Lissu na mahubiri ya Haki, Uhuru na Usawa

The king mswati

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
787
820
Kama kichwa kinavyojieleza, Mh. Tundu Lisu kwenye kampeni zake amekuwa akihubiri sana kuhusu, Haki, uhuru na usawa. By the way yuko sahihi lakini huyu mnyaturu mwenzangu wa huku Ikungi Singida bado hajanishawishi mimi kwenye hili suala mimi nimpigie kura, bado kabisa kwa sababu hii suala la Haki, uhuru na usawa ni kweli linatakiwa kuwepo ila inabidi liwe na mipaka yake, huu ni ukweli usiopingika.

Lazima haki, uhuru na usawa viwe na mipaka kulingana na misingi ya nchi ilivyojengwa. Ukiruhusu demokrasia sana, uhuru sana, usawa sana believe me nchi haiwezi kwenda mbele hata kidogo, zaidi tutaishia kuzozana tu hatutofanya maendeleo yeyote ya maana. Nawapeni mfano mdogo tu, angalieni nchi kama Urusi, China, Ufalme wa Saudia Arabia na Libya ile ya kipindi cha Gadaffi, nchi hizi zilipiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kipindi zinatawaliwa kibabe sana.

Siyo kwamba uhuru haki na usawa havikuwepo; no, vilikuwepo ila vilikuwa na mipaka yake. Urusi imeanza kuwa taifa lenye nguvu ya kiuchumi, technolojia, viwanda na kijeshi ikiwa chini ya Kiongozi mbabe Joseph Stalin ambae alitawala tangu 1924 hadi alipokufa 1954, na Urusi ilianza kuwa tishio sana kwa nchi za Ulaya na Marekani kipindi cha utawala wa huyu jamaa na marekani ilimwogopa vibaya mno, huyu alikuwa mbabe kuliko hata Vladmir Putin anaetawala Urusi ya sasa.

The same ukija China walikuwa na Mao ze Dong alitawala kibabe hadi China ikatoboa, mpaka leo china bado inaongoza kwa record ya kunyonga watu hadi kufa (hasa wala rushwa) duniani kuliko nchi yeyote ile kila mwaka, si kwamba hawana demokrasia bali ina mipaka ya demokrasia.

Njoo kwenye ufalme wa Saudia arabia, wambea wambea kama Lisu wanatandikwa vibaya mno ili nchi iende mbele, Njoo libya ya Gaddafi wote tunajua, Ubabe ulikuwepo ili nchi iende mbele.

Kwa hiyo sisemi kwamba haki isiwepo, uhuru usiwepo, au usawa usiwepo bali mimi nazungumzia mipaka ya hivi vitu, maana Lissu anataka kutuaminisha haki, uhuru na usawa kwa level ambayo haiwezo kuwepo hata siku moja, sisi tunahitaji maendeleo mambo ya haki, uhuru na usawa ni umbea tu kufarakanisha watanzania maana kama ni uhuru tunao, haki ipo kwa kiasi chake haki hizo nyinginezo tutazikuta Mbinguni maana kama unaa akili Duniani hakunaga haki, na hakuna nchi yenye haki zote Duniani.

Bora tu kura yangu irudi kwa Magufuli hata kama walitaka kukuua ila huenda walifanya hivyo kuiokoa Tanzania (maana huwezi jua), bora tu nimpe mzee wa anaehubiri Tanzania ya viwanda, Tanzania isiyopangiwa mambo na mabepari kuliko nikupigie ww kura ukawalete wakoloni waanze kuiba tena rasilimali zetu, uturudishe kwenye mikataba ya madini isiyoeleweka ambayo magu alishaivunja, dhahabu yetu ianze kwenda tena Japan sijui China tukidanganywa eti ni mchanga (sijui ni mchanga gani huo unaosindikizwa na askari wenye bunduki)

Acha tu nimchague Magufuli hata kama nimesoma niko mtaani sina ajira, ila wewe unanitia wasiwasi sana mahubiri yako ya haki na urafiki na mabepari.
 
Unahangaika bure magu ameshachafuliwa sana hasafishiki tena unga juhudi za Lissu za kuirudisha nchi kwenye misingi ya haki na utawala bora.
 
Mfano nikikuuliza ni haki gani ambayo ww unaitaka na ambayo kwenye utawala wa magufuli umeikosa, sina hakika kama utakuwa na majibu ya maana 🤔🤔🤔
 
Anachohubiri ni ulaghai wa kiwango cha PHD kwa sababu hata kwenye chama chake hiyo haki,usawa na uhuru havipo.

Chama chake kianze kutekeleza hiyo slogan kwa vitendo.
 
Binafsi zaidi ya uhuru hakuna lingine kutoka kwa mgombea wa CDM alichoweza kunishawishi.

Amechukulia upungufu wa Magufuli ambao unafahamika lakini kwenye mengine bado sijashawishika.
 
Kama kichwa kinavyojieleza, Mh. Tundu Lisu kwenye kampeni zake amekuwa akihubiri sana kuhusu, Haki, uhuru na usawa. By the way yuko sahihi lakini huyu mnyaturu mwenzangu wa huku Ikungi Singida bado hajanishawishi mimi kwenye hili suala mimi nimpigie kura, bado kabisa kwa sababu hii suala la Haki, uhuru na usawa ni kweli linatakiwa kuwepo ila inabidi liwe na mipaka yake, huu ni ukweli usiopingika.

Lazima haki, uhuru na usawa viwe na mipaka kulingana na misingi ya nchi ilivyojengwa. Ukiruhusu demokrasia sana, uhuru sana, usawa sana believe me nchi haiwezi kwenda mbele hata kidogo, zaidi tutaishia kuzozana tu hatutofanya maendeleo yeyote ya maana. Nawapeni mfano mdogo tu, angalieni nchi kama Urusi, China, Ufalme wa Saudia Arabia na Libya ile ya kipindi cha Gadaffi, nchi hizi zilipiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kipindi zinatawaliwa kibabe sana.

Siyo kwamba uhuru haki na usawa havikuwepo; no, vilikuwepo ila vilikuwa na mipaka yake. Urusi imeanza kuwa taifa lenye nguvu ya kiuchumi, technolojia, viwanda na kijeshi ikiwa chini ya Kiongozi mbabe Joseph Stalin ambae alitawala tangu 1924 hadi alipokufa 1954, na Urusi ilianza kuwa tishio sana kwa nchi za Ulaya na Marekani kipindi cha utawala wa huyu jamaa na marekani ilimwogopa vibaya mno, huyu alikuwa mbabe kuliko hata Vladmir Putin anaetawala Urusi ya sasa.

The same ukija China walikuwa na Mao ze Dong alitawala kibabe hadi China ikatoboa, mpaka leo china bado inaongoza kwa record ya kunyonga watu hadi kufa (hasa wala rushwa) duniani kuliko nchi yeyote ile kila mwaka, si kwamba hawana demokrasia bali ina mipaka ya demokrasia.

Njoo kwenye ufalme wa Saudia arabia, wambea wambea kama Lisu wanatandikwa vibaya mno ili nchi iende mbele, Njoo libya ya Gaddafi wote tunajua, Ubabe ulikuwepo ili nchi iende mbele.

Kwa hiyo sisemi kwamba haki isiwepo, uhuru usiwepo, au usawa usiwepo bali mimi nazungumzia mipaka ya hivi vitu, maana Lissu anataka kutuaminisha haki, uhuru na usawa kwa level ambayo haiwezo kuwepo hata siku moja, sisi tunahitaji maendeleo mambo ya haki, uhuru na usawa ni umbea tu kufarakanisha watanzania maana kama ni uhuru tunao, haki ipo kwa kiasi chake haki hizo nyinginezo tutazikuta Mbinguni maana kama unaa akili Duniani hakunaga haki, na hakuna nchi yenye haki zote Duniani.

Bora tu kura yangu irudi kwa Magufuli hata kama walitaka kukuua ila huenda walifanya hivyo kuiokoa Tanzania (maana huwezi jua), bora tu nimpe mzee wa anaehubiri Tanzania ya viwanda, Tanzania isiyopangiwa mambo na mabepari kuliko nikupigie ww kura ukawalete wakoloni waanze kuiba tena rasilimali zetu, uturudishe kwenye mikataba ya madini isiyoeleweka ambayo magu alishaivunja, dhahabu yetu ianze kwenda tena Japan sijui China tukidanganywa eti ni mchanga (sijui ni mchanga gani huo unaosindikizwa na askari wenye bunduki)

Acha tu nimchague Magufuli hata kama nimesoma niko mtaani sina ajira, ila wewe unanitia wasiwasi sana mahubiri yako ya haki na urafiki na mabepari.
Uzuri hauna mipaka.
 
Mfano nikikuuliza ni haki gani ambayo ww unaitaka na ambayo kwenye utawala wa magufuli umeikosa, sina hakika kama utakuwa na majibu ya maana 🤔🤔🤔
Sijapata haki ya kuongezewa mshahara kila mwaka tangu aingie madarakani ameongeza Mara moja tu.
 
🤣🤣🤣 hiyo siyo haki broo.... Serikali inaweza hata kushusha mshahara wako pale inapobidi kufanya hivo, angalia haki za raia kwa ujumla acha kujiangalia ww kama ww, inaonekana ww mbinafsi sana 🙂🙂🙂
 
Binafsi zaidi ya uhuru hakuna lingine kutoka kwa mgombea wa CDM alichoweza kunishawishi.

Amechukulia upungufu wa Magufuli ambao unafahamika lakini kwenye mengine bado sijashawishika.
Uko sahihi nakuunga mkono kwa asilimia mia 💪💪💪, na always hatuwezi pata kiongozi ambae amekamilika kwa asilimia mia ila walau mazuri ya magufuli ni mengi kuliko madhaifu yake, full stop, Alafu nimeskia akisema kuwa akipewa ridhaa ya kuingia ikulu (Lisu) basi atawarudisha kazini wote waliotumbuliwa kwa vyeti feki, sasa sijui anawarudisha wakafanye nn wakati waliingia kazini kiharamu haramu, xometime nakuwa sikumelewi huyu jamaa zaid ya uhuru anaoutaka na katiba mpya labda, ila tofaut na hapo hajanishawishi kabisa 🤔🤔🤔
 
Uzuri gani unauzungumzia, hujaeleweka ebu weka sawa hoja yako 🤔🤔🤔
Wewe unataka kuweka mipaka kwenye tunu kama haki, embu tueleze unataka kuweka mipaka gani kwenye haki ya mtu. Huwezi kumpa mtu nusu haki au hata 99% ya haki yake, unapaswa kumpa mtu 100% ya haki yake.
 
Haki ya msingi ya mwanadamu ni kuishi tu, zingine ni ziada 🙂🙂🙂
 
Back
Top Bottom