Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
Ney Wa mitego alishayaona haya
Lissu azidi kumcharukia Magufuli, akerwa mtuhumiwa wa Range Rover zilizofichwa kwenye makontena ya mitumba kusota mahabusu siku 23
Mar 27, 2017 by Raia Mwema in Habari
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, amesikitishwa na hatua ya Jeshi la Polisi – kitengo cha Bandari kuendelea kumshikilia Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju, bila kumfikisha mahakamani ama kumwachia kwa dhamana.

Ramadhani ndiye anayehusishwa na tukio la kusafirisha magari matatu ya kifahari aina ya Range Rover katika makontena ambayo taarifa zake zilionyesha mzigo huo ni nguo za mitumba, tukio lililofichuliwa na Rais Dk. John Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar e s Salaam takriban wiki moja iliyopita.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na pia Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliweka bayana hayo leo, Machi 27, 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya Lissu ambayo ‘tovuti’ hii imeinasa, Ramadhani amekuwa mahabusu kwa wiki kadhaa sasa.

“Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu. Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita. Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile,” anaeleza Lissu

Anaendelea; “Suala lake limeshafika kwa DPP (Mwendesha Mashitaka) na kwa RPC Simon Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.”

Kwa mujibu wa Lissu, hayo ndiyo madhara ya rais kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Anasisitiza; “Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.”

Anasema japokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, lakini yeye si DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

“Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

“Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju. Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.”

“Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) na AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) pamoja na Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba. Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii,” anasema Lissu na kuongeza kuwa kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo hayo aliyoyaita mabaya.
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Hivi unadhani ukitenda kosa, haki zako zote zinafutwa?

Tatizo kubwa ni kwamba kuna watu wanataka kuficha makosa yao kwenye makosa ya wengine

Same story na ya madawa ya kulevya na vyeti...
 
Hapo ndipo tunaona Jamaa aliamua kucheza game ya kuigiza.

Sasa alishtukiza kitu gani wakati mtuhumiwa alikuwa ameshakamatwa tangu tarehe 4/3.

So alienda bandarini anajua kuwa anaenda kuangalia magari aina ya Range rover.

Sifa zingine hazina hata kiki. Ndio maana ilibuma kumbe watu walijua sio kushtukiza Bali amekuja kwa taarifa.
 
Labda uelewa wangu mdogo ila nijuacho raisi alienda bandarini baada ya kuambiwa kuna makontena ya mchanga wa madini baada ya kuyaona ndipo yule aliyekuwa anakaimu akampa taarifa kuhusu kukamata hayo ma range sio kwamba alienda kukamata yeye
 
Watu wengine hawawezi hata kujiongeza, Mbona kila kitu kilikuwa kinaelezeka, Rais alifahamishwa juu ya kontena na hakawapongeza, sasa hizi habari za kusema rais amegundua zimetoka wapi? au waandishi makanjanja na wale wapenda kukosoa?
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Yatakuwa ya bashite kwani ndio mwenye historia ya kupora Magari ya kifahari.
Kajiongeze kidogo hata kwenye English course juu ya hili ili uoate credit. Lissu anakuonyesha uvunjifu wa sheria unavyowacost RAIA nawe unaingiza ulevi wako wa itikadi za kipuuzi. Na bado lile LA mchanga mliloanza kulikoroga eti ni dhahabu wakati ni shaba. Show za kibabe hazidumu.
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Njaa mkuu huyu Rais wetu wa society kashachungulia mtonyo apo mbona tumtegemee kuwa na kesi kila mahakama badala ya kutengeneza hoja/muswada utakaowasaidia watanzania wote....ukwaju ni kama muhujumu uchumi fikiria tungepoteza kodi kiasi gani kama yangepita ayo magari huku ni Taifa linalochechemea kiuchumi ambalo linategemea kodi zake liendelee.
 
kina Ray wamchukue Mkulu waigize nae kwa kweli maana ana kipaji
 
HAHAHAHA CHADEMA NI MWENDO WA KUTETEA WAHUJUMU UCHUMI
 
Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
[emoji2] tamthilia wakamzibe nape kwa hoja ya makontena
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Kuna watu ni vichwa ngumu, wewe ni mmoja wao. Maidhui ya Tundu Lissu hayasemi kuwa hajaficha. Mtu kama kakamatwa na jambo lazima apelekwe mahakamani ili akafungwe au kuachiwa huru.
 
Labda uelewa wangu mdogo ila nijuacho raisi alienda bandarini baada ya kuambiwa kuna makontena ya mchanga wa madini baada ya kuyaona ndipo yule aliyekuwa anakaimu akampa taarifa kuhusu kukamata hayo ma range sio kwamba alienda kukamata yeye
Mushaanza kukwepa, siku ile ilitajwa kabisa kugundua makontena yaliyo na magari badala ya Nguo. Labda kama waandishi walipotosha.
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Sijui kama huwa unaunganisha akili yako na vidole vyako, kuna haki za msingi za mtu na usiangalie kipuuzi. hapo huyu ni mtuhumiwa tu. anyway hata nikikuleza haki za mtuhumiwa hutanielewa.
 
Back
Top Bottom