Lissu: Hakikisheni mnaenda kumzika Odinga

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu amewaagiza viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Bara John Heche kuhakikisha wanashiriki kwenye ibada ya mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na aliyekuwa Kinara wa Upinzani nchini humo marehemu Raila Odinga aliyefariki jana, Oktoba 15.2025, akiwa nchini India

Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini ametoa agizo hilo wakati akisalimiana na Heche akiwa kwenye kizimba cha chumba namba moja (1) cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam baada ya jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru kuhairisha kesi hiyo kwa muda

Taarifa kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa tayari mwili wa Raila Odinga umewasili nchini humo, na atapumzishwa kwenye makazi yake ya milele Jumapili, Oktoba 19.2025
 
Bahati mbaya ushauri wa Raila hawakuufuata kuhusu kusimamisha uchaguzi
 
Nina sikitika kusema kuwa awatabahatika kuvuka mipaka ya Tanzania...😭😭😭
 
Back
Top Bottom