LISSU KUACHIWA AGOSTI 21? MAJAJI KUAMUWA KAMA ANA KESI YA KUJIBU AU LA SIKU YA IJUMAA
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Agosti 17, 2026 kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 21, 2026 siku ya Ijumaa ambapo Majaji watatu wataamuwa kama Tundu Lissu ana kesi ya kujibu au la.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 248
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji ni muhimu kukumbuka kuwa, mimi ni mshtakiwa pekee katika kesi hii na ikumbukwe katika kesi ya Khatibu Gandi inasema maneno ya mtu mmoja, hayatengenezi uhaini, kwa ushahidi uliotolewa haujathibisha nia ya kutenda kosa la uhaini then on the basis kuwa kusipokuwa na primafacie case nitaitwa nijitetee kwa kipi?
Ni ushahidi gani nisipojitetea utanitia hatiani? Ushihidi ukoje kuhusu publication ya reasonable act?
Lazima kuwe na ushahidi wa machapisho au matendo ya wazi wakati wa pre trial Upande wa Mashtaka wanasema mimi nilichapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV, hivyo uthibitisho wa haya maneno ulitakiwa uwepo Jambo Tv.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwaelekeze ukurasa wa 185 wa record za Mahakama, upande wa mashtaka ulionyesha ushahidi wa nyaraka 9 na aina 2 za vielelezo ikiwemo Video clips, hawajaleta hata moja.
Shahidi PW 17 ni shahidi pekee wa eye witness aliyenishuhudia kwenye mkutano, testimony ya mashahidi, shahidi PW 17 ndiyo shahidi mwenye ushahidi mzito, alisema yeye na wenzake watano ndiyo waliorecord na kurusha, amesema kwa maneno yake na kwa maandishi kupitia kielelezo D16 na ni shahidi wao, Kwahiyo kama ni tuhuma ya publication siyo yak wangu, aliyepublish ni PW 17 na amesema mpaka leo vipo kwao.
Ushahidi wa nani aliyechapisha hawajaujibu.
Waheshimiwa Majaji, walidai ooh wewe ndiye uliyeitisha Mkutano, shahidi wao PW 17 amesema mwaliko waliupata kwa afisa habari wa Chadema anaitwa Brenda Rupia, na nikamuuliza uliniona mimi nikifanya maandalizi nikipanga viti akasema, hakuna.
Kwenye hili suala la tatu hawajathibitisha kabisa kosa la kuchapisha maneno.
Naomba nimalizie,
Kama hakuna proof ya kucommint treason act, hakuna intention maana yake ni kuwa hakuna primafacie case, na kama hakuna primafacie case mkiruhusu nijitetee mtakuwa mnafanya makosa ya kisheria.
Sasa Waheshimiwa majaji msipokubali mnafanyaje? Mnafanya kile ambacho sheria imewataka mfanye kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) kufanya finding ya kuwa hakuna case ya kujibu.
Waheshimiwa Majaji naomba kama mtatoa huo uamuzi muutoe leo, kama mnaridhika na hoja hii, reason ruling mtatupa baadae, hakuna haja ya mimi kurudishwa Ukonga leo. Hili ni la pili;
La 3 lipo kwenye kifungu cha 367 cha CPA (Sheria ya Makosa ya Mwenendo wa Jina), kama mashtaka ni ya uonevu ya kusingizia mnaweza kuamuru mtuhumiwa alipwe fidia, haya maumivu yangu na familia yangu nani atafidia?? mashahidi wote 17 mmewasikia.
Hivyo naomba iamriwe kuwa sina kosa la kujibu pia ipangwe tarehe nije kuthibitisha madai/ fidia yangu.
Naomba niwape Waraka wa kikosi kazi wa Umoja wa Mataifa, uamuzi wa tarehe 23/2/2026 unaosema niachiwe mara moja na kulipwa fidia. Hivyo Waheshimiwa Majaji msimamo ni kuwa hakuna primafacie case na kwakuwa hakuna Primafacie case, sheria inawataka muandike findings ya NO CASE TO ANSWER
Waheshimiwa majaji ya kwangu ni hayo tu.
Mhe. Lissu anamaliza na kuketi.
Jaji Ndunguru : Ehee Jamhuri ?
Wakili wa serikali Katuga anasimama anasema Upande wetu kwanini tunaona mshatikiwa ana kesi ya kujibu ni kutokana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) (d)
Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...
"WANASEMA KITU KIMOJA SAHIHI HAPA, WANASEMA TUTAHAMASISHA UASI, NI KWELI TUTAHAMASISHA UASI, TUTAKINUKISHA VIBAYA......"
Waheshimiwa DPP Vs Philipo Joseph Mtonda, 217 Rufaa ya jinai, Tanzlii 2021.... case hii ili cite case Tambaklal na ikarudia maneno ya hiyo Landmark cases ya Tambklal case.