List ya beach nzuri DSM

List ya beach nzuri DSM

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
28,051
Reaction score
52,593
Naombeni list ya beach nzuri za kuogelea weakend ukitoa Coco beach hapa DSM, ziwe na usalama sio za wakabaji na wabakaji na ni muda gani mzuri wa kuogelea? Mdau toka bush.
 
Ukijibiwa nijulishe nina mgeni nae anataka kwenda Beach, last weekend nilimpeleka Coco Beach hakupapenda.
 
Bwagamoyo na Zaa Inzi Bar nilishafika labda huko Pangani, hopefully wale jamaa hawapo tena siku hizi
 
Naombeni list ya beach nzuri za kuogelea weakend ukitoa Coco beach hapa DSM, ziwe na usalama sio za wakabaji na wabakaji na ni muda gani mzuri wa kuogelea? Mdau toka bush.
Unapouliza jambo ni vizuri ujifunze kwanza kuuliza swali.

Si kila anayekwenda beach anaogelea baharini, kuna hotel nzuri sana Dar beach front lakini hazima ufukwe mzuri kwa ajili ya kuogelea baharini.

Kwakuwa hauko specific nakushauri hivi, Ramada hotel Mbezi Beach ni hotel nzuri yenye beach front lakini kuogelea utatumia swimming pool ambalo liko upande wa baharini.

Ila kama shida yako ni kuogelea baharini basi Kigamboni ndiko kwenye fukwe zinazofaa kwa kuogelea baharini, kwa mfano unaweza kwenda Sun rise ufukwe wao uko poa sana na ni msafi na ukitaka kulala hapo hapo huduma inapatikana.

Swali lingine?
 
Ukifika huko beach....kaa mbali na wale vijana wanaokodisha mapira ya kuogelea.......wale vijana ni hatari sana kwa kuwabaka mabinti za watu........

Wanajifanya wanamfundisha binti kuogelea alafu wanampeleka kwenye kina kirefu......ambapo wanajua binti hawezi kujitegemea mwenyewe bila ya msaada wako....na hapo wanamtishia kumuacha hapo....kama atawanyima ile kitu.......kwa uoga wa mawimbi na hofu ya kifo binit anakuwa hana la kufanya zaidi ya kuwakubalia.....na wakati mwingine kubakwa......
 
Back
Top Bottom