Lissu: Hoja ya jambo muhimu unaijenga kwenye uongo

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,529
2,000
Mwanasheria Msomi Tundu Lissu ameendelea kulichambua swala la madini nchini huku akionesha kutokubaliana na namna Serikali inavyoliendea swala hili. Akizungumza katika mahafali ya CHASO Dodoma jana Lissu amesema hapingi kila kitu kinachofanywa na Magufuli bali anapingana na namna swala la madini linavyoshughulikiwa. Lissu amesema baadhi ya vitu anavyopinga ni namna swala hilo linavyofanywa kisiasa na katika msingi wa uongo hali ambayo amesema inatudhalilisha na kutufanya tuonekane kituko na kwamba huko nje wanatucheka.

Akifafanua zaidi Lissu amesema hoja ya uongo ni namna ambavyo kamati ya Rais ya Profesa Mruma na ile ya Orosso ilivyodanganya umma na dunia kwa ujumla. Lissu anasema kwake hizo ripoti ni professorial rubbish kwa sababu zimesema uongo. Lissu anasema Profesa Mruma alikuwa mjumbe wa kamati ya Jaji Bomani na yeye ndiye aliyepeleka takwimu za madini kwenye kamati kupitia taasisi anayoiongoza ya Geological Survey of Tanzania (GST) na takwimu alizozipeleka kwenye kamati ya Jaji Bomani na anazozitoa sasa ni tofauti. Tazameni taarifa zilizopo GST taasisi ambayo Profesa Mruma ndiye bosi halafu angalieni alichokuja nacho kwenye kamati ya Rais ni uwongo. Je ni nani anayedanganya kati ya kamati ya Rais ya Mruma au ile ya Bomani? Je ni nani anayedanganga kati ya GST na kamati ya Mruma?.
Tundu Lissu anasema huwezi kupambana na wazungu kwa hoja dhaifu tena za uongo na kwa matamko ya kisiasa na usikubali wazungu wakuambie kwamba unavunja sheria utaumia. Madini ya Tanzania yanajulikana na zaidi Bulyanhulu STAMICO wamefanya exploration toka 1977. Kama kamati ya Mruma ingekuwa ni kweli basi Bulyanhulu ingekuwa inaongoza duniani kwa dhahabu. Kwa hapa Tanzania Bulyanhulu siyo ya kwanza ni ya pili baada ya Geita na hizi ni taarifa za GST ambayo inaongozwa na Mruma.

Kwa upande mwingine Lissu amesema kwamba kuna watu hawamwelewi wanasema amehongwa jambo ambalo halishangai maana hajaeleweka miaka 18 hashangai kutokueleweka hata leo.
Kwa upande wake Rais Magufuli kabla ya yote anapaswa

1. Ajitoe kwenye mikataba ya kimataifa ya kulinda wawekezaji mfano MIGA.

2.Abadilishe sheria za ndani za madini.

3. Ndipo apitie mikataba pamoja na wawekezaji ili iendane na sheria mpya kwa manufaa ya watanzania.

Lissu anasema hakubaliani na utaratibu uliotumiwa na Magufuli kwani unaweza kuiingiza nchi kwenye matatizo akitolea mfano wa Zimbabwe na Venezuela. Wanasema nawatisha mimi natoa tahadhali tu " wanasema mbona hawajaenda mahakamani ...ole wenu wakienda". Lissu alisema kilichofanyika kuzuia mchanga hakijafuata utaratibu na kwamba hiyo inaweza kupelekea ACACIA wakaenda mahakamani kudai fidia na kwamba tutakuwa hatuna pa kuponea maana tumevunja mkataba na sheria zetu wenyewe.

Lissu anasema tuliwakabidhi Mali zetu kisheria lazima tuzirudishe kisheria.
 
Magonjwa Mtambuka

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
23,422
2,000
Mwanasheria Msomi Tundu Lissu ameendelea kulichambua swala la madini nchini huku akionesha kutokubaliana na namna Serikali inavyoliendea swala hili. Akizungumza katika mahafali ya CHASO Dodoma jana Lissu amesema hapingi kila kitu kinachofanywa na Magufuli bali anapingana na namna swala la madini linavyoshughulikiwa. Lissu amesema baadhi ya vitu anavyopinga ni namna swala hilo linavyofanywa kisiasa na katika msingi wa uongo hali ambayo amesema inatudhalilisha na kutufanya tuonekane kituko na kwamba huko nje wanatucheka.

Akifafanua zaidi Lissu amesema hoja ya uongo ni namna ambavyo kamati ya Rais ya Profesa Mruma na ile ya Orosso ilivyodanganya umma na dunia kwa ujumla. Lissu anasema kwake hizo ripoti ni professorial rubbish kwa sababu zimesema uongo. Lissu anasema Profesa Mruma alikuwa mjumbe wa kamati ya Jaji Bomani na yeye ndiye aliyepeleka takwimu za madini kwenye kamati kupitia taasisi anayoiongoza ya Geological Survey of Tanzania (GST) na takwimu alizozipeleka kwenye kamati ya Jaji Bomani na anazozitoa sasa ni tofauti. Tazameni taarifa zilizopo GST taasisi ambayo Profesa Mruma ndiye bosi halafu angalieni alichokuja nacho kwenye kamati ya Rais ni uwongo. Je ni nani anayedanganya kati ya kamati ya Rais ya Mruma au ile ya Bomani? Je ni nani anayedanganga kati ya GST na kamati ya Mruma?.
Tundu Lissu anasema huwezi kupambana na wazungu kwa hoja dhaifu tena za uongo na kwa matamko ya kisiasa na usikubali wazungu wakuambie kwamba unavunja sheria utaumia. Madini ya Tanzania yanajulikana na zaidi Bulyanhulu STAMICO wamefanya exploration toka 1977. Kama kamati ya Mruma ingekuwa ni kweli basi Bulyanhulu ingekuwa inaongoza duniani kwa dhahabu. Kwa hapa Tanzania Bulyanhulu siyo ya kwanza ni ya pili baada ya Geita na hizi ni taarifa za GST ambayo inaongozwa na Mruma.

Kwa upande mwingine Lissu amesema kwamba kuna watu hawamwelewi wanasema amehongwa jambo ambalo halishangai maana hajaeleweka miaka 18 hashangai kutokueleweka hata leo.
Kwa upande wake Rais Magufuli kabla ya yote anapaswa

1. Ajitoe kwenye mikataba ya kimataifa ya kulinda wawekezaji mfano MIGA.

2.Abadilishe sheria za ndani za madini.

3. Ndipo apitie mikataba pamoja na wawekezaji ili iendane na sheria mpya kwa manufaa ya watanzania.

Lissu anasema tuliwakabidhi Mali zetu kisheria lazima tuzirudishe kisheria.
Hapo ndio kalihutubia taifa?
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,021
2,000
Lissu ni mtu makini na anaejua mengi kuhusu mambo ya madini kwa muda mrefu.
Tatizo lipo kwa ccm ambao ndio wezi wa RASLIMALI zetu. Lkn wezi hawa wa ccm kupitia wabunge wa ccm (mayuda iskarioti) wamekuwa wakipitisha mambo haya ya kipuuzi kama vile nao hawana watoto watakaoumia.
Mfano mwingine ni mswada wa dharura wa GESI ulivyopitishwa kwa DHARURA na haraka na hawa MAYUDA ISKARIOTI wetu ikiwa haina faida kwa nchi bali kwa wezi wa nje. KIBAYA KABISA WALIHONGWA KILA MBUNGE WA CCM ili wapitishe mikataba hiyo.
 
kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,139
2,000
Eti huko nje wanatucheka!!!!Huyu Lissu mnafiki sana,huyu si ndio alisema Tutashitakiwa?Nchi itakuwa kama Zimbabwe?
Ni Lisu huyo huyo alieanza kuzungukia migodi akiwa mwana harakati akipinga unyonyaji wa hao wazungu wa migodi.
Hajabadirika kamwe, ni yule yule aliepiga kelele kuhusu mikataba kupitishwa kwa hati ya dharula.
Hajawahi kubadirika.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom