Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Kwa hali ilivyo matumaini ya Barcelona kufika fainali ya kombe la Mabingwa wa Ulaya ni madogo sana.
Lazima wafunge magoli matano bila majibu dhidi ya washindani wagumu waliokwishabeba ubingwa wa ligi (Bundesliga) iliyo na ushindani mkubwa, na iliyojaza wachezaji nyota wenye uzoefu mkubwa. Hapa Barcelona itahitaji kutumia mbinu zao zote, lakini watahitaji bahati
Pengine ni mapema mno kusema vilabu ya Ujerumani ni vigogo wapya wa soka ya Ulaya, nategemea kuwa mwaka kesho timu za La Liga zitarudi na usongo mkubwa zaidi, lakini ni dhahiri kwamba Bayern Munich ni moja ya timu itakayokuwepo kati ya timu za kuogopwa.
Tangu mwanzo wa ligi hii ya Mabingwa watu wengi waliwatabiria vijana hawa wa Heynckes Jupp kushinda Ligi ya Mabingwa msimu huu, lakini matokeo ya wiki iliyopita katika uwanja Allianz yameongeza imani ya wengi juu ya uwezekano huu, huku wanaoipenda Barca wakiombea muujiza Camp Nou.
Nilitarajia Bayern Munich - ambao wamepoteza tu mara mbili nyumbani msimu huu, dhidi Bayer Leverkusen katika Bundesliga na dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa - kuelekea Nou Camp na ushindi mwembamba wa goli moja au mawili. Hivyo kuwa na mabao manne ni kitu kilichostua ulimwengu wa soka, na walistahili kabisa kwa jinsi walivyocheza, walivyoifanya timu ya Barcelona, inayocheza soka la kuvutia, na inayotajwa kuwa ni Klabu nzuri kuliko zote zilizowahi kuwepo, ionekane ya kawaida sana.
Siri ya Mafanikio ni Kocha
Wengi watataja wachezaji mahiri kama Ribery Franck, Arjen Robben, Thomas Muller na wenzao kama siri ya ushindi, lakini Uongozi wa kocha Jupp Heynckes, ambaye yu katika siku za mwisho za mkataba wake Bayern, ni siri kubwa ya mafanikio haya.
Tunazungumzia mengi juu ya umahiri wa makocha maarufu kama Sir Alex Ferguson, Jose Mourinho na Pep Guardiola - ambaye ataifundisha Bayern kuanzia majira ya joto baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu - lakini Heynckes yuko juu pia licha ya kusahaulika.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 alishaiongoza Real Madrid kuchukua Kombe la Ligi ya Mabingwa mwaka 1998, Bayern kwa taji la Bundesliga mwaka 1989 na 1990, na sasa, katika awamu yake ya tatu ya kufundisha Munich, ana uwezekano wa kutwaa na timu yake mataji matatu la Ligi, Kombe la Ujerumani na Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Unaweza kusema kwamba itakuwa namna nzuri kwa Heynckes kukamilisha kazi yake, kwani anasemekana kutaka kustaafu kufundisha soka mwisho wa msimu. Wengi wanajiuliza kwa nini ustaafu wakati ndio unafikia kilele cha mafanikio ya kazi yako?
Kuna Klabu nyingi kubwa zinatafuta makocha wazuri, na bila shaka Heynckes atatakwa sana kujiunga nao, kutokana na uzoefu na mafanikio yake ambayo yanafanya CV yake kuwa kali.
CV ya Heynckes itaimarishwa kwa angalau kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa; Barcelona ina wachezaji wazuri sana na iko vizuri ki-timu, na kama timu yoyote inaweza kusonga mbele ikiwa nyuma kwa magoli manne, kwa sasa timu hiyo ni Barcelona, na bila shaka watatafuta magoli mawili ya mapema.
Lakini Bayern ni imara pia, wana kila ubora gani unaoweza kuutarajia katika timu - kasi, nguvu, akili, vipaji binafsi – ni wagumu kwa aina yoyote ya wapinzani wakiwa na Bastian Schweinsteiger mwenye uwezo mkubwa wa kuunganisha washambuliaji mbele yake.
Lakini tujikumbushe, Bayern Munich ilitarajiwa kushinda kirahisi dhidi ya Arsenal katika mzunguko wa timu 16 za mwisho, baada ya kushinda mechi ya kwanza katika Emirates 3-1 lakini hatimaye kupigwa 2-0 nyumbani na Gunners na wangeweza hata kufungwa bao la tatu. Hili ndilo linaweza kuwatia moyo Barcelona.
Ukienda katika mchezo wa marudiano na magoli mengi na usipoanza vizuri inaweza kuwa ni vigumu sana kwa timu kutulia na kulinda ushindi, lakini ukiangalia nguvu za kimwili, ufundi, kasi na uzoefu wa Bayern, naona uwezekano mdogo sana wa kupoteza kwa magoli matano.
Hawaendi kujihami ndani ya eneo lao la 18 na badala yake kucheza mpira wa kasi yao nitashangaa kama Bayern hawatapata walau bao moja kule.