Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Mastratejisti wa Serikali ya Magufuli watakuwa walifurahi sana na kujipongeza, baada ya hotuba ya kwanza bungeni ya Profesa Palamagamba Kabudi, waziri mpya wa Sheria na Katiba. Nderemo, vifijo, na makofi yaliyokuwa yanapigwa, pamoja na vibwagizo, na wabunge wa CCM siku hiyo, ni ushahidi tosha.
Katika hotuba hiyo, Profesa Kabudi alionekana hatimaye kuja kama mkombozi wa serikali ya CCM kule Bungeni, kutokana na kuwa chini ya utawala wa Tundu Antipas Mughwai Lissu, ambaye alikuwa anawapeleka puta maspika, wenyeviti na wabunge wa CCM kwa ujumla.
Licha ya lugha yake kali, iliwabidi wapokee hoja zake na kutumia ujuzi wake wa sheria. Kumleta naibu spika ambaye ni mahiri wa sheria, Dakta Tulia, inaweza pia kuwa kwa ajili ya kuwadhibiti wapinzani wakiongozwa na Tundu Lissu katika uwanja huu.
Mhariri Mkuu wa Gazeti la Raia Mwema, Godfrey Dilunga, alikuwa na haya ya kusema kuhusu mtanange huu:
“Swali la kujiuliza, ataendelea kuachiwa mwanya huu? Katika kutafakari swali hili, kule bungeni sasa kuna Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, msomi wa kiwango cha juu, mwepesi katika kumbukumbu za matukio ya kisheria, kisiasa, kijamii na hata kiuchumi, unaweza kusema siri ya uimara wa Lissu katika zama hizi ndio maisha ya kawaida ya kisomi ya Profesa Kabudi (huu ni mjadala mwingine wa siku zijazo).” [ Gazeti Raia Mwema, Toleo la Mei 4, 2017.] Tujadili
1. Kwa maoni yangu, Tundu Lissu ana nafasi kubwa ya kujipambanua na kumwacha kwa mbali Profesa Kabudi, kwa sababu zifuatazo:
2. CV ya Lissu. Pamoja na kwamba kisomi, Profesa Kabudi yuko juu sana zaidi kuliko Lissu katika uwanja wa Sheria, lakini Lissu ana faida ya kuishi yale aliyosoma, kusoma zaidi katika yale anayolazimika kupambana nayo. Karibu maisha yake yote baada ya kuhitimu, ameyatumia katika kupambana na mifumo ya sheria kandamizi na nyonyaji.
Amepambana na makampuni ya madini yanayovuruga mazingira na kubambikiza kesi kwa wananchi “vidomodomo”. Kwa hiyo Lissu ana uzoefu mkubwa sana katika field na ana data nyingi sana kwenye “finger tips” kuliko Profesa Kabudi, ambaye pamoja na kuwa ameshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kupambana na mifumo, kama alivyodokeza kwenye hotuba yake Bungeni, wakati anahitimisha mjadala wa wizara yake bungeni 25 April 2017, lakini sehemu kubwa hasa ni katika kushughulika na nadharia katika tafiti na kufundisha darasani.
3. Passion ya Lissu. Hiki ndicho huonekana wazi kila mara Lissu anapokamata maiki. Kwa jinsi anavyoongea, uchaguzi wake wa maneno, tone yake, lugha yake ya mwili, Lissu hurusha ngumi nzito sana kwa wale anaowasema, kiasi kwamba wanakuwa katika wakati mgumu sana wamsikilizapo.
Hurusha makombora mazito sana yenye nguvu. Hii ni kutokana na kwamba toka ameanza kupambana, hajabadilisha kambi wala kubadili msimamo. Anaishi anayoyasema. Hii binafsi huwa inanishangaza sana kwa sababu najua kwamba makampuni ya Madini yana uwezo mkubwa wa kifedha na yamewa “garagaza” wengi waliojaribu kuyapinga, kwa kuwavuta mashati.
Wakati Profesa Kabudi mwanzo alionekana kama mtetezi wa wanyonge na mpinga ukandamizaji, baadaye alionekana “kuvutwa shati”, hasa mwanzoni mwa mijadala ya “Katiba Mpya”. Hapo akawa mtu wa kuisemea serikali, na serikali ikawa inamtumia “kutoa semina kwa wabunge”, ambazo zilioneshwa moja kwa moja na TBC.
Lakini baadaye Tume ya Katiba ya Warioba ilipochezewa rafu na serikali, wakanyang’anywa magari njiani, ambapo akina Polepole walianza kuzunguka nchi nzima wakiiandama serikali na kutetea rasimu ya katiba, Kabudi akageuka na kuwa mwiba kwa serikali. Hivi karibuni amevutwa tena shati na sasa ni mtetezi wa serikali katika mambo ya kisheria.
Kwa maoni yangu, si rahisi Kabudi kuwa na Passion ya kiwango cha Lissu. Anaweza kweli ku-summon passion kwa kiwango fulani, kama ilivyoonekana kwenye hotuba yake Bungeni, kwa kukumbusha aliyofanya miaka ya nyuma sana, lakini si kwa muda mrefu, na si kwa kiwango cha Lissu.
4. Historia. Historia iko upande wa Lissu. Ni kweli kwamba serikali ya CCM imesimamia uundwaji na usainiwaji wa mikataba mibovu kuwahi kutokea katika Historia ya wizi wa madini duniani. Hata Chifu Mangungu katika ujinga wake wote, hafikii rekodi ya CCM. Katika awamu mbalimbali za marais chini ya CCM, uwekezaji katika madini uliasisiwa, baada ya kuwekwa pembeni na Baba wa Taifa, Rais Nyerere. Mkapa ndiye alifungulia mbwa, na kuanzia hapo Tanzania imepigika vibaya sana kwa mfululizo wa mikataba ya wizi wa mchana.
Kuanzia mikataba ya umeme (IPTL, Net Group Solutions, Richmond, Dowans, Aggreko, Songas), mikataba ya madini, mikataba ya Gesi na mafuta, ni nchi inaliwa kulia, kushoto, juu na chini. Achilia mbali Ufisadi kupita Kagoda, na dada yake Meremeta, Rada, Escrow, Loliondo, bila kusahau wizi mkubwa kupitia ukwapuaji wa nyumba za Serikali.
Kwa rekodi kali ya wizi na ufisadi mkubwa wa kiwango hicho, mtu anayesimama kuibeba serikali ya CCM, atahitajika kuwa na ubavu wa pekee kubeba tani zote hizo za kashfa, wizi na ufisadi. Kitu ambacho sidhani Profesa Kabudi anaweza kufanya. Hiyo haihitaji uprofesa wa Chuo Kikuu, labda Uprofesa wa aina ya Maji Marefu.
Katika kudhihirisha hili, katika mjadala wa sasa kuhusu mchanga wa dhahabu, Lissu ameng'ara sana kwa sababu anaweza kueleza kwa uwazi na ufasaha, historia yake ya mapambano. ni mtu anaelewa vizuri tatizo liko wapi na hivyo kama kweli nchi inataka kushughulikia matatizo haya, ianzie wapi.
Ushauri: CCM iwe mpole, ichape kazi. Irejeshe nyumba za serikali, hapo angalau Rais Magufuli atakuwa na ile “moral high ground” ya kushughulika na mambo mengine. Washughulike na kurekebisha mikataba mibovu. Wasijali hata kujikata miguu na mikono, ali mradi mwili mzima upone kansa hii.
Waache kupambana na upinzani. Hata kama wapinzani wanawakumbusha wananchi mambo ambayo kwa CCM ni mwiko kuyakumbusha, wao wasijali. Waache Bunge live ili wananchi wasiwafikirie kwamba wana mambo ya kuficha. Hapo Mastratejisti wala hawatakuwa na kibarua cha kuwatafuta “magicians” wa kuiokoa Serikali ya CCM.