,251
Likes
30,217
Points
280
Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2008
27,251 30,217 280
Wanabodi,

Niko kwenye ukumbi wa BOT hapa jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika kongamano kubwa la kibiashara kati ya India na Tanzania ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.


clip_image002.gif


clip_image004.gifclip_image006.gif


INDIAN BUSINESS FORUM

TANZANIAclip_image008.gif
clip_image010.gif
TAARIFA KWA UMMA

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA

Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la Kongamano hili ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha wafanyabiashara kutoka katika sekta zifuatazo: Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara. Makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi tano za juu kiuwekezaji hapa nchini (kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji). Kulingana na takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, Kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2.122. Miradi inayoongoza katika kusajiliwa na TIC katika kipindi hicho ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53% ni miradi ya kutoka sekta hii.

Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unashiriki ila idadi kubwa ni wafanyabiashara Watanzania wenzetu wenye asili ya India.

Kwa sasa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, ndio anahutubia.

Fuatana nami.

Paskali
 

Forum statistics

Threads 1,237,817
Members 475,675
Posts 29,302,101