4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,319
- 12,999
Sawa tu ,Hata kuku, asema hivyo hivyo kumhusu mwewe ..
Sawa tu ,Hata kuku, asema hivyo hivyo kumhusu mwewe ..
Tuisubiri next step.Isiwe dua la kuku. Nyomi huchizisha. Kuna hatari kuwa tushindwa kutambua matumizi ya nyomi.
Kumbuka hatukumwunga mkono Ndugai, Bashiru, Pole pole, Mwingira na wengi wengine.
Sasa hivi chawa wameelekeza madongo yao kwa kina Slaa.
Matamko rasmi au muhimu ya chama yanachelewa mno au hata kutokuwapo kabisa.
Kulihitajika chaguzi kwa nafasi zote chamani tokea chibi hadi juu. Wakapewa watu nafasi kwa umahiri na kupigwa chini bIla kuchelewa wasipokidhi mategemeo.
Siasa ni sayansi tunaweza kuwa tunakosa mtu wa callibre ya chikwette (cunning} kama mwana mikakati.
Chadema na chikwette mmoja ingechukua nchi mapema asubuhi.
Usiwabeze Cdm , wamefanya kazi ya siasa kwenye mazingira magumu yasiyo fair hata kidogo, na bado wamesavaivu kwa kitambo kirefu.Anachofanya Lissu kwa kitengo hiki cha habari na propaganda kama kipo kinapewa wapi publicity?
Au unadhani kazi hiyo itafanywa na TBC, Channel 10 au ITV mwaka 2026?
Kulikoni habari zao zinazopotoshwa hapa na pale au hata kupambana na negative publicity kutokea kwa mahasimu wao kama CCM na vibaraka wao?
Kuna wanachama wanaotanga astray Kwa kukosa miongozo. Imekuwa kama vifaranga wa kuku kila mmoja kuchakura kivyake.
"Bila kurudi kwenye drawing board kwanza kuweka mambo sawa, yanayoendelea ni kama kuvuja kwa pakacha.
Nyomi isiyo tafsirika kwenye uwanda wa maamuzi kwa sababu yoyote haisaidii.
Tujipange kwa ushindi ndani au nje ya wizi wao.
Ni wazi kuwa ma CCM na washirika wao hawawezi kuupenda ushauri huu.
Vipi ndugu, wewe ni mmoja wao?
Nami niongeze nimekoshwa na wako uandishi mengi mazuri umenena ila lugha uliyotumia ni ngumu kukuelewa!Nani asiyezijua ghiliba na faulo za CCM? Hii ikiwa tokea kwenye kucheza visivyo na taasisi za umma? Kununua wapinzani na ikibidi hata kukimbia na masanduku ya kura mchana mchana?
Wananchi kote nchini wamechoshwa na uhuni wao huu. Kinachokosekana ni mbadala wa waliodhamiria kufanya kweli kwa vitendo. Siyo kwa maneno!
"Kwamba kote mnakokwenda kuna nyomi la kufa mtu? Kwamba hivyo ni kote hadi usukumani Chatto na hata Kizimkazi, Makunduchi huko?
"Kwani hiyo bado ni habari tena? Tulipo sasa ni kuwa, nyomi ipo; sawa! Halafu?"
CHADEMA Nyomi si Habari Tena, Tujidhatiti kumaliza Mchecho
Pamoja na nyomi lote, mwizi mbobezi wa kura mbona anamaliza mchezo asubuhi na mapema tu? Kwani Ali Bongo au Munangagwa ilikuwaje? Au hata 2015 na pia 2019/20 nako je?
"Ilihitajika katiba mpya yenye mazingira sawa na ya haki kwa wote. Kuna hatari kuwa katiba mpya haitakuwapo kwenye uchaguzi mkuu huu unaokuja."
Kwani ilikuwa ni lazima ufanyike 2024/25?
Inafahamika kuwa ni kwa maslahi ya CCM, katiba mpya isiwepo. Hii angalau iwe hivyo hadi chaguzi za 2029/30.
Cha kujiuliza, "Kwa hiyo?"
"Hata kama kutakuwa na tume huru, bila Mahakama huru, bado ngoma iko pale pale." Kumbe kimbilio letu wakifanya tale mambo yao litakuwa wapi?
Kususia uchaguzi hakuwezi kuwa dili. Alisusa Seif na bado watu wakala kwavraha zao. Labda kama ni kuusimamisha kabisa, wote usiwepo, kama tunaweza.
"Kama kuusimamisha hatuwezi ni muhimu kujipanga kuona tunashinda uchaguzi huu ndani ya rafu zao zote zilizopo. Hii ikiwa zote tunazozijua au hata tunazoweza kuzibashiri.
Kujipanga kwa ushindi ndani ya rafu zao inawezekana. Hata hivyo huko hakuwezi kufanikishwa tokea majukwaani. Sana sana labda kutokea kwenye drawing boards, chini ya wapanga mikakati wabobezi wenye kueleweka.
Kitengo cha habari na propaganda hakiwezi kuwa hiki kilichopo. Kilichopo hakijui habari ni nguvu wala hata hakiijui nguvu ya habari. Hiki hakijui hata namna ya kuzi shape siasa za nchi kuelekea tunakotaka sisi pasipokuwa na kutumia nguvu au kutumia nguvu kubwa mno.
Hiki kilichopo, kama kipo, hakifai. Akiita jiwe ni jipu!
"Hiki kilikuwa ni cha kuanza nacho."
Kama chama ni muhimu kuwa na namna thabiti ya kuwadhibiti wanachama wake. Wakiwamo hata wale uchwara wa mitandaoni. Ikibidi hata kwa kuwakana hadharani tu, inatosha sana.
Tutamtoa CCM tukishirikiana na wengine bila kujali majina yao alimradi tunaokubaliana nao kwa wakati husika. Tukawapate wapi malaika, ya Rabi vidampa sisi?!
Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini
Hatutamtoa CCM tukitumia Malaika. Kwenye hilo tunapaswa kuwa wakali kweli kweli, ikibidi hata tukiwa na bakora mikononi.
Chama chenye malengo ya kuchukua nchi hakiwezi kuendekeza upuuzi au hata wapuuzi wachache wenye kujinasibu nacho.
Chama chenye kulenga kuchukua nchi katika hali yetu kinapaswa kudhamiria na kuonekana hivyo ikiwamo hata kwa mwonekano wa usoni tu.
Wawekwe pembeni wote walioko chamani kifursa.
Iwe kazi tu!
Jiwe yeye akisema; "Hapa Kazi tu." Kwa hakika alimaanisha.
Haipo namna nyingine.
Lissu na Mbowe wanapigania kuongeza kura ili 2025 waongeze majimbo na kura ili wapate Mgao wa ruzuku zaid ya huu wa sasa
Mtaani kugumu kila biashara mgumu
ukipata fursa ya kulamba 2 billion ya ruzuku kila mwezi si haba kwa gharama ya porojo tu jukwaani
Nami niongeze nimekoshwa na wako uandishi mengi mazuri umenena ila lugha uliyotumia ni ngumu kukuelewa!
Sawa tu ,
Usiwabeze Cdm , wamefanya kazi ya siasa kwenye mazingira magumu yasiyo fair hata kidogo, na bado wamesavaivu kwa kitambo kirefu.
Kwenye mazingira ambayo mshindani wako ni muajiri namba moja , wa vyombo vya dola na vya maamuzi. Ni jambo gumu kupambana na mshindani wa hivyo na kumshinda. Unless utumie njia zisizo rasmi na haramu ili kuwalazimisha kuja mezani.
Nchi ambayo vyombo vya habari, haviwezi kumzungumzia mpinzani positively, bali labda negatively!! Nchi ambayo vyombo vya maamuzi huelekezwa nini cha kuamua !!.
Mbaya zaidi wananchi wa nchi hii ni waoga. Hawawezi kutetea haki zao za msingi. Mfano kwenye swala kama la bandari. Wananchi wange react tu, lisingeendelea .
Nadhani wapongezwe vinginevyo wachukue njia haramu.
Tuisubiri next step.
Elimu ikikolea pressure itakolezwa!
Hilo la media za CDM kusinzia nimesema sana humu. Website haijafanyiwa updates toka uchaguzi wa 2020, yaani hadi ni aibu.Wapi unasoma kabezwa Chadema? Au hata wapi unaona kadogoshwa?
Kwamba CCM amehodhi dola na hataki kuachia? Chama cha siasa jukumu lake kuu ni kuhodhi dola kadri iwezekanavyo kama haipokonywi.
Kama haipokonywi CCM itaendelea kuhodhi dola milele na hiyo ni haki yao kwenye jamhuri ya mabwege.
Mabwege ni sote kama hatutoki hata kuelezana ukweli huu, ninao usema hapa waziwazi.
Unategemea CCM wameonee huruma nani kumpa ushindi? Mbinu za ushindi ni pamoja na faulo, rafu na hata wizi! Hayo ni muhimu kuyajua.
Ghiliba za CCM zitasimamishwa Kwa mipango yote overt au covert kwa maana ndivyo hivyo hivyo wao wanavyo hodhi dola pia.
Vyombo vya habari gani ambavyo ungependa viongelee habari za wapinzani? TBC, channel 10, ITV au AYO TV?
Kwani hata websites, accounts zao rasmi, au vile vi TV online vyao vinasema nini? Kuna updates zozote au hata updates zozote za maana huko?
Vipi vitengo vyao vya habari na propaganda? Wanavyo kweli? Vimelala au vimekufa? Wanajua unuhimu wake? Kama wanajua, wanafanya nini ku reflect unuhimu huo?
Tunapolaumu media, kama chama tunafanya nini kujitangaza wenyewe katika yaliyo mikononi mwetu?
Hili la kuwalaumu watanzania au wananchi kuto "react" ndiyo kichekesho kingine kwenye kuonyesha ubwege wetu kama upinzani:
View attachment 2741741
Kwa statement kama hIzo za kuwalaumu wananchi, huwa hasa mna mlenga nani?
Kwani hata wanahitajika wananchi wangapi?
Kwani wale wanachama walio kwenye digital registration 8.5m+, wao siyo wananchi? Au Labda mwananchi yupi ambaye huyo kama ange "react" ndiyo mngefarijika sasa amewajibika?
Siyo kuwa tunataka kuvuna tusipo panda?
Ninakazia:
Nyomi zisizokuwa na tija ni za nini?
Hilo la media za CDM kusinzia nimesema sana humu. Website haijafanyiwa updates toka uchaguzi wa 2020, yaani hadi ni aibu.
Noma sana!
Nimesema kama mimi maana sio msemaji wa yoyote. Kwani vipi boss, ama unataka kujigeuza kaka mkuu wetu huku jukwaani nini boss?Kulisema wewe au nani kasema si hoja wala hayapo mashindano ya nani kasema na nani bado.
Hoja ni kuwa huo ni ukweli na unatugharimu.
Siyo huo tu, turudi kwenye drawing board kwanza tukajipange kikamilifu kuchukua nchi sasa.
Hii ikawe rasmi kabisa Sasa na bila kumwonea mtu haya.
Na inawezekana!
Ni kweli tunahitaji mbinu mpya bila kuacha za zamani kama maridhiano uku mmoja akisapot na mwingine akikataa apo mtawachanganya CCM watashindwa waende nanani na nani wamuache uko mbele inabidi Mbowe na Lissu waonyeshe mgawanyiko ili kubeba kila mmoja kundi lake mwisho wa siku wataaungana na kuwaacha CCM midomo wazi.
Swala la kupenya kwenye vyombo vya habari ilo ni gumu kutokana na kilanja Nape kuchagulia vyombo ni habari ipi irushwe ipi iiachwe kwa mazingira ayo itabidi kwenda na social media ili kufikisha ujumbe kwa jamii,
Kumbuka zoezi la kutenganisha dini kubwa na serikali limefanikiwa kwa %nyingi lakini pia kitendo cha kwaacha wenye Watanganyika kudai Tanganyika kupitia Katiba Mpya ni mbinu kali ambayo CCM wameshindwa kuisoma na kuielewa kutokana na Adv.Mwabukusi, Dr.Slaa na Mdude kuongoza kikosi kinachoimega Ccm Katikati uku TEC wakipitia upande wa pili kumalizia kipande cha wanaCCM kuanzia serikalini mpaka kwenye vyombo vya Usalama.
Kinachotakiwa
1.CHADEMA kujijenga kwanza kwa kuunda vikosi kasi vya kulinda kula kila kituo wasiopungua 1000 kwa kila kituo.
2.Kuimarisha kikosi cha propaganda kama mtoa uzi alivyoeleza
3.Kupokea watu wenye ushawishi kwenye CHAMA kwa kusudi maalumu bila kuangalia mazingira yao labda kama ni wezi au wamehusika moja kwa moja kwenye mkataba wa bandari.
4.Kujenga ukaribu na viongozi wa nchi zilizotuzunguka kama Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi na nyingine zenye ushawishi Jumuhia ya Madora
5.Kuwasemea wakulima na wafanyabiashara ambao wanaumizwa na serikali hii bila kusahau watu wa kanda ya Ziwa ambapo kuna wapiga kura wengi.
Mengine wanajua siwezi kuyaweka wazi ila aya naona yanapungua wakifanikiwa apo CCM itabaki kwenye tawi linalosubiri kukatwa.
Jeuri yooote ya CCM iko kwenye Ibara ya 41 (7) ya Katiba yetu,nanukuu:- 'Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa Ibara hii,basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.' Kwa vile Tume ya Uchaguzi inapokea maelekezo toka kwa mamlaka ya uteuzi wake ambaye ni Rais na Mweyekiti wa CCM na ambaye pia ni mgombea wa urais, basi wasimamizi wa uchaguzi wanaweza kufanya rigging ya kiwango chochote kile kwani wanajua tume ikiisha tangaza milango yote ya kisheria kuweza kuhoji wizi huo inakuwa imefungwa automatically. Watu tunapolialia Tume huru na Katiba mpya ni kwa ajili ya uhuni kama huu. Kwa muundo huu wa Tume ya uchaguzi na Katiba hii CCM siku zote wataiba kura na kuchakachua matokeo ya kura za urais kwa vile Katiba ya sasa inatoa kinga kwa uhuni huu.Kuwa na tume huru hakuna maana yoyote kwani kukichezwa rafu anayeamua ni mahakama.
Kama mahakama haikuwekewa mazingira sahihi ya kuwa na uhuru wake kamili malalamiko ya nyani kala mahindi yatamkuta hakimu ngedere kwenye ubora wake. Halafu itakuwa je?
Ni heri kuwa na mahakama huru kuliko hata kuwa na tume huru. Kinacho wabeba Kenya ni mahakama huru.
Zingatia uhuru wa mahakama ni tokea kwenye katiba, uteuzi wa majaji hadi kwenye maamuzi.
Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na hata Rutto wanaijua vyema joto na faraja ya mahakama kuwa huru.
Bila hivyo uchaguzi utaibiwa na hakuna lolote la maana litaidhibiti hali hiyo.
Mbona wilaya ya Nkasi, Jimbo la Nkasi kaskazini rafu za CCM ziligonga mwamba baada ya Wananchi wazalendo kuchachamaa haki itendeke.Nani asiyezijua ghiliba na faulo za CCM? Hii ikiwa tokea kwenye kucheza visivyo na taasisi za umma? Kununua wapinzani na ikibidi hata kukimbia na masanduku ya kura mchana mchana?
Wananchi kote nchini wamechoshwa na uhuni wao huu. Kinachokosekana ni mbadala wa waliodhamiria kufanya kweli kwa vitendo. Siyo kwa maneno!
"Kwamba kote mnakokwenda kuna nyomi la kufa mtu? Kwamba hivyo ni kote hadi usukumani Chatto na hata Kizimkazi, Makunduchi huko?
"Kwani hiyo bado ni habari tena? Tulipo sasa ni kuwa, nyomi ipo; sawa! Halafu?"
CHADEMA Nyomi si Habari Tena, Tujidhatiti kumaliza Mchecho
Pamoja na nyomi lote, mwizi mbobezi wa kura mbona anamaliza mchezo asubuhi na mapema tu? Kwani Ali Bongo au Munangagwa ilikuwaje? Au hata 2015 na pia 2019/20 nako je?
"Ilihitajika katiba mpya yenye mazingira sawa na ya haki kwa wote. Kuna hatari kuwa katiba mpya haitakuwapo kwenye uchaguzi mkuu huu unaokuja."
Kwani ilikuwa ni lazima ufanyike 2024/25?
Inafahamika kuwa ni kwa maslahi ya CCM, katiba mpya isiwepo. Hii angalau iwe hivyo hadi chaguzi za 2029/30.
Cha kujiuliza, "Kwa hiyo?"
"Hata kama kutakuwa na tume huru, bila Mahakama huru, bado ngoma iko pale pale." Kumbe kimbilio letu wakifanya yale mambo yao litakuwa wapi?
Kususia uchaguzi hakuwezi kuwa dili. Alisusa Seif na bado watu wakala kwa raha zao. Labda kama ni kuusimamisha kabisa, wote usiwepo, kama tunaweza.
"Kama kuusimamisha hatuwezi ni muhimu kujipanga kuona tunashinda uchaguzi huu ndani ya rafu zao zote zilizopo. Hii ikiwa zote tunazozijua au hata tunazoweza kuzibashiri.
Kujipanga kwa ushindi ndani ya rafu zao inawezekana. Hata hivyo huko hakuwezi kufanikishwa tokea majukwaani. Sana sana labda kutokea kwenye drawing boards, chini ya wapanga mikakati wabobezi wenye kueleweka.
Kitengo cha habari na propaganda hakiwezi kuwa hiki kilichopo. Kilichopo hakijui habari ni nguvu wala hata hakiijui nguvu ya habari. Hiki hakijui hata namna ya kuzi shape siasa za nchi kuelekea tunakotaka sisi pasipokuwa na kutumia nguvu au bila ya kutumia nguvu kubwa mno.
Hiki kilichopo, kama kipo, hakifai. Akiita jiwe ni jipu!
"Hiki kilikuwa ni cha kuanza nacho."
Kama chama ni muhimu kuwa na namna thabiti ya kuwadhibiti wanachama wake. Wakiwamo hata wale uchwara wa mitandaoni. Ikibidi hata kwa kuwakana hadharani tu, ilikuwa inatosha sana.
Tutamtoa CCM tukishirikiana na wengine bila kujali majina yao ali mradi tunaokubaliana nao kwa wakati husika. Tukawapate wapi malaika, ya Rabi vidampa sisi?!
Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini
Hatutamtoa CCM tukitumia Malaika. Kwenye hilo tunapaswa kuwa wakali kweli kweli, ikibidi hata tukiwa na bakora mikononi.
Chama chenye malengo ya kuchukua nchi hakiwezi kuendekeza upuuzi au hata wapuuzi wachache wenye kujinasibu nacho.
Chama chenye kulenga kuchukua nchi katika hali yetu kinapaswa kudhamiria na kuonekana hivyo ikiwamo hata kwa mwonekano wa usoni tu.
Wawekwe pembeni wote walioko chamani kifursa.
Iwe kazi tu!
Jiwe yeye akisema; "Hapa Kazi tu." Kwa hakika alimaanisha.
Haipo namna nyingine.
Nimesema kama mimi maana sio msemaji wa yoyote. Kwani vipi boss, ama unataka kujigeuza kaka mkuu wetu huku jukwaani nini boss?
Mbona wilaya ya Nkasi, Jimbo la Nkasi kaskazini rafu za CCM ziligonga mwamba baada ya Wananchi wazalendo kuchachamaa haki itendeke.
Nashangaa Chadema hawataki kuja Nkasi kujifunza juu ya namna Umma unaweza kupata unachotaka. Najui akinaTundu, Mbowe, Heche and the like, hawafanyi hivyo wanaogopa mhe. Aidah Kenani asije akawapiku umaarufu.
Chadema kuna kugombaniana vyeo na hili litaibuka tu ktk miaka miwili mitatu ijayo.
Inashangaza Ktk mikutano yao yoote Chadema sijawahi sikia wanaitolea Nkasi mfano ili wilaya nyingine wajifunze na kuiga.
Tundu ndoto zake ni kuwa Rais; Mbowe ndoto zake ni kuwa Rais, n.k. Imbombo jilipo!
Walichofanya Wananchi wazalendo, tena vijana tu wa kati ya miaka 18 - 35 ndicho Chadema wanatakiwa kufanya kama kweli wana Nia ya dhati kuchukua dola mikononi mwa CCM. Nakwambia ile 2020 ndiyo kwa mara ya kwanza nilishuhudia uhalisia wa 'people's power'. Ni hatari!
Polisi walinyoosha mikono, JWTZ walipelekwa, wakasalimu amri. Vijana waliwahakikishia Askari kuwa wangewaua kweli lakini wasingewamaliza wote. Mmh, ilikuwa scenario ya aina yake. Ofisi za DC, DED, Usalama wa Taifa, nyumba za mbunge wa zamani Kessy, DED, OCD zoote zilizingirwa kimkakati (under complete siege) na inasemekana vilipuzi vilivyotengenezwa kienyeji vilikuwa vimeandaliwa tayari kwa mashambulizi yenye uharibifu mkubwa. Alhamdullah intelligence unit ya Serikali ilitoa taarifa mapema juu ya hali halisi ilivyo na inasemekana JPM baada ya kupata taarifa aliagiza matokeo yatangazwe kama yalivyo ili kuiepusha Nchi na machafuko ya aina hiyo kwani vijana ktk wilaya nyingine Nchini wangeiga na Nchi ingewaka moto!
Chadema mnafanya makosa kumdharau huyu binti mpambanaji mhe. Aidah, she is very strategic. Msiogope wala msione aibu kwa sababu ya madigrii yenu kwenda Nkasi kumwomba mhe. Aifah "awapige shule" juu ya namna ya kuing'oa CCM.