LIVE: Barca VS Bavaria...the last kick of dying horse...

Gang Chomba

Platinum Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,734
Reaction score
4,871
KILABU cha Barca leo kinaingia katika Dimba lake la Nou Camp kwenda pambana na KLABU ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchutama mara 4 katika Dimba la Alianz Arena pale Munich wiki moko ilopita Barca wanajaribu kuja kufanya mchezo wa Soka uonekane mchezo wa miujiza, hasa ukizingatia wanahitaji la kupata takriban magoli manne ili mtanange huo uzidishiwe muda ama magoli 5-0 ili wapate kuingia moja kwa moja katika fainali pale Wembley.

Bayern ni timu iliokamilika kila Idara tofauti na Barcelona ambayo ukuta wao umekuwa ukifananishwa na ukuta wa Kariakoo Lindi au hata wa Mji Mpwapwa.

Nanga itapaa saa 2145hrs kwa saa za Africa ya Mashariki.
 
leo Barca nae anaondoka,Kina Frank hawana mchezo
 
1st legg Barca walikimbizwa muda wote wa mchezo na hata kupelekea yule mwanasoka bora wa jumuiya ya FIFA kujisingizia ugonjwa ambao alishapona zaamaaani.

Wazungu ni watu makini ambao hupenda kufanya vitu vyao kwa akili pasipo kukurupuka. Huyu bwana kama angekuwa mgonjwa wiki ilopita basi asingepewa ruhusa ya kukanyaga uwanjani.
Mara kadhaa tumesikia mchezaji flani hachezi eti kwa kuwa tu ana FLU...
Sasa iweje huyu bwana asiwe fit 100% then apewe nafasi ya kutimbwilika uwanjani?

Haya ni madhara ya kumtengeneza mchezaji mpaka kuwa overrated...
Ni wazi kuwa huyu kisebengo alikamatwa na hakuweza kufurukuta, hivyo kwa kujikomba na kujikosha pasipokuwa na haya ndo akajishaua kuja na porojo ati alikuwa mgonjwa na hakuwa fit 100%.
 
KILABU cha Barca leo kinaingia katika Dimba lake la Nou Camp kwenda pambana na KLABU ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchutama mara 4 katika Dimba la Alianz Arena pale Munich wiki moko ilopita Barca wanajaribu kuja kufanya mchezo wa Soka uonekane mchezo wa miujiza, hasa ukizingatia wanahitaji la kupata takriban magoli manne ili mtanange huo uzidishiwe muda ama magoli 5-0 ili wapate kuingia moja kwa moja katika fainali pale Wembley.

Bayern ni timu iliokamilika kila Idara tofauti na Bayern ambayo ukuta wao umekuwa ukifananishwa na ukuta wa Kariakoo Lindi au hata wa Mji Mpwapwa.

Nanga itapaa saa 2145hrs kwa saa za Africa ya Mashariki.

Mkuu naona kuna makosa kidogo ya kiuandishi katika aya ya pili kutoka mwisho. Siwezi ku ya bold natumia kam china
 
Mkuu hapo red fanya editing... Barcelona leo wataingia wakiwa hawana cha kupoteza kwani tayari wameshapoteza kwa 95%. Barca leo wate watafanya hujuma kuanzia dk ya 1 mpk 90. Natabiri barca wakipata goli ndani ya dk 20 za mwanzo, tutarudisha goli zote 4 na bayern kuutafuta mpira kwa tochi. Tukutane hiyo 2145
 
Mkuu naona kuna makosa kidogo ya kiuandishi katika aya ya pili kutoka mwisho. Siwezi ku ya bold natumia kam china

Hayo masahihisho unayoyasema ndo hayo alioyazungumzia pia 072?
Kama ndo hayo siyaombei radhi ng'o, kwani uongo?
 
Mkuu natumia kamchina sasa ila aya hii ndo ina makosa

................................................................................

Bayern ni timu iliokamilika kila Idara tofauti na
Bayern ambayo ukuta wao umekuwa
ukifananishwa na ukuta wa Kariakoo Lindi au hata
wa Mji Mpwapwa.
....................................................................................

Mstari wa kwanza na wa pili ndo unamakosa hebu soma kwa umakini
 
KILABU cha Barca leo kinaingia katika Dimba lake la Nou Camp kwenda pambana na KLABU ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchutama mara 4 katika Dimba la Alianz Arena pale Munich wiki moko ilopita Barca wanajaribu kuja kufanya mchezo wa Soka uonekane mchezo wa miujiza, hasa ukizingatia wanahitaji la kupata takriban magoli manne ili mtanange huo uzidishiwe muda ama magoli 5-0 ili wapate kuingia moja kwa moja katika fainali pale Wembley.

Bayern ni timu iliokamilika kila Idara tofauti na Bayern ambayo ukuta wao umekuwa ukifananishwa na ukuta wa Kariakoo Lindi au hata wa Mji Mpwapwa.

Nanga itapaa saa 2145hrs kwa saa za Africa ya Mashariki.

Aseee, nilikua tizi ila akili yote ilikua huku na nilivyoona tu hii heading, "the last kick of a dying horse" nikacheeekaaa na nikahisi ni wewe tu.
Sasa Mzee mwenzangu huoni kama huyu dying horse anaweza akaokota rozali msikitini kama RM jana almanusura maji yakwee kilima, ile match yao ya marudiano na Arsenal kwenye knock out stages, wakiwa kwao inanifanya niwe 50/50 na matokeo ya leo though they have the upper hand ukichukulia huo ukuta wa mji mpwampwa wanaoutumia unaweza kuwacost kwa kweli kwa kina Mandzukic.
 
Ngumu sana kwa Barca soma zaidi hapa

Kwa hali ilivyo matumaini ya Barcelona kufika fainali ya kombe la Mabingwa wa Ulaya ni madogo sana.

Lazima wafunge magoli matano bila majibu dhidi ya washindani wagumu waliokwishabeba ubingwa wa ligi (Bundesliga) iliyo na ushindani mkubwa, na iliyojaza wachezaji nyota wenye uzoefu mkubwa. Hapa Barcelona itahitaji kutumia mbinu zao zote, lakini watahitaji bahati

Pengine ni mapema mno kusema vilabu ya Ujerumani ni vigogo wapya wa soka ya Ulaya, nategemea kuwa mwaka kesho timu za La Liga zitarudi na usongo mkubwa zaidi, lakini ni dhahiri kwamba Bayern Munich ni moja ya timu itakayokuwepo kati ya timu za kuogopwa.

Tangu mwanzo wa ligi hii ya Mabingwa watu wengi waliwatabiria vijana hawa wa Heynckes Jupp kushinda Ligi ya Mabingwa msimu huu, lakini matokeo ya wiki iliyopita katika uwanja Allianz yameongeza imani ya wengi juu ya uwezekano huu, huku wanaoipenda Barca wakiombea muujiza Camp Nou.

Nilitarajia Bayern Munich - ambao wamepoteza tu mara mbili nyumbani msimu huu, dhidi Bayer Leverkusen katika Bundesliga na dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa - kuelekea Nou Camp na ushindi mwembamba wa goli moja au mawili. Hivyo kuwa na mabao manne ni kitu kilichostua ulimwengu wa soka, na walistahili kabisa kwa jinsi walivyocheza, walivyoifanya timu ya Barcelona, inayocheza soka la kuvutia, na inayotajwa kuwa ni Klabu nzuri kuliko zote zilizowahi kuwepo, ionekane ya kawaida sana.

Siri ya Mafanikio ni Kocha
Wengi watataja wachezaji mahiri kama Ribery Franck, Arjen Robben, Thomas Muller na wenzao kama siri ya ushindi, lakini Uongozi wa kocha Jupp Heynckes, ambaye yu katika siku za mwisho za mkataba wake Bayern, ni siri kubwa ya mafanikio haya.

Tunazungumzia mengi juu ya umahiri wa makocha maarufu kama Sir Alex Ferguson, Jose Mourinho na Pep Guardiola - ambaye ataifundisha Bayern kuanzia majira ya joto baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu - lakini Heynckes yuko juu pia licha ya kusahaulika.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 alishaiongoza Real Madrid kuchukua Kombe la Ligi ya Mabingwa mwaka 1998, Bayern kwa taji la Bundesliga mwaka 1989 na 1990, na sasa, katika awamu yake ya tatu ya kufundisha Munich, ana uwezekano wa kutwaa na timu yake mataji matatu la Ligi, Kombe la Ujerumani na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Unaweza kusema kwamba itakuwa namna nzuri kwa Heynckes kukamilisha kazi yake, kwani anasemekana kutaka kustaafu kufundisha soka mwisho wa msimu. Wengi wanajiuliza kwa nini ustaafu wakati ndio unafikia kilele cha mafanikio ya kazi yako?

Kuna Klabu nyingi kubwa zinatafuta makocha wazuri, na bila shaka Heynckes atatakwa sana kujiunga nao, kutokana na uzoefu na mafanikio yake ambayo yanafanya CV yake kuwa kali.

CV ya Heynckes itaimarishwa kwa angalau kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa; Barcelona ina wachezaji wazuri sana na iko vizuri ki-timu, na kama timu yoyote inaweza kusonga mbele ikiwa nyuma kwa magoli manne, kwa sasa timu hiyo ni Barcelona, na bila shaka watatafuta magoli mawili ya mapema.

Lakini Bayern ni imara pia, wana kila ubora gani unaoweza kuutarajia katika timu - kasi, nguvu, akili, vipaji binafsi – ni wagumu kwa aina yoyote ya wapinzani wakiwa na Bastian Schweinsteiger mwenye uwezo mkubwa wa kuunganisha washambuliaji mbele yake.

Lakini tujikumbushe, Bayern Munich ilitarajiwa kushinda kirahisi dhidi ya Arsenal katika mzunguko wa timu 16 za mwisho, baada ya kushinda mechi ya kwanza katika Emirates 3-1 lakini hatimaye kupigwa 2-0 nyumbani na Gunners na wangeweza hata kufungwa bao la tatu. Hili ndilo linaweza kuwatia moyo Barcelona.

Ukienda katika mchezo wa marudiano na magoli mengi na usipoanza vizuri inaweza kuwa ni vigumu sana kwa timu kutulia na kulinda ushindi, lakini ukiangalia nguvu za kimwili, ufundi, kasi na uzoefu wa Bayern, naona uwezekano mdogo sana wa kupoteza kwa magoli matano.

Hawaendi kujihami ndani ya eneo lao la 18 na badala yake kucheza mpira wa kasi yao nitashangaa kama Bayern hawatapata walau bao moja kule.
 
Aseee, nilikua tizi ila akili yote ilikua huku na nilivyoona tu hii heading, "the last kick of a dying horse" nikacheeekaaa na nikahisi ni wewe tu.
Sasa Mzee mwenzangu huoni kama huyu dying horse anaweza akaokota rozali msikitini kama RM jana almanusura maji yakwee kilima, ile match yao ya marudiano na Arsenal kwenye knock out stages, wakiwa kwao inanifanya niwe 50/50 na matokeo ya leo though they have the upper hand ukichukulia huo ukuta wa mji mpwampwa wanaoutumia unaweza kuwacost kwa kweli kwa kina Mandzukic.

Aaah utakuwa mjinga wakati wa kwenda...lakini wakati wa kurudi mpaka Chocho utakuwa ushazinyaka.
So usitegemee ya Arse8 yajirudie leo.
 
Barca bila Messi ni kama story ya wana wa Israel wakiwa jangwani( trailing by 4 goals) bila Mussa
 
kifo cha Mbwa huanzia puani.
Sasa pua zilishakufa tangu Alianz Arena...
Whats next?
 
KILABU cha Barca leo kinaingia katika Dimba lake la Nou Camp kwenda pambana na KLABU ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchutama mara 4 katika Dimba la Alianz Arena pale Munich wiki moko ilopita Barca wanajaribu kuja kufanya mchezo wa Soka uonekane mchezo wa miujiza, hasa ukizingatia wanahitaji la kupata takriban magoli manne ili mtanange huo uzidishiwe muda ama magoli 5-0 ili wapate kuingia moja kwa moja katika fainali pale Wembley.

Bayern ni timu iliokamilika kila Idara tofauti na Barcelona ambayo ukuta wao umekuwa ukifananishwa na ukuta wa Kariakoo Lindi au hata wa Mji Mpwapwa.

Nanga itapaa saa 2145hrs kwa saa za Africa ya Mashariki.

Am almost spearing my all two eyes on screen, cant wait to see Barcelona passing this hard mountain.
 
Messi bench, atakuwa anajamba jamba pale bench kama ile mech vs PSG
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom