LIVE: Arsenal VS Bayern Munchen...

LIVE: Arsenal VS Bayern Munchen...

Gang Chomba

Platinum Member
Joined
Feb 29, 2008
Posts
20,734
Reaction score
4,869
Arsenal inaingia Dimbani leo kupambana na ngoma ngumu barani Uropa yaani Bayern Munich kutoka Bavaria Ujerumani.

Arsenal ikiwa na kumbukumbu mbaaya zaidi kwa kutolibeba kombe la klabu Bingwa Barani Ulaya, inaingia dimbani ikiwa haipewi nafasi yoyote ya kuweza kufanya vyema na kuingia hatua ya robo fainali kiasi kwamba wachambuzi wa maswala ya Soka wametanabaisha kuwa hata mechi zote mbili zingalichezwa uwanjani Emirates basi Arsenal wangeyaaga mashindano.

Bayern wanaingia uwanjani wakiwa wamekamilika kila Idara. Wana kocha mzuri, wana kocha mtarajiwa mzuri pia.
Wana wachezaji weengi wa kiwango cha juu tofauti na kilabu cha Arsenal.

DID YOU KNOW?
Arsenal and Bayern Munich have met four times before in the Champions League, with the Gunners
victorious just once.
Their last meeting was also at the Champions
League last-16 stage, which the German side won
3-2 on aggregate in 2004-05.

Olivier Giroud has four assists in the group stages of
the Champions League this season; only Zlatan
Ibrahimovic has more with five.

Lukas Podolski has scored three goals from three
shots on target in the Champions League this term. He is 17/2 to score the first goal in the game
with BetVictor.
Bayern Munich had the most different goalscorers in the group stage, with nine.
The German side also conceded the fewest shots on
target in the group stage, with just 17 against. TThe Bavarians last won in England in April 2001,
with a 1-0 quarter-final victory over Manchester
Utnited on course to winning the tournament. Mario Gomez (mnyama) has scored 25 goals
in 26 Champions League starts.

Gang Chomba Prediction...
Arsenal 1-3 Bayern Munich

Ofisi zangu za utabiri zipo Magogoni...
 
Gang Chomba
Mimi huwa sinunui hizi historia. Ni kelele tu za kuuza habari wala hazina mantiki yeyote ile. Timu zinabadilika kila mwaka wa usajiri.

Kwenye karatasi, Bayern Munchen wanaonekana wako bora zaidi ya Arsenal lakini mpira sivyo hivyo. Juzi juzi kashindano ya Africa Cup of Nation yamedhihirisha hivyo.

Cha muhimu ni kusubiri hizo dakika 180 ambazo zitatoa jibu mbadala.
 
Last edited by a moderator:
Hata ujae vp hauwezi kudunda Baharini...
miujiza ya mwisho ni ile ya yule mzee wa Loliondo ambaye juzi kati ameonekana anatoka pharmacy kununua mkojo wa Punda
Ahahahahah..mkuu kwani gemu la leo linachezwa baharini?We subiri tu uone Gooners watakavyoishangaza dunia.
 
Gang Chomba
Its true Arsenal wanakimbembe against the bavarians, ila sidhani ni kwa usiku huu wa leo, naamini leo tutaona kandanda la hali ya juu na a balanced match na matokeo can go either way.
ila kwa returned leg mambo yanaweza kuwa mabaya kidogo but mind u that, Munich huwa wanapata shida sana na team za England, kumbuka ya mwaka jana!
 
Hata ujae vp hauwezi kudunda Baharini...
miujiza ya mwisho ni ile ya yule mzee wa Loliondo ambaye juzi kati ameonekana anatoka pharmacy kununua mkojo wa Punda

Hahahahahahaaa, Chombaaaa!
 
Ushindi leo bila wasi wasi.

Tukianza na kasi tunauwezo wa kuwafunga, lakini kama tutaanza kwa kusinzia kusubiri mpaka tufungwe ndio tuamke tutajuta
 
Ahahahahah..mkuu kwani gemu la leo linachezwa baharini?We subiri tu uone Gooners watakavyoishangaza dunia.

tatizo sio kuishangaza Dunia...
Tatizo ni kuwa ushindi wa Arsenal ni finyu sawa na Bata kumeza Boga...
Kitu ambacho hakiwezekani
 
Ushindi leo bila wasi wasi.

Tukianza na kasi tunauwezo wa kuwafunga, lakini kama tutaanza kwa kusinzia kusubiri mpaka tufungwe ndio tuamke tutajuta

Mpira ungekuwa ni kasi basi wamarekani wangekuwa mabingwa.
Wangewatumbukiza akina Tim Montigomery, Justin Gatlin, Shawn Clawford, Michael Johnson, John Drumond, Morris Green, Tyson Gay na nguli wengine...
 
Kuishabikia Arsenal unaweza kupata vidonda vya tumbo, ila kwenye football 1+1 inaweza kuwa =3

Timu za Uingereza zinapokuwa kwenye UEFA games huwa ni tofauti sana.
 
Mimi namuangalia afro Dante,Javi Martinez,Robben,Gomez,Ribbery,Lahm,Bastian,Kroos,Mandzukic,Alaba Sungura,Muller,Shaqili,nk leo maana haya majina tu na kasi yao sijui Koncielyn leo asiwe na mapepe akajifunga,ila emirates Arsenal nafasi wanayo,kimbembe kule Munich,maana hata Chelsea ilikuwa dhali lao,walikubali kucheza kama defensive kama minnows(vibonde)
 
Mpira ungekuwa ni kasi basi wamarekani wangekuwa mabingwa.
Wangewatumbukiza akina Tim Montigomery, Justin Gatlin, Shawn Clawford, Michael Johnson, John Drumond, Morris Green, Tyson Gay na nguli wengine...

Reggae boyz wangekuwa mabingwa, Usain Bolt, Asafa Powell, Yohan Blake, Nesta Carter na nguli wengine.
 
Bayern defence yao sio nzuri so cha msingi ni Arsenal kutengeneza nafasi na kuzitumia maana game ya pili kule Munich itakuwa ngumu sana kwa Arsenal
 
Bayern defence yao sio nzuri so cha msingi ni Arsenal kutengeneza nafasi na kuzitumia maana game ya pili kule Munich itakuwa ngumu sana kwa Arsenal

Mkuu nafikiri haufuatilii kwa karibu Bundesliga. Msimu huu wa ligi, Byaern wafungwa magoli 7 tu katika mechi 22! Utapata wapi defence nzuri zaidi ya hiyo Ulaya?
 
Mkuu nafikiri haufuatilii kwa karibu Bundesliga. Msimu huu wa ligi, Byaern wafungwa magoli 7 tu katika mechi 22! Utapata wapi defence nzuri zaidi ya hiyo Ulaya?

Teh teh JF ndo napoipendea...
Inakulazimu kabla ya kuandika uchunguze kwanza.
Enhee Peasant kamanda lete utamu
 
Reggae boyz wangekuwa mabingwa, Usain Bolt, Asafa Powell, Yohan Blake, Nesta Carter na nguli wengine.

Dah big G ninayo ila mate yamekauka...
Haya sheikh...kila la kheri na Reggae Boys wako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom