Nani asiyezijua ghiliba na faulo za CCM? Hii ikiwa tokea kwenye kucheza visivyo na taasisi za umma? Kununua wapinzani na ikibidi hata kukimbia na masanduku ya kura mchana mchana?
Wananchi kote nchini wamechoshwa na uhuni wao huu. Kinachokosekana ni mbadala wa waliodhamiria kufanya kweli kwa vitendo. Siyo kwa maneno!
"Kwamba kote mnakokwenda kuna nyomi la kufa mtu? Kwamba hivyo ni kote hadi usukumani Chatto na hata Kizimkazi, Makunduchi huko?
"Kwani hiyo bado ni habari tena? Tulipo sasa ni kuwa, nyomi ipo; sawa! Halafu?"
CHADEMA Nyomi si Habari Tena, Tujidhatiti kumaliza Mchecho
Pamoja na nyomi lote, mwizi mbobezi wa kura mbona anamaliza mchezo asubuhi na mapema tu? Kwani Ali Bongo au Munangagwa ilikuwaje? Au hata 2015 na pia 2019/20 nako je?
"Ilihitajika katiba mpya yenye mazingira sawa na ya haki kwa wote. Kuna hatari kuwa katiba mpya haitakuwapo kwenye uchaguzi mkuu huu unaokuja."
Kwani ilikuwa ni lazima ufanyike 2024/25?
Inafahamika kuwa ni kwa maslahi ya CCM, katiba mpya isiwepo. Hii angalau iwe hivyo hadi chaguzi za 2029/30.
Cha kujiuliza, "Kwa hiyo?"
"Hata kama kutakuwa na tume huru, bila Mahakama huru, bado ngoma iko pale pale." Kumbe kimbilio letu wakifanya yale mambo yao litakuwa wapi?
Kususia uchaguzi hakuwezi kuwa dili. Alisusa Seif na bado watu wakala kwa raha zao. Labda kama ni kuusimamisha kabisa, wote usiwepo, kama tunaweza.
"Kama kuusimamisha hatuwezi ni muhimu kujipanga kuona tunashinda uchaguzi huu ndani ya rafu zao zote zilizopo. Hii ikiwa zote tunazozijua au hata tunazoweza kuzibashiri.
Kujipanga kwa ushindi ndani ya rafu zao inawezekana. Hata hivyo huko hakuwezi kufanikishwa tokea majukwaani. Sana sana labda kutokea kwenye drawing boards, chini ya wapanga mikakati wabobezi wenye kueleweka.
Kitengo cha habari na propaganda hakiwezi kuwa hiki kilichopo. Kilichopo hakijui habari ni nguvu wala hata hakiijui nguvu ya habari. Hiki hakijui hata namna ya kuzi shape siasa za nchi kuelekea tunakotaka sisi pasipokuwa na kutumia nguvu au bila ya kutumia nguvu kubwa mno.
Hiki kilichopo, kama kipo, hakifai. Akiita jiwe ni jipu!
"Hiki kilikuwa ni cha kuanza nacho."
Kama chama ni muhimu kuwa na namna thabiti ya kuwadhibiti wanachama wake. Wakiwamo hata wale uchwara wa mitandaoni. Ikibidi hata kwa kuwakana hadharani tu, ilikuwa inatosha sana.
Tutamtoa CCM tukishirikiana na wengine bila kujali majina yao ali mradi tunaokubaliana nao kwa wakati husika. Tukawapate wapi malaika, ya Rabi vidampa sisi?!
Kutokuungwa mkono Bashiru, Polepole, Ndugai na wengine, tujitathmini
Hatutamtoa CCM tukitumia Malaika. Kwenye hilo tunapaswa kuwa wakali kweli kweli, ikibidi hata tukiwa na bakora mikononi.
Chama chenye malengo ya kuchukua nchi hakiwezi kuendekeza upuuzi au hata wapuuzi wachache wenye kujinasibu nacho.
Chama chenye kulenga kuchukua nchi katika hali yetu kinapaswa kudhamiria na kuonekana hivyo ikiwamo hata kwa mwonekano wa usoni tu.
Wawekwe pembeni wote walioko chamani kifursa.
Iwe kazi tu!
Jiwe yeye akisema; "Hapa Kazi tu." Kwa hakika alimaanisha.
Haipo namna nyingine.