Pengine kuna umuhimu wa kuwepo na ufahamu, hata kama haukusemwa waziwazi, ili watu waelewe kwamba kama kuna kikundi cha watu, iwe ni kwa dhamira yao wenyewe, au kwa kutumwa na mamlaka wanaoendelea na mipango ya kudhuru wananchi wenzao, wao pia waanze kujitambua kwamba hawatakuwa salama wanapofanya mipango ya namna hiyo.
Hii lugha ni muhimu ianze kueleweka na watu wasitilie shaka juu yake.
Kama serikali inao wajibu wa kulinda usalama wa raia zake, lakini ikaamua kwa maksudi kutotimiza wajibu wake huo kwa baadhi ya watu (raia zake), kwa vile tu hao watu wana misimamo tofauti na wao, basi wajibu wa hao wanaowindwa ni wao kujilinda kwa njia yoyote ile inayofaa.
CHADEMA ni lazima wawe na utaratibu maalum wa kuwalinda viongozi wao. Atakayethubutu kuwatisha na kuwadhuru, afanye hivyo akiwa na ufahamu kwamba atalipa uovu huo kwa uovu kwa njia moja au nyingine.