Lissu: Hoja ya jambo muhimu unaijenga kwenye uongo

Mwanasheria Msomi Tundu Lissu ameendelea kulichambua swala la madini nchini huku akionesha kutokubaliana na namna Serikali inavyoliendea swala hili. Akizungumza katika mahafali ya CHASO Dodoma jana Lissu amesema hapingi kila kitu kinachofanywa na Magufuli bali anapingana na namna swala la madini linavyoshughulikiwa. Lissu amesema baadhi ya vitu anavyopinga ni namna swala hilo linavyofanywa kisiasa na katika msingi wa uongo hali ambayo amesema inatudhalilisha na kutufanya tuonekane kituko na kwamba huko nje wanatucheka.

Akifafanua zaidi Lissu amesema hoja ya uongo ni namna ambavyo kamati ya Rais ya Profesa Mruma na ile ya Orosso ilivyodanganya umma na dunia kwa ujumla. Lissu anasema kwake hizo ripoti ni professorial rubbish kwa sababu zimesema uongo. Lissu anasema Profesa Mruma alikuwa mjumbe wa kamati ya Jaji Bomani na yeye ndiye aliyepeleka takwimu za madini kwenye kamati kupitia taasisi anayoiongoza ya Geological Survey of Tanzania (GST) na takwimu alizozipeleka kwenye kamati ya Jaji Bomani na anazozitoa sasa ni tofauti. Tazameni taarifa zilizopo GST taasisi ambayo Profesa Mruma ndiye bosi halafu angalieni alichokuja nacho kwenye kamati ya Rais ni uwongo. Je ni nani anayedanganya kati ya kamati ya Rais ya Mruma au ile ya Bomani? Je ni nani anayedanganga kati ya GST na kamati ya Mruma?.
Tundu Lissu anasema huwezi kupambana na wazungu kwa hoja dhaifu tena za uongo na kwa matamko ya kisiasa na usikubali wazungu wakuambie kwamba unavunja sheria utaumia. Madini ya Tanzania yanajulikana na zaidi Bulyanhulu STAMICO wamefanya exploration toka 1977. Kama kamati ya Mruma ingekuwa ni kweli basi Bulyanhulu ingekuwa inaongoza duniani kwa dhahabu. Kwa hapa Tanzania Bulyanhulu siyo ya kwanza ni ya pili baada ya Geita na hizi ni taarifa za GST ambayo inaongozwa na Mruma.

Kwa upande mwingine Lissu amesema kwamba kuna watu hawamwelewi wanasema amehongwa jambo ambalo halishangai maana hajaeleweka miaka 18 hashangai kutokueleweka hata leo.
Kwa upande wake Rais Magufuli kabla ya yote anapaswa

1. Ajitoe kwenye mikataba ya kimataifa ya kulinda wawekezaji mfano MIGA.

2.Abadilishe sheria za ndani za madini.

3. Ndipo apitie mikataba pamoja na wawekezaji ili iendane na sheria mpya kwa manufaa ya watanzania.

Lissu anasema hakubaliani na utaratibu uliotumiwa na Magufuli kwani unaweza kuiingiza nchi kwenye matatizo akitolea mfano wa Zimbabwe na Venezuela. Wanasema nawatisha mimi natoa tahadhali tu " wanasema mbona hawajaenda mahakamani ...ole wenu wakienda". Lissu alisema kilichofanyika kuzuia mchanga hakijafuata utaratibu na kwamba hiyo inaweza kupelekea ACACIA wakaenda mahakamani kudai fidia na kwamba tutakuwa hatuna pa kuponea maana tumevunja mkataba na sheria zetu wenyewe.

Lissu anasema tuliwakabidhi Mali zetu kisheria lazima tuzirudishe kisheria.
Ujinga mwingine tiba yake siyo Elimu, inaweza kuwa tiba ya ujinga ni ujinga. Lisu ni mjinga hivyo hatushangai kumuuona anafanya ujinga na kuongea ujinga. Kama hapingi kwanini haungi mkono? Kwa sababu huwezi kuacha kupinga na wakati huohuo ukaacha kuunga mkono. Tundu Lisu ni Popo.
 
Eti huko nje wanatucheka!!!!Huyu Lissu mnafiki sana,huyu si ndio alisema Tutashitakiwa?Nchi itakuwa kama Zimbabwe?
Jamaa ni arrogant sana yaani kusema tafiti za tume ni professorial rubbish sio kauli nzuri kabisa
 
Lissu mruma kasema tunaibiwa na unakiri anayo maabara yake ya kupimia vikole pale GST, wewe hata munzani hauna hebu usitupotezee muda, sisi tuko driving school tayari kupokea noah
Ndio hapo sasa yaani lissu kimbele mbele sana kwa kuingilia taaluma za wengine.
 
MWANDISHI WA MAKALA ILIYOSABABISHA GAZETI LA MAWIO KUFUNGIWA
ADAI KUTISHIWA MAISHA NA WATU WASOJULIKANA
TAARIFA INA REPOTIWA KUTOKA DW NOW
 
Badala ya kuunga mkono mabadiliko yanayofanywa na jpm ndo kila sk tunafatilia yule kigeugeu wa singida anavyozidi kugeuza geuza mambo
 
Back
Top Bottom