Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Wewe na Lisu mnaongelea vitu viwili tofauti hata kama mhusika wa vyote viwili ni mtu mmoja. Msome tena LISU.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Umuofia kwenu....
Jana nimepata habari za ndani juu ya hili sakata la kukamatwa kwa kontena zikisemekana ni mitumba. Kiufupi hapo zamani watu walidanganya sana nature ya mizigo iliyo ndani ya kontena tena ujanja wao wote walikuwa wakifanya kwa kivuli cha transit cargo. Ujue transit cargo hapo mwanzo zilikuwa hazilipi VAT na hata ukaguzi wake kwenye scanner ulikuwa hafifu kwani ilikuwa haina maslahi kimapato ingawa hii mizigo ilikuwa inabaki humuhumu. Ujio wa scanner mpya na msimamo wa JPM kuwa lazima kila mzigo upite scanner ndio umefumua madudu mengi. Kulingana na mtoa taarifa wangu anasema "kweli JPM amefanikiwa kuwapoteza wapiga dili wengi bandarini" kwani pale scanner kuna wanajeshi,TISS,TRA na watu wa bandari. Pia port manager ameweka informers kibao. So ili upige dili hawa wote mpaka uwaweke sawa.
Turudi kwenye mada
Inasenekana huyu Bwana ukwaju aliingiza hizi kontena tangu mwezi wa tisa mwaka jana. Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa ni kawaida ya bwana ukwaju kukwepa kodi kwa njia hiyo ya kusingizia mitumba na pia kufanya ni transit. Sasa Bwana ukwaju alimtumia dogo flani aende kwenye kampuni ya clearing( sitaitaja) ili mzigo utolewe mwaka huu February. Ujue agent yeye huwa anafanyia kazi taarifa anazoletewa. Sasa Bill of lading ilionuesha ni mitumba. Hii bill of lading inajazwa ulaya wakati agent hayupo so hapa udanganyifu umeanzia kwa shipping line. Ok agent akaendelea kufanya kazi yake mpaka akawa amepata release order. Lakini ikaja kugundulika mzigo unadaiwa zaidi ya $80,000 ikiwemo na storage charge(kumbuka mzigo wa tangu September mwaka jana) Bwana Ukwaju alikuwa ameshaanza kunegotiate apunguziwe gharama kwa kuwaandikia TRA bila ya agent kujua. Sasa TRA wakawasiliana na agent kumjulisha juu ya negotiations alizoanzisha bwana ukwaju. Hapa kengele ya hatari ikalia kwa agent. Kumbuka wakati hili kontena linashughurikiwa tayari bwana ukwaju alishaleta kazi nyingine of the same nature kupitia kwa dogo aliyemtuma mwanzo. Agent baada ya kuwa na mashaka akamwambia dogo anaomba akutane na mwenye mzigo ndipo bwana ukwaju akaenda kwa agent akamwambia yeye achape kazi tu kwani kila mtu ni wake mle bandarini. Agent kwa kutotaka kuharibika akawaandikia TRA kuwa anajitoa katika shughuri za kushughurikia huo mzigo na atafutwe agent mwingine. Ikumbukwe haya yote yametokea kabla ya kontena kukamatwa au kupita scanner.
Sasa bwana ukwaju sijui alitafuta agent mwingine au la? Lakini inasemekana mzigo haukupita scanner na tayari alikuwa ameshapanga timu yake ili kutoa mzigo. Nadhani kulikuwa na mazingira ya kuzungukana mzigo ukakamatiwa getini ukiwa katika hatua za mwisho za kutoka. Au ni mainformer ndio walitoa taarifa hilo mie sijui. Ndipo mzigo ukaamuliwa urudishwe scanner na ubainika kumbe sio mitumba bali ni range rover.
Bwana ukwaju alishafanikiwa kutoa gari zingine mfano ile inayoonekana ina namba za zanzibar ilishatolewa ikaenda zanzibar na kupewa namba wakati ile gari documents zilionyesha ni transit to zambia. Ile gari ilikamatiwa zanzibar na inavyoonekana alikuwa anawatumia agents tofauti tofauti. Ile picha inayooshesha gari yenye namba za Zanzibar ni kwenye kituo cha polisi bandari. Kwa hiyo hakuna uongo katika hilo. Sema sio sawa kusema JPM alikamata yale magari. Magari yalikamatwa either kwa kuzungukana kwenye pesa au kwa mamlaka husika kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kama haya magari yalikamatwa baada ya kuzungukana. Je, nini maana ya kuwa na taasisi nyingi za usalama pale bandari? Inamaana wameamua kujiunga for common interest? Gari ilifanikiwaje kufika geti la kutoka bila ya kupita scanner? This is a home work for JPM.
TUNDU LISSU
Rais wa TLS ameshaingia katika kumtetea Bwana ukwaju. Naomba hili lisichukuliwe kisiasa kwani anatekeleza majukumu yake ya kutetea hata muuaji. Kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa hata akiwa ni muuaji. Lissu amelalamika kwa nini Bwana ukwaju anashilikiwa na polisi kwa siku 23 bila ya kufikishwa mahakamani au kupata dhamana. Hili nalo ni la msingi ili haki za watuhumiwa zilindwe. Inasemekana Bwana ukwaju ana ukwasi wa kutisha. Inasemekana polisi wananufaika sana na ukaaji wake pale kituoni kwani ukikaa na waridi lazima unukie waridi.
Wasalaam
Ndimu mkata shombo
 
Issue hapa sio magari wala Ramadhani Ukwaju kushikiliwa na polisi, hapa ni kila mtu anatafuta kiki na 'front page' za magazeti.

Ni mahabusu wangapi walioko korokoroni kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani? Ningemwelewa na kumpongeza Lisu kama hiyo hoja angeitoa kwa kulenga wote wanaofikwa na hiyo dhuluma. Ila ukiangalia kwa picha kubwa kwenye hii issue, Lissu anakanyaga anakopita Magufuli. Hii haina maslahi mapana kwa taifa.
Raisi Magufuli ana matatizo yake, Lissu kwa umahiri wake hastahili kupita kwenye matatizo ya Magu ili kuonyesha ubora wake.
 
Acha kutufanya wajinga. Alisema ile issue alishaisikia na siku hiyo amejionea mwenyewe. Kilichompeleka ni ile michanga. Chuki imewaletea upofu.
Unayejifanya mjinga ni wewe unayejitoa ufahamu. Vyombo vya habari vyote viliripoti "Rais Magufuli akamata kotena ...." Hizo habari nimeripoti mimi?
 
Kila kitu Chato.Kuna yule ameshikwana magari ya kifahari baada ya kupora wamuliki/wafanyabiashara na kuwatisha hajaguswa kisa Msukuma.
Yupi huyo dada?
 
Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
Halafu bashite mbona hataki kuweka vyeti mezani weka vyeti wacha maneno
 
Mh. Tundu Lisu(Mb) na Rais wa Tanganyika Law Society, kwanini Sheria za Forodha hazikutumika pia ni vema Wananchi wajulishwe kukamatwa kwa Bw. Ramadhan Mussa Hamisi Ukwaju alishayatoa hayo magari au bado yalikuwa mkononi mwa TRA- Forodha kama yalikuwa bado mkononi mwa Forodha kulikuwa hakuna sababu ya Sheria ya Forodha,inayoruhusu Jeshi la Polisi kuhusika kumuweka au kumkamata wangehusika tu pale taratibu za Forodha kukamilika na kubainika amekiuka Sheria.
Ni kwa nini Rais anahusishwa wakati mali zilikuwa mkononi mwa Forodha?
Sheria ya Forodha na Kanuni zake inaelekeza vipi mwingizaji mzigo inapobainika hakueleza mzigo wake kwenye "Bill of Landing" na je kwenye Single Entry alidanganya?
Hapo taratibu za Sheria zingetumika na sio kumtoa Rais Ikulu , waliofanya hivyo wanampotisha Rais kwa maslahi yao na huyo Bw. Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju Sheria itamkinga kama atapelekwa Mahakamani na Mahakama ikawa huru katika kuteleza wajibu wake Kikatiba na Sheria.
 
Aisee... Nikupongeze kwa kuiona point.....

This was not expected itoke kwako....

By the way, Kama Ukwaju yupo ndani toka March 4, 2017... raisi alishitukiza nini kwenye kukamata yale magari?
Rais alichokifanya ni kuwatia moyo watendaji bandarini na kwa kweli aliwapongeza sana pale hadharani hususan baada ya kumueleza kwamba wameshika makontena kama hayo kule bandari ya Zanzibar, kwenye ICD's (bandari kavu) na hapo Dar.
Yaelekea watu ndio hawakumuelewa Rais.
 
Sasa raisi amekamata nini? Kumbe makontena yalikamatwa 3 weeks ago? hii nchi ishanishinda

[emoji23][emoji23][emoji23] ndugu unajitekenya na kucheka mwenyewe!! siku alipoenda bandarini alipelekwa kwenye makontena hayo haliyokuwa na magari! afisa wa bandari akawa anamuelezea jinsi walivyotumia scanner kubaini udanganyifu huo uliofanywa na waagizaji.

wakafungua, wakamuonesha hayo magari yaliyofunikwa na mitumba na magodoro.

sasa ndugu habari ya kusema magu ndo ameyakamata hayo makontena uliitoa wapi??
 
Halafu bashite mbona hataki kuweka vyeti mezani weka vyeti wacha maneno

ataweka vyeti tu, we nenda mahakamani! wakimtaka aweke ataweka!

we unamwambia aweke vyeti mezani kama nani?? amekuja kufanya interview kwako??
 
Hii ni aibu nyingine kwao, kumbe siku aliyoenda bandari ilikuwa ni usanii tu wa kutafuta kiki.
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Aidha hujaelewa au unapotosha makusudi!
Lisu halalamikii mtu kukamatwa! Analalamika mtu kushikiliwa na polisi kwa wiki tatu bila kufilishwa mahakamani na bila kupewa dhamana! Utaratibu huo ni kinyume cha sheria!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Viwanda viwanda viwanda

Kila siku drama viwanda tutaanza kujenga lini? Kumbukeni Tanzania ya Magufuli Ni Tanzania ya viwanda

Suala la viwanda lilikuwa kibwagizo tu, muhimu ilikuwa ni kuingia magogoni kulinda maslahi tu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani hiyo kitu imenikera! Angekuwa anashaurika basi, kama ana washikaji wangemwambia anajipaka kufanya drama za kitoto!
Ah! Viroba vyenyewe wamezuia; ningeagiza kimoja niamke nacho hapa!
Mi itabidi tu niagize bapa, hizi drama kama za class 4 aise, sio za kiutu uzima kabisa
 
Back
Top Bottom