Lissu vs Kabudi: Ngoma Inogile...

Lissu vs Kabudi: Ngoma Inogile...

Kabudi tayari ameshapotezwa siku nyingi na Lissu.
Na ndio maana kwenye issue ya Makinikia Kabudi hajasogeza pua yake baada ya kuona zile nondo na data alizoshusha Lissu.

CCM wao waendelee kupeleka vilaza mle ndani tu kama Kibajaji, Msukuma, Jah People, yule dogo wa Ulanga nk nk.. maana qualifications wao ni kusoma na kuandika.
 
mtoa mada upo sahihi , lakini huwezi kumlinganisha Lissu na Kabudi kama umewahi kufanya naye kazi Kabudi au ukashiriki mijadala ya kikatiba na kisheria Kabudi ni kiumbe kingine katika dunia hii, wapi wasipomfahamu Kabudi waulize akina Bagbo na watara wa Ivorycoast
 
Lisu kala mpunga wa wazungu credibility yake haipo tena
Weka ushahidi ili tukuondoe kwenye kundi la watu ambao uelewa wao unashuka kwa kasi kubwa kiasi cha kutoelewa Lissu anazungumza nini!
 
Labda sijakuelewa lakini kama umeweka hili bandika kumsifu Lissu kwa kile anachokisimamia naona umeji contradict, Lissu katika masuala mengi hapo juu yenye utata hakusita kuishauri serikali iwachukulie hatua watuy waliokosea hadi kumshinikiza waziri mkuu aachie ngazi japo hakuna mahakama yeyoote iliyothibitisha ufisadi wa Mheshimiwa Lowasa.
Lissu aliunga mkono kamati ya bunge iliyoleta uchunguzi wa EPA na ushauri wa Kamati kuhusu kuchukuliwa hatua kwa wahusika, Lissu aliunga mkono Escrow japo pia wawekezaji walikuwepo hapo pia, Na kubwa zaidi Lissu aliunga mkono kamati ya Richmond, sasa sijui kuna tofauti gani ya hizo kamati zilizopita na hii ya rais. Kama aliunga mkono kamati iliyomtuhumu mtu bila kumuuliza ama kufanya mahojiano naye iweje leo aionee huruma Tanzania sababu tu kamati imeundwa na rais ati tutafika pabaya?

Wewe huoni hapo anacheza na siasa zaidi kuliko utaalamu wake kama mwanasheria mwanasiasa? Ndiyo maana kugeuka geuka huko kunawafanya watanzania wasiwaamini wanasisasa wa sampuli ya Lissu japo wanachokiongea kina maana lakini wanaongea wakati ambao si muafaka ama wanachokisema hakitoka mioyoni mwao.

Nilishasema huko nyuma Taifa hili lingeweza kukombelewa na watu kama kina Zitto, Lema, Lissu, Bashe, Nassari na wengine wengi sana vijana ambao wapo hata CCM lakini tatizo kubwa ni kwamba hawaaminikia. Ukimtoa Bashe hakuna hata mbunge mmoja kati ya hao niliowataja hapo juu mwenye uthubutu wa kuwahoji wakubwa wao kama kina Mbowe ama Magufuli kwa CCM. Bashe pekee ndiye kijana anayejiamini kukikosoa hata chama chake. Lissu umemsikia lini anakisema chama chake kwa kupotoka kutuletea mtu ambaye alituhumiwa na bunge kwa kulipotezea taifa pesa nyingi????

Jaribu kuwa mkweli na kumwambia Lissu pamoja na ujasiri wake wa kumchamba mpaka Nyerere lakini anafyata mkia wake ulio katikati ya mapaja yake likija jambo kuhusu viongozi wake wa CDM. Na mimi ninayesema hivi ni critical wa Magufuli lakini sipendi kila mara kusikia watu wakimlaum Magufuli kwa masuala ya nyumba wakati kuna wenzake tunataka mpaka kuwaweka Ikulu alishirikiana nao. Kama tunawasamehe kina Mtei, Lowasa, Sumaye walioshika nyadhifa kubwa zaidi ya magufuli sioni sababu kwanini tuendelee kumsulubisha Magufuli kwa kosa kutimiza kazi yake kama waziri.

Una lengo zuri lakini umetandaza blanketi kubwa mno juu ya hoja zako, umetoa kauli bila kuzipa uzito wa hoja. sikuwa na maana hasa ya kumsifu Lissu, nilikuwa naangalia hatua zilizochukuliwa kumdhibiti Lissu, na jinsi ninavyodhani kwamba hizo hazitoshi. mwisho nimetoa ushauri juu ya nini hasa kifanyike, ili kuepuka kushughulika na watu binafsi moja kwa moja kama ilivyo hivi sasa, na badala yake taifa lijielekeze katika ku-deal na issues. tunahitaji Rais ambaye ataliunganisha taifa pamoja na resource zake zote, za upinzani na za wananchi wengine, katika kushughulika na matatizo ya nchi hii. ndiyo ushauri ambao mtu kama Jenerali Ulimwengu huwa anautoa. kuwa na mijadala ya kitaifa ambayo itabeba maoni ya wigo mpana katika taifa letu.

Tatizo kubwa la Serikali ya CCM ni kwamba inataka kufanya maovu lakini iendelee bila kufanya uwajibikaji wa kweli kwa watenda maovu hayo. pia inataka kushughulika na upinzani kwa kutumia ubabe, badala ya kutumia njia rahisi sana ya kushughulikia kero za wananchi, na kuwaacha wapinzani wafanye shughuli zao kwa mujibu wa sheria.

Unasema kwamba Lissu alikubaliana na kamati mbalimbali ulizotaja. nikupe mfano wa kamati ya Mwakyembe, kuhusu Richmond. Upinzani ulipokea mapendekezo ya kamati, na Bunge lilitoa maazimio ambayo yalihitaji kutekelezwa na Serikali. lakini ni majuzi tu KUB ameikumbusha serikali kutekeleza yale yaliyopendekezwa. Serikali ilitekeleza machache tu. Kuhusu Escrow, kulikuwa na makubaliano kati ya upinzani na Serikali juu ya hatua za kuchukua. lakini kumbuka kwamba kulikuwa na ule mgao wa fedha za kigeni, zilozochukuliwa kwenye viroba, na huu haukuwekwa wazi. ulio "vuja" ni ule tu wa Benki ya Mkombozi. na hapo ndipo hatua zote zilielekezwa. Upinzani wamekuwa wakilazimika kukubaliana na kiduchu kinachokubaliwa na wabunge wa CCM, ili angalau Taifa lisonge mbele. hayo hayo yalifanyika pia wakati wa mchakato wa Katiba.

Unakumbuka jinsi wapinzani, Lissu akiwemo, walivyofanya jitihada kuonesha kwamba kama "process" ya kuandika katiba mpya iko "flawed", basi matokeo ya mwisho, yaani Katiba yenyewe, itakuwa "flawed". walidiriki kwenda "kunywa chai" ikulu ili kujaribu kuweka mambo sawa na Rais Kikwete. mwisho wa yote ilibidi wakubaliane kwa shingo upande na machache waliyopata, japo si kwa kiwango walichohitaji. ukiangalia hoja za upinzani katika hili la Katiba, nyingi zilikuwa zina faida kwa Taifa zima. mfano kuwaweka wabunge wa sasa kuwa automatic members wa Bunge la Katiba, hiyo ilizuia moja kwa moja vifungu vilivyokuwa vinawadhibiti wabunge.

Huu utayari wa wapinzani kukaa chini na Serikali ya CCM ili kuweka mambo sawa, umekuwa ukikosolewa sana na watu kama Mzee Mwanajiji (yule wa zamani, siyo wa sasa). lakini mimi binafsi niliona ni jambo jema kwa mustakabali wa nchi yetu.

Kwa hoja hizo, sikubaliani kabisa na hoja yako kwamba Lissu anacheza na hoja kisiasa kuliko kisheria.

Kuhusu Nyerere, mimi namheshimu sana huyu Baba wa Taifa. lakini sina tatizo na watu kama Lissu wanaomkosoa sana. na hata Nyerere mwenyewe hatashangaa na hilo. enzi zake, Profesa Shivji alikuwa mpinzani mkubwa sana wa Nyerere, na walikuwa wanatoana jasho pale Nkrumah. Nyerere alipenda sana mijadala na alikaribisha watu wam-beat kwa hoja. Leo utashangaa Shivji ndiyo alikuwa Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, akiongoza jitihada za kumuenzi. alimkosoa siyo kwa nia mbaya, ila alitaka Nyerere atoe kilicho bora. Leo Lissu anajadili mapungufu ya Nyerere, kinachotakiwa ni wenye hoja kinzani wajitokeze. hoja hujibiwa kwa hoja. CCM na serikali yake wanajibu hoja kwa ubabe na mabavu. na pia wanamtumia Nyerere kufunika maovu yao tu, na wala hawamuenzi katika mantiki na misingi ya falsafa zake. kwa maoni yangu, Nyerere angempenda zaidi Lissu kuliko hao wanaotoa "lip service" kwake, kujifanya wanamtetea kumbe ni mbwa mwitu hatari. Nyerere alikuwa mpigania wanyonge, jambo ambalo Lissu analifanya kwa moyo wote.

Kuhusu Lissu kuisema CHADEMA, hiyo inaweza kuwa ni ishu ya style. huwa nasikia kwamba katika vikao vyao, huwa kuna minyukano mikali, ambapo wengine wanaweza kupendelea hili wengine lile. mwisho wa yote wanafikia muafaka. hilo ndio la msingi.
Weakness pekee ya Lissu ninayoweza kuisema, ni kwamba tunahitaji wapiga kelele wa aina yake wengi zaidi, ili awe more moderate, asipayuke mno kama anavyofanya hivi sasa
 
Analysis nzuri japo imekosa tu mifano hai (references) but ni nzuri.
hapo kwenye kukosa references ndio msingi wa udhaifu wa analysis yake. ametoa blanket statements ambazo nimejaribu kuzijibu kwa kiasi fulani
 
Bavicha sijui wanavuta bange ya wapi.Yaa Tundu Lissu mnamlinganisha na Prof.Palamagamba Kabudi?
Tundu Lissu kiboko yake ni Tulia Acson,kabudi yupo juu sana.
Tulia alimtuliza Lissu ndani ya nusu saa tu.Tundu Lissu alikuja na mikoba mitano imejaa vitabu lakini alishindwa
Toa hoja...acha kutufunika kwa blanketi
 
Bavicha sijui wanavuta bange ya wapi.Yaa Tundu Lissu mnamlinganisha na Prof.Palamagamba Kabudi?
Tundu Lissu kiboko yake ni Tulia Acson,kabudi yupo juu sana.
Tulia alimtuliza Lissu ndani ya nusu saa tu.Tundu Lissu alikuja na mikoba mitano imejaa vitabu lakini alishindwa
Huwezi kulinganisha huyo ajuza na lissu hata siku moja hata huyo propessa hana ubavu wa kujilinganisha na lissu
 
Back
Top Bottom