DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,674
Nimetafakari sana na kuona tunahitaji kikosi kazi kitakacho mshauri Rais jinsi ya kulivusha Taifa,katika kipindi hiki kinachohitaji busara kubwa sana.kwani Siku za nyuma Watanzania walipopita kwenye kipindi kama hiki Baba wa Taifa kwa uwezo binafsi [Personal or individual skills] kama ni Mchezo wa mpira wa mguu ni kiwango cha mchezaji mmoja kuwa na uwezo mahiri wa kucheza zaidi ya wenzie katika timu, mfano wake ni kama Pelle,Maradona na zama za kina JJ Okocha, na Ronaldo de Lima,kwa kiwango cha sasa tunasema Messi.
Lakini kuna ubishi unaendelea kuwa Ronardo De Lima ni mzuri zaidi ya Messi kwa zama ma enzi zake.Kwa hilo mimi nakubaliana nao wote wanaokubali Ronaldo ni mzima kwenye mchezo wa soka kwenye zama zake, kuliko Messi wa sasa kwa kulingana na mazingira na nyakati zetu za sasa,kulinganisha na mazingira ya Ronaldo ya zama hizo.Uwezo wa Ronaldo kucheza na mabeki wenye misuri mizito duniani wakati huo nabado akaweza kupenya na kutikisa nyavu basi ni mcheza bora zaidi ya kiwango cha Messi cha sasa.Vivyo hivyo katika siasa za nyumbani Tanzania Mwalimu kwa zama zake,ukilinganisha na watawala wetu wa sasa kiwango cha Mwalimu kwa Taifa hili ni sawa na Pelle japo wapo wakina Messi wa leo katika siasa za sasa.Na Messi amezaliwa akakua na kujua kuwa hata acheze vipi bado hatomfikia Pelle mfalme wa Soka.
Kwenye siasa zetu hapa nyumbani tunaitaji wakina Ronaldo kuhimili mikiki ya misuko suko kulingana na zama na nyakati tulizo nazo kwa sasa.Na kulivusha Taifa kama Mwalimu alivyoweza kupitia hatihati hizo nabado akalivusha Taifa toka kwenye majaribu hayo.Hivyo nakubali Mwalimu kwa zama hizo na alikua na kiwango cha juu wakati huo cha kuwavusha Watanzania katika kuelewa siasa na maswala mazima ya maendeleo yao kama Taifa,ukilinganisha na zama hizi tulizo nazo [Pelle v/s Messy].
Maamuzi ya kitaifa na kimataifa mara nyingi yanahitaji mwamuzi, awe na busara na uthubutu wa kuweza kufanya dhidi ya hilo atakalo kufanya au kuamua hatima yake.
Nimejifunza vitu fulani vizuri sana kuusiana na Rais wa 35 [Rais wa Marekani mwaka 1961-1963], Mr John Fitzgerald Kennedy [JFK].Nimepata kuona sinema [Movie] ya Kennedy na ndugu yake Robert Francis ''Bobby'' kennedy [RFK]. Kupitia sinema hiyo nilijifunza na kuona ni jinsi gani kiongozi akisukumwa kufanya maamuzi magumu na mazito kwa Taifa kwa kasi na umakini mkubwa sana, na bado akafanya kazi hiyo kwa uamakini huo.
Kupitia kikosi kazi,[Taski Force] chake wakati huo wa vita baridi [Cold War] Viongozi wengi wa kijeshi na Serikali walikuwa wakitaka Marekani ingie vitani, kutokana na chokochoko za vita baridi kati ya USSR na Marekani ikiwemo na Cuba.Lakini kupitia JFK na Bobby ,wamarekani hawakuingia vitani na ukawa ndio mwisho wa vita baridi na hivyo,kuwa mtu muhimu sana kwa bidii binafsi aliepusha dunia kuingia kwenye vita ya TATU YA DUNIA.Hiyo yote pamoja na mapungufu yake kama binadamu katika kupenda wakina mama Warembo kama alivyodondoka kwa mcheza sinema maarufu na mrembo wa wakati huo Marilyn Monroe.Lakini bado alibaki kuwa kiongozi wa kupigiwa mfano kwa maamuzi binafsi ya kielevu na uthubutu [Intellecutal and Braveness decisions].
Aikuishi hapo Rais wa 42 [Mwaka 1993-2001] Taifa hilo Kubwa Duniani Mr William Jefferson ''Bill" Clinton nae kama waliomtangulia akafuata nyayo kwa kuwa na maamuzi yaleyale ya busara na welevu mkubwa kiasi kuhufanya uchumi wa Taifa hilo kuwa mkubwa sana Dunia na kuongeza umaarufu wa Taifa ilo kufahamika sana Duniani kote kama Super Nation,nae pamoja na hayo bado akabaki kuwa binadamu asiekamilka na kupata doa dogo la kupenda wanawake warembo kama vile Monica Samille Lewinsky.
Kwa sasa wataalamu wanaendelea kufanya utafiti kuona kuna uhusiano gani ,kwa watu aina hiyo wenye uwezo mkubwa wa kutoa majibu yanayotatiza jamii kitaifa na kidunia, wanakuwa na ugonjwa wa kupenda wakina mama warembo [JFK v/s Monroe na Bill v/s Monica] .Bado wanaendelea kwa kuwa utafiti ni kitu endelevu uenda siku moja watatwambia majibu sahihi ya utafiti wao juu ya watu hawa wenye uelevu na uthubutu [Intellectual and Braveness] inakuwaje wanakuwa na kaugonjwa haka kakupenda wakina dada warembo.
Nikilejea kwenye hoja halisi kama ningepewa nafasi nani amsaidie Rais wetu kwa ushauri wa kupata mambo ya msingi yawe Dila [Vision] kutuvusha,ningependa kumuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,kuunda kikosi kazi [Task Force] ya kutuvusha kutoka kwenye misukosuko ya kitaifa,kikosi kazi hicho kitachompa ushauri wa nini kifanyike ili tuvuke.Kuna mambo mengi ya msingi yamelizongo Taifa na yanahitaji majibu na maamuzi makali na yenye uthubutu,kama alivyosema swahiba wake Edward Lowasa.
Kama ningepata fursa hiyo timu yangu ya kumshauri Rais wetu katika mambo ya msingi ambayo Taifa linataka majibu,Panel kama kikosi kazi cha ushauri bila kujali chama,itikadi ya kisiasa,dini ili kulitoa Taifa katika kipindi hiki kigumu,kilichogubikwa na wingu la sintofahamu nyingi.Na maamuzi yatakayopatikana hapo yamuongoze Rais katika kutoa mwafaka wa majibu jamii inayoyategeme ili kulivuka daraja hilo.
KIKOSI KAZI [TASK FORCE]
1: Waheshimiwa Marais wote wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
A: Mhe: Ali Hassan Mwinyi
B: Benjamini William Mkapa
2: Marais wote wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
3: Mjane wa Baba wa Taifa
4: Mawaziri Wakuu Wafuatao
A: Salim Mohamed Salim
B: Judge: Joseph Sinde Warioba|
C: David Cleopa Msuya
D: John Marecela
5: Wakuu wa Jeshi na Wanadhimu Wakuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ],waliopo Madarakani na Wastaafu.
6: Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa [DG] wastaafu na walioko madarakani.
7: Viongozi wa Kisiasa
A: DK Wilbrod Slaa
B: Maalim Seif Sharif Hamad
C: Pro Ibrahim Lipumba
D: DK Wilson Mukama
E: Mchungaji Mtikila
F: Freeman Mbowe
8: Viongozi wa Kidini
A: Kaldinali Polycarp Pengo na katibu wake Tanzania Episcopal Conference [TEC]
B: Sheikhy Issa Shaban Simba na Katibu wake wa BAKWATA
C: Mkuu wa Jumuiya ya Wakristo na Katibu wa Jumuiya hiyo Christian Council of Tanzania [CCT] na Katibu wa Jumuiya hii.
D: Mkuu wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheri la Tanzania Askofu DK Alex Malasusa
E: Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana la Tanzania Mchungaji Mokiwa
F: Askofu wa Kanisa la Wasabato Mchungaji Joshua Kahula.
G: Mkuu wa Kanisa la Assemblies of God Dk Barnabas
H:Wazee wa Jadi [Nikimaanisha wazee wa kimila toka pande zote za Tanzania ]
I: Viongozi wa madhhebu ya Hindu na bohara.
9: Wanataaluma kada muhimu.
A: Prof Issa Shivji [Sheria na Katiba UDSM]]
B: Xavier Lwetama [UDSM]
C: Renatus Mkinga [Dar es
D: Pro Baregu [Mwanza]
E: Wakuu wa Vyuo vya UMMA,kama [UDSM,DODOMA,IFM,CBE,MZUMBE n,k]
F: Tindu Lissu [Sheria na Mambo ya Mikataba]
G: ZitoKabwe [Elimu na Changamoto kwa vijana wa sasa]
H: Viongozi Mwenyekiti na katibu wa Jumuiya ya Serikali za ya wanafunzi wa vyuo Elimu ya juu na chuo kikuu.
10: Viongozi wa Serikali ni kama ifuatavyo
A:John Pombe Magufuri [Waziri]
B: Samweli Sitta [Waziri]
C: DK Harrison George Mwakyembe [Naibu Waziri]
E: Anna Tibaijuka. [Waziri].
11: Taasisi
A: Mkurugenzi wa Takukuru Mr Edward Hosea
B: Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Nchini [TNGP ] Usu Mallya
C: Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake [TAMWA]
D: Katibu mfuko wa Mwalimu Nyerere foundation.[Joseph Butiku]
E: Mkurugenzi wa HAKI ELIMU Tanzania.
12: Wazee waliotukuka katika utumishi wa umma ndani ya Serikali na nje ya Serikali
A: Peter Kisumo
B: Sir George Kahama
C: Judge Mark Bomani
D: Edwin Mtei
E: Reginald Mengi