Lissu is too shallow compared to Prof Kabudi

Nimekushauri tu. Najua kuwa wewe ni mmoja wa wanaJF wanaopenda kurefusha mada zao na kuzitetea hata kama wameandika 'pumba'. Shaurika!
Huyu hakuwa na chakuchangia humu leo.

Ni wale ambao hupenda kuanzisha mada ili aonekane ana replies nyingi.

Akiendelea hivi Nitamuweka kwenye kundi la nisiosoma mada zao kama gudume, beira boy, demiss, shunie nk
 
Asante Petro.

Lkn mimi nataka niende nje ya mada kidogo.

Kwanini wanasheria wa humu JF hamtusaidii pale mijadaya ya kisheria inapozuka na kuleta ukakasi kwenye jamii??

Ni uvivu? Uoga? Au kutokujua??
Mkuu, mimi si mmojawapo. Mara nyingi tu huchangia, kwa maana ya kuchambua, au huanzisha mada za kisheria. Please acknowledge!😀

Mifano:
1.Jicho la kisheria: Kumsweka rumande mwananchi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa/Wilaya - JamiiForums

2. Mita 200: Jicho la kisheria (Tafsiri yangu binafsi) - JamiiForums

3. Uteuzi wa Wabunge 10: Jicho la kisheria - JamiiForums
 
Kuwa na mjadala huu inamaana Lissu sio wa mchezo mchezo!
Huwezi kuuliza kati ya Real Madrid Na Yanga ipi timu bora!!!!!Utaonekana kichaa!!
Utapaswa uweke mjadala wa Real Madrid na Barcelona ndio watu wataanza kujadili!!!
 
Kuwahi kusoma si kigezo cha kwamba unajua kila kitu; kifupi Lissu yuko vzr mno; we ulijua hayo aliyoyasema Lissu?

Lissu mi lilishamkubali kitambo sana alivyosema hakuna UGAIDI wa chini ya idadi ya watu wawili ... mijamaa ya upande wa pili ikabakia midomo wazi.
 
Ukiangalia wale wanao mshabikia Lissu wengi ni Vilza tu
Hakuna wajualo zaidi ya ushabiki na Kufuata mkumbo
Kabudi ni level nyingine kabisa
 
Hamna na hamtaweza kusikiliza maoni yake kwa sababu ni tishio kiupande wenu utawezaje kumsikiliza mtu unaemuona ni adui yako.
Tishio?unataka kusema yeye anamiliki jeshi na vifaa vya kijeshi.
 
Ungeeleweka vizuri kwa kutoa mifano, bila mifano inakuwa ni bytes tu zinapotea na zoezi la vidole.
 
Lissu ni mropokaji na mpiga kelele tu hajui lolote kinacho mbeba ni kwamba wananchi wanahamu kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi na kiutawala.
una maana hata mahakamani anako shida kesi huwa analopoka tu mahakimu wanamuelewa, wanasheria wa serikali nao wanamwelewa mkuu acha utani basi

Yule bwana anajua sana, ukichanganya na sauti ya mamlaka aliyo jaaliwa basi ni raha sana
 
Lissu ni mropokaji na mpiga kelele tu hajui lolote kinacho mbeba ni kwamba wananchi wanahamu kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi na kiutawala.
Wewe mabadiliko hayo huyataki yatokee?
 
Ulichoandika hakina mashiko ya kisheria na kimantiki zaidi ya kuonesha ushabiki na mapenzi yako binafsi au ya kundi lako kwa kabudi. Sijaona hoja yoyote ya kuwalinganisha hao wawili kisheria maana hakuna mahali wanapokutana kwenye masuala ya sheria zaidi ya kwenye siasa! Siasa imesheheni uwongo uwongo mwingi na maneno matamu.
 
Kabudi ni mwalimu, ilitegemewa amwage shule.
Lisu ni nationalist fanatic, someone with fire in his stomach to persue his cause even after so many bullets.
Mpunguzieni kabudi mshahara kidogo alafu tuone shule atakayoitoa.
 
Wew unajulikana ni moja ya watu wanaotamani Lisuu apotee
 
Kuwa na mjadala huu inamaana Lissu sio wa mchezo mchezo!
Huwezi kuuliza kati ya Real Madrid Na Yanga ipi timu bora!!!!!Utaonekana kichaa!!
Utapaswa uweke mjadala wa Real Madrid na Barcelona ndio watu wataanza kujadili!!!
Hahahaha umemaliza mjadala mkuu
 
una maana hata mahakamani anako shida kesi huwa analopoka tu mahakimu wanamuelewa, wanasheria wa serikali nao wanamwelewa mkuu acha utani basi

Yule bwana anajua sana, ukichanganya na sauti ya mamlaka aliyo jaaliwa basi ni raha sana
Kule huwa na heshima,anaheshimu mahakama....

Ila anavyo ishauri serikali hutumia command hatakama anajenga hoja,ila uwasilishaji wake sasa.

Nyerere aliwahi kusema hatakama baba ana njaa unapompelekea ugali utengeneze vizuri ili umvutie ukipeleka ugali una sura ya hovyo hovyo hata hamu ya kula itaisha.
 
Tukiacha ushabiki wa kisiasa Lissu ni mweupe mno huwezi kumlinganisha na Prof. Kabudi. Lissu makelele ndiyo yanayombeba.
 
Kabudi ni mwalimu, ilitegemewa amwage shule.
Lisu ni nationalist fanatic, someone with fire in his stomach to persue his cause even after so many bullets.
Mpunguzieni kabudi mshahara kidogo alafu tuone shule atakayoitoa.
Mshahara mbali elimu mbali. Kuna ambao hawakugusa shule kabisa lakini leo hii ni mamilionea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…