Lissu: Si mara ya kwanza tunaahidiwa kuwekewa mikataba wazi. Kumuunga mkono Rais si lazima

Action speaks louder than words!

Lisu ni mwongeaji tu, hakuna alilowahi kulifanya kwa taifa hili...

Msomi ambaye anaamini katika maneno kuliko vitendo hana faida kwa taifa letu.! Yeye huwa anajifanya anajua kila kitu lakin utendaji ni zero kabisa.
Asimami kwenye jambo moja huwa ni mtu wa kugeuka geuka.

Binafsi nampongeza Magufuri, kwa hakika amethubutu japokuwa ni kwa kiasi lakini amejitahidi..
 
Dah! Kamanda Lissu katika ubora wake. Kashusha nondo za hali ya juu! Mikataba yote ya madini ikiwemo almasi, dhahabu, uranium, gesi na mafuta, ujenzi kiwanja cha ndege chato, ununuzi kivuko uozo cha Dar Bwagamoyo, mikataba ya umeme na symbion, IPTL, mikataba ya kununua ndege toka bombardier na Boeing na mkataba na Uturuki wa kujenga reli ambao mwanzoni ulitakiwa usainiwe na China, mikataba wa Lugumi nao. Mikataba ya ujenzi wa barabara nchini. Yote hii ipelekwe bungeni mara moja bila kuchelewa na wahusika wote waliosababisha Taifa kuingia hasara kubwa ya matrilioni ya shilingi wapandishwe kizimbani mara moja na mali zao zote kufilisiwa.

Hapo tutathibitisha kwamba Magufuli kaamua kufanya kweli na kupambana na wezi na mafisadi nchini badala ya kuwakingia kifua. Vinginevyo itakuwa yale yale ya CHANGA LA MACHO.
Si tumeamua kuwa "Wazalendo"? na zile nyumba za umma za masaki na Osterbay zilizouzwa kwa ACACIA weusi kwa be ipoa zirudishwe.... Hapo ndipo tutajua ni kweli watu wamezaliwa upya.
 
Kwani Mheshimiwa Mtukufu sana Rais Magufuli ni zao la Mfumo gani ?..
Kwenye maswala ya msingi tukiingiza uchama hakika tutafeli...

Kama kweli tunataka tufike mahali ni lazima tubadiri misimamo yetu na kushikamana kujenga taifa letu..

Tukianza kuangalia mazao ya mfumo tawala (CCM) naweza kusema yapo katika vyama vyote vya Upinzani..
Kwa mfano: CUF (mwenyekiti wake ni zao la chama tawala), ACT (Mwenyekiti ni zao la chama tawala), CHADEMA ( Mgombea urais 2015 ni zao la chama tawala)..

Kwa hiyo ndugu mm naona bora tumsapoti tu rais aliyeko madarakani, kwa hakika amejitahidi kuthubutu tena kwa vitendo
...
Huo ndo ukweli!!!
 
Action speaks louder than words!

Lisu ni mwongeaji tu, hakuna alilowahi kulifanya kwa taifa hili...

Msomi ambaye anaamini katika maneno kuliko vitendo hana faida kwa taifa letu.! Yeye huwa anajifanya anajua kila kitu lakin utendaji ni zero kabisa.
Asimami kwenye jambo moja huwa ni mtu wa kugeuka geuka.

Binafsi nampongeza Magufuri, kwa hakika amethubutu japokuwa ni kwa kiasi lakini amejitahidi..
Magu nami namkubali
Lisu kahamia kutetea watu wa mshiko sioni ajabu alianza kwa lowasa sasa kwa wazungu kisha lambishwa
Dhamira ya kiongozi au mtu huwezi ijua kwa kuhisia au dhana kuwa itakuwa kama yule au hao
Angesubiri kwanza hata mwezi ndo aropoke
 
Ningepewa chance Lissu ningemtoboa macho awe kipofu maana anaichukia mno Tanzania, kashindwa kabisa kuchagiza maendeleo jimboni kwake kageuza kuwa Mbunge wa TAIFA, na kisutu anakwenda kuliko Jimboni
 
Kwenye maswala ya msingi tukiingiza uchama hakika tutafeli...

Kama kweli tunataka tufike mahali ni lazima tubadiri misimamo yetu na kushikamana kujenga taifa letu..

Tukianza kuangalia mazao ya mfumo tawala (CCM) naweza kusema yapo katika vyama vyote vya Upinzani..
Kwa mfano: CUF (mwenyekiti wake ni zao la chama tawala), ACT (Mwenyekiti ni zao la chama tawala), CHADEMA ( Mgombea urais 2015 ni zao la chama tawala)..

Kwa hiyo ndugu mm naona bora tumsapoti tu rais aliyeko madarakani, kwa hakika amejitahidi kuthubutu tena kwa vitendo
...
Huo ndo ukweli!!!

Mkuu kwa hiyo unaamini hao ulio wataja bado wanawaza/wanatenda kama walivyokuwa ktk Vyama vyao awali ?..

Sidhani kama hiyo kitu inaniingia Akilini kumuunga mkono Mtu anae onesha Chuki za wazi kwa Wananchi walewale (Watanzania) kisa tu hawawazi na kufikiri na kutenda kama yeye,ameshasema atawafukuza Bungeni na wakija Mtaani atawashughulikia...Ina make sense kweli kugawanywa hivi na Raia namba moja ?

Hii Nchi sio Mali ya Mtu mmoja jamani ,au kwa sababu wenzetu mmeshika mpini ?..
 
Ningepewa chance Lissu ningemtoboa macho awe kipofu maana anaichukia mno Tanzania, kashindwa kabisa kuchagiza maendeleo jimboni kwake kageuza kuwa Mbunge wa TAIFA, na kisutu anakwenda kuliko Jimboni

Punguza mapovu wewe keng...
 
Mlitaka jpm awafukuze ili mpate hoja mpya ya jpm kukimbiza wawekezaji? Mbona yeye lissu aliyekuwa akibwabwaja kuwa tutashitakiwa, ameshindwa kutolea ufafanuzi leo?hakika hizi siasa za kuvizia hazitowaacha salama:D
Umemwomba atoe ufafanuzi akashindwa? Nani anayevizia wenzie kama unataka kufikiri kwa uhuru? BTW, bado unawaita ACACIA kuwa ni wezi? Mbona mlichokuwa mnashauriwa mkawaita watoa ushauri kuwa sio wazalendo ndio mnaenda kukifanya?
 
There are some individuals need to rest in eternal peace, to save the nation! CinC, please...
 
Tuachane na yaliyopita lisu tujenge nchi yetu,kwa maana hiyo wewe unatakaje?kila kutu unapinga na kulalamika,maana hata wakoloni walikua adui tungeamua tugomee Uhuru kwa sababu tumenyonywa tungeonekana Wa aina gani?cha ajabu kina tamko la raid wewe unapinga je unataka nini?
 
Tuachane na yaliyopita lisu tujenge nchi yetu,kwa maana hiyo wewe unatakaje?kila kutu unapinga na kulalamika,maana hata wakoloni walikua adui tungeamua tugomee Uhuru kwa sababu tumenyonywa tungeonekana Wa aina gani?cha ajabu kina tamko la raid wewe unapinga je unataka nini?
Huku sio kupinga ndugu!!
Hii inaitwa justification of an action.
A brilliant person must have high capacity of reasoning. You don't need to be a yes man.

Changamsha akili

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
For the Record: What Goes Around Comes Around!!!

Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.

Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.

Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.

1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.

2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.

Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.

Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99 nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.

Kwa miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.

Watu hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.

Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.

Wachache tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.

Kwa mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'

Baadhi yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi '08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.

Kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.

Tunaambiwa ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama tunaona amekosea???

Hebu naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni hivyo, fikiria yafuatayo:

1) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba, kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara Tarime.

Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!

2) Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini) inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.

3) Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.

4) Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi, uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic changes excepted.

Aidha, licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.

5) Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini (Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.

6) Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu miaka ya mwanzo ya '90.

Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.

Lakini je, hii ni mara ya kwanza tunaahidiwa hayo???

Mwaka '08 Jemedari Mkuu wa kabla yake alituahidi hivyo hivyo. Tuwe na subira kabla ya kuanza kushangilia prematurely.

7) Nimemsikia Magufuli akielekeza wahusika wote wa uchafu huu washughulikiwe. Kweli???

(a) Je, Jakaya Kikwete aliyesaini leseni za Bulyanhulu na Nzega mwaka '94 anaponaje???

(b) Je, Ben Mkapa aliyekuwa Rais na Mwenyekiti wa Cabinet wakati haya yanafanyika anaachwaje???

(c) Je, waliokuwa mawaziri na manaibu wao wote wakati haya yanatokea wanasalimikaje???

(d) Je, wale washangiliaji na wapiga meza wa bungeni, ambao waliunga mkono kila walicholetewa bungeni na kukipitisha kilivyo wanakosaje lawama???

8) Nimesikia Acacia Mining hawana hata leseni/usajili wa kuendeshea shughuli zao hapa nchini. Labda. Hata hivyo, jiulize yafuatayo:

(a) Hivi wamekuwa wanalipa kodi kama PAYE, SDL, income tax, withholding tax, mrahaba, n.k., kwa kutumia jina gani miaka yote hii???

(b) Je, wana akaunti yoyote katika benki za Tanzania??? Kama ndio, wamezifungua kwa jina gani???

Kama hapana, wanalipaje mishahara ya wafanyakazi wao wa Kitanzania au watoa huduma mbali mbali wa Kitanzania???

(c) Je, wanalipa bili za umeme kwa TANESCO au za simu kwa Vodacom, Tigo, Airtel, n.k. kwa kutumia jina gani???

(d) Je, wamesajiliwaje katika Soko la Hisa la Dar kama Acacia kama wanaendesha shughuli zao kihuni hivi???

(e) Kuna kitu kinaitwa 'estoppel' katika Sheria yetu ya Mikataba (the Law of Contract Act, Cap. 345) na katika Sheria yetu ya Ushahidi (the Law of Evidence, Cap. 6).

Je, estoppel haituhusu kwenye suala hili la leseni au usajili ya Acacia???

Kama estoppel inahusika, je, hoja hii ya ukosefu wa usajili ina uzito gani, kama upo, kisheria???

9) Nimesikia Sheria za Madini zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Sawa kabisa.

Lakini je, kwanini Rais Magufuli hajasema chochote juu ya Sheria za Gesi Asilia na Mafuta ambazo zilipitishwa haraka haraka kwa Hati ya Dharura baada ya sisi 'waropokaji' kutimuliwa bungeni na Spika Anna Makinda mwaka '15???

Au Rais wetu anaamini kwamba Sheria za Gesi Asilia na Mafuta hazina matatizo licha ya kupitishwa kwa utaratibu ule ule uliotumika kwa Sheria za Madini???

10) Wakati tunaingojea kwa hamu mikataba ya madini iletwe bungeni, hebu na tujiulize yafuatayo:

(a) Mikataba ya uchimbaji gesi asilia na mafuta nayo iko wapi???

(b) Mikataba ya manunuzi ya Bombardier na Dreamliner za Magufuli nayo italetwa bungeni au itabidi tusubiri aondoke madarakani kwanza kama ilivyokuwa kwa JK na BM???

(c) Mikataba ya ujenzi wa airport Chato na Reli ya Standard Geji ya Waturuki au Wachina na mabarabara kibao nayo italetwa bungeni au ndio basi tena tusubiri Bwana mkubwa atakapoondoka madarakani???

Wakati tukisubiri kufukuzwa bungeni na Spika Ndugai kwa maelekezo ya bosi wake, na wakati tukisubiri dhahama ya Bwana Mkubwa nje ya Bunge, hebu na tujiulize hivi nani hasa ndiye mzalendo wa kweli wa nchi hii???

Hebu na atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli.

Sijazungumzia bado plagiarism ya taarifa mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali katika Taarifa ya Kamati ya Prof. Osoro. Hili ni la baadae.


LISSU punguza kelele. Iunge serikali mkono ikifanya vizuri, ipinge ikikosea, wewe kila kitu unaoinga tu, ng'ombe ikioia sana hakawii kupasuka. Ndiyo kuna Mengi unazungumza ya ukweli, sana nyingine unapinga vitu vya maana kwa Watanzania. Please grow up.
 
Back
Top Bottom