Lissu: Polisi hawana sifa ya kuchunguza mauaji yao

Lissu: Polisi hawana sifa ya kuchunguza mauaji yao

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,797
Reaction score
165,543
Haya yamesemwa na Lissu katika mahojiano na gazeti la TanzaniaDaima.

"Katika mazingira ya mauji ya Kinondoni, Jeshi la Polisi ndio mtuhumiwa namba moja. Watuhumiwa hawa watachunguzaje mauaji haya kwa uhuru, uwazi na weledi unaohitajika?

"Ili ukweli wote ujulikane,kunahitajika kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi wa mauji hayo. Tume ya haki za binadamu ina mamlaka hayo Kikatiba na kisheria," alisema Lissu.

Mbunge huyo alisema,"uchunguzi wowote utakaofanywa na Polisi hautakuwa na Credibility yoyote. Ndio maana tayari Polisi na wakubwa wao wa kisiasa wana majibu kwa CHADEMA inahusika hata kabla ya kufanya uchunguzi wenyewe."

Chanzo: TanzaniaDaima(summary)
 
Tatizo la uhai ukitoka huwa haurudi tena. Hata wakichunguza haitasaidia kurudisha uhai wa Akwilina na wengine waliouawa na polisi.
 
Tatizo la uhai ukitoka huwa haurudi tena. Hata wakichunguza haitasaidia kurudisha uhai wa Akwilina na wengine waliouawa na polisi.

Ni kweli uhai wa Akwilina hautarudi, ila wahusika waliofyatua risasi za moto na walio waamuru kufanya hivyo wakiwekwa wazi na kuwajibishwa kisheria itazuia mwingine tena asimfuate Akwilina kwa njia ile ile!
 
Jeshi la polisi limekiri mauji, baadhi wawajibike ama wawajibishwe kwa heshima wafiwa na Watanzania kwa ujumla.
 
Tatizo la uhai ukitoka huwa haurudi tena. Hata wakichunguza haitasaidia kurudisha uhai wa Akwilina na wengine waliouawa na polisi.


Kwa hiyo suluhisho ni kuwaacha waendelee kuua?
 
Ni kweli uhai wa Akwilina hautarudi, ila wahusika waliofyatua risasi za moto na walio waamuru kufanya hivyo wakiwekwa wazi na kuwajibishwa kisheria itazuia mwingine tena asimfuate Akwilina kwa njia ile ile!
Kule Iringa waliua mwandishi David Mwangosi halafu alitoa amri akapandishwa cheo.
 
Lawama ziwaangukie wafuatao, aliyebuni mbinu ya kununua wapinzani, chakubanga kwa kumnunua yule mtumwa, yule mtumwa asingekubali kununuliwa uchaguzi usingerudiwa,msimamizi aliyewanyima wakala wa Chadema hati za utambulisho na mwisho polisi waliotumia risasi za moto kuwapiga waandamanaji.
 
Kumbe punguwani tupo wengi eti[emoji15][emoji15]
Mimi simo katika kundi lenu. Ila najua it won't help or else baada ya mauaji ya mwandishi David Mwangosi kule Iringa usingetegemea mambo haya kutokea tena. Lakini yametokea na kwa aina ya askari wetu ambao kwao busara ni ziro yataendelea kutokea. Hivyo kuamini kama wakijichunguza ndio itakuwa mwisho wa haya wanayoyafanya ndio upunguani wenyewe ambao mimi sio mwanachama
 
Haya mambo bila kufanya action hawa jamaa watatufanya mdoli wa kujifunzia shabaha!watakuwa wanapiga juu inaua chini!
 
Kwa hiyo suluhisho ni kuwaacha waendelee kuua?
Ni kwa vileha waachi tabia hiyo. Wanaua halafu wajichunguze wenyewe kisha wajishitaki wenyewe ndio haisaidii. Kama ni kujifunza na kuacha wangeacha baada ya mauaji ya mwandishi Mangosi kule Iringa.
 
Iv kwani kweli polisi n wengi kuliko raia au mbn tunawaacha sana wanatuzoea iv tukiamua kudeal nao mmoja moja nasi tuseme n watu wasio julikana itakuaje na familia zao watajisikiaje mbona wanajifanya kua wao si binadamu au ndo wakishavaa zile saree akili zinawaruka
 
Tatizo la uhai ukitoka huwa haurudi tena. Hata wakichunguza haitasaidia kurudisha uhai wa Akwilina na wengine waliouawa na polisi.
Watu wote wangekua na akili kama zako nadhani hata ajali za Ndege,Magari,Meli na vinginevyo wasingekua wanahangaika kufanya uchunguzi baada ya ajali,

Investigation inasaidia kuzuwia the same mistake to happen again na muhusika au sababu "root cause" kujulikana.
 
Uchunguzi wa nini tena wakati polisi walishakiri kuua. Chakufanya cheni yao kuanzia waziri hadi mfyatuaji risasi wawajibike
 
Back
Top Bottom