PreGE2025 Lissu! No reforms no election ni sawa lakini zingatia haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika kipindi Cha hivi karibuni Chadema wamezindua kampeni ya 'No reform -No election' (NRNE).

Lissu kama mwenyekiti na icon ya chama amejikita zaidi kuelezea ubovu wa katiba na Sheria mbovu za uchaguzi, zinazopekelea kutokuwa na chaguzi zilizo Huru na Haki (free and fair elections). Hili ni sawa kabisa, na yeyote mwenye uelewa, kuangazia mbele na kulitakia mwema TAIFA hili huku akiweka uchawa na maslahi binafsi pembeni, atakubali kuwa Kuna haja kubwa ya kufanya reforms kwenye tume na namna ya uendeshaji wa chaguzi zetu.

Ili kupata uungwaji mkono wa umma wa watanzania, na kuishinikiza serikali kufanya reforms, Lissu na Chadema Kwa ujumla wakaja na kampeni hii. Aidha, Chadema hawana jeshi, wanategemea nguvu ya umma kushinikiza hili.
Hivyo ili wapate kuungwa mkono na majority ya watanzania (siyo wanachadema tu), Lissu apanue Wigo kutoka katika kuwa gwiji wa sheria na kujipambanua zaidi Kwa wananchi Kwa kuangazia masuala ya uchumi, huduma za jamii na maendeleo ya wananchi. Ajikite kujenga hoja kwa kuwaeleza wananchi mambo yanayo wagusa Moja Kwa Moja kama ajira, huduma za jamii, kilimo, uchumi, rushwa na marekebisho ya Sheria ya mifuko ya jamii hususani NSSF Kwa kurejeshwa fao la kujitoa au kuruhusu mtu kulipwa fedha zake zote anapopoteza ajira ndani ya kipindi Cha miezi Sita, marekebisho juu ya kikotoo n.k.

Yeye kama icon ya chama anapaswa kuwaeleza wananchi jinsi CCM ilivyo shindwa kutatua kero za wananchi, nini CHADEMA itafanya na kwanini wananchi wanapaswa kuiamini CHADEMA na kuikataa CCM, halafu ndo aingize habari za madhaifu ya katiba na chaguzi zetu na mwisho apigilie msumari wa 'No reform -No election'.

Aidha napendezwa na jinsi Heche anavyojenga hoja; anaongelea masuala yanayowagusa wananchi kwa kutoa mifano ya nchi mbali mbali. Na ni Kwa namna gani sera mbovu za CCM na usimamizi duni wa raslimali za TAIFA, unazorotesha maendeleo ya nchi, huku akijenga matumaini ya wananchi juu ya Chadema.

Nakutanabahisha Lissu, usifanye hotuba zako zikatawaliwa na maudhui Moja tu ya uchaguzi. Wananchi wataona huna unachowaletea au kuwatetea zaidi ya kupigania tume huru ili kupata madaraka Kwa manufaa yako ya kisiasa na Chama chako. Pia ukweli mchungu ni kuwa epuka kumtaja taja Magufuli, pamoja na madhaifu na madhila yote ya Magufuli bado Kwa watanzania walio wengi ikichagizwa na Madhaifu ya awamu hii ya mama, Magufuli amekuwa branded au kuonekana kama mtetezi wa wanyonge na shujaa wa watanzania. (Though he was fickle, dictator, impassive and sadist. But you can not ignore public sentiments in regard to him).

Katika ulingo ya siasa unapaswa kuangazia mambo yafuatayo:
1. Tambua na kuzungumzia changamoto au matatizo yanayoikabili jamii ya eneo husika na TAIFA Kwa ujumla. (Addressing social problems)
1. Taja Madhaifu ya mpinzani wako, Kwa Chadema Mpinzani wao ni CCM . (Disreputation of your opponent)
2. Toa hoja au sera mbadala kushughulikia changamoto zinazoikabili jamii. (Suggest alternatives or solutions)
3. Jenga matumaini ya wananchi juu yako au Chama chako.(Instill hopes)
**********************************

Nakala Kwa: Erythrocyte , Pascal Mayalla , Bams , Yericko Nyerere , Yoda , johnthebaptist 'et al'
Hiyo kazi wamemuachia Heche.Hat hivyo Chadomo hawanaga watu Waziri kwenye maeneo ya Uchumi na Biashara,Wamewekeza sana kwenye mambo ya sheria na propaganda Kwa sababu za kujihami na rungu la Dola.

Wangepata mtu kama Zito au Kafulira ingewasaidia au wanikodi Mimi niwe nawasaidia wanipe mpunga 😆😆

Kazi ya mambo ya sera za Uchumi wanaoweza vyema kabisa ACT Wazalendo,hata CCM hawana kitu wanaotegemea zaidi makada waliokuwa Watumishi wa Umma.
 
Mtoa mada umewahi kidogo, hayo yote ni mema lkn wakati wa kuyasema kwa manasiasa wanaojielewa muda wake bado, stay tuned
 
Mtu yeyote timamu akimsikiliza slaa ,heche na lema,tundu lissu unajua kabisa Wana brainy kubwa na ni watu wenye Marengo mema na hili TAIFA
uko sahihi lakini bahati mbaya mfumo wetu wa nchi ulivyosetiwa kwenye sheria,uchaguzi na uongozi wenye maslahi kwa taifa hao wenye brain kubwa uliowataja mfumo wetu wa sasa hauwahitaji wala hauwezi kuwatumia kwa faida ya nchi zaidi ya kuwapiga vita hivyo ni ngumu sana hawa brain kubwa kupata nafasi..mfumo wetu umejaa vilaza watupu wasio na maono zaidi ya kupiga madili kwani uongozi umefanywa kama fursa za ulaji kwao na vizazi vyao tu na biashara ya udalali wa rasilimali za nchi ..tungekuwa na taasisi ya usalama na jeshi serious hawa washenzi wasingekuwa wanachezea nchi namna hii ya ajabu yaani ni kinyaa hata kuyasikia..na bahati mbaya zaidi watanzania wengi tunawataka walio kwenye huo mfumo mbovu unaowanufaisha eti ndio wafanye hizo Reform tangu lini mtu akate mkono unaomlisha.!
 
eti free and fair election ,degree mzima unakuja na civics ya form tu hapa ongezea neno credible

andika hivi,free ,fair and credible election
 
Walioandika hicho kitabu Cha civics form two (na siyo form tu uliyo andika) ni masters and PhD holders, kwahiyo siyo mbaya kwangu kuja na hiyo elimu ambayo kwako unaniona iko chini lakini Kwa upeo wangu inatosha kueleweka Kwa wanajukwaa. Nashukuru pia Kwa kuongezea neno credible, vipi hilo neno liko civics ya form ngapi bhana, au ni GS ya form 5-6 au ni DS ya 1st to 3rd year pale jalalani.!!?
 
Hiyo kazi wamemuachia Heche.Hat hivyo Chadomo hawanaga watu Waziri kwenye maeneo ya Uchumi na Biashara,Wamewekeza sana kwenye mambo ya sheria na propaganda Kwa sababu za kujihami na rungu la Dola.

Wangepata mtu kama Zito au Kafulira ingewasaidia au wanikodi Mimi niwe nawasaidia wanipe mpunga 😆😆

Kazi ya mambo ya sera za Uchumi wanaoweza vyema kabisa ACT Wazalendo,hata CCM hawana kitu wanaotegemea zaidi makada waliokuwa Watumishi wa Umma.
Mambo mengine unajitolea tu, hususani Yale ya ukombozi wa nchi yetu. Hebu fikiria akina Mzee Rupia na Abduwakili Sykes walijitolea kumchangia na kumwezesha Nyerere wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika. Au yeye Nyerere binafsi aliacha kazi yenye mshahara na kujiunga na harakati za ukombozi ambayo Kwa wakati huo ilikuwa ya kujitolea. Kwahiyo mkuu mengine waweza jitolea tu.
 
Mimi sio shabiki sana ya vyama vya siasa ila napenda haki.Niwasikiavyo Tundu na Heche nawaona wamegawana mmoja akizungumzia udhaifu wa kanuni za uchaguzi na mwingine sababu za umasikini wa wananchi pamoja na huduma mbovu.
 
Walioandika hicho kitabu Cha civics form two (na siyo form tu uliyo andika) ni masters and PhD holders, kwahiyo siyo mbaya kwangu kuja na hiyo elimu ambayo kwako unaniona iko chini lakini Kwa upeo wangu inatosha kueleweka Kwa wanajukwaa. Nashukuru pia Kwa kuongezea neno credible, vipi hilo neno liko civics ya form ngapi bhana, au ni GS ya form 5-6 au ni DS ya 1st to 3rd year pale jalalani.!!?
jitahidi Kwa levo Yako credible usiiache
 
Back
Top Bottom