Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Lissu azidi kumcharukia Magufuli

Huyu Tundu simuelew huyo ukwaju amekaa siku 23? Jamn ni juzi tu hapo mkuu kenda bandarini...Tundu anasema amekamatwa toka tarehe 4 mmh so ni tarehe 4 mwez wa tatu, tarehe 4 mwez wa tatu kabla hata ya kutumbuliwa nape kabla hata mako hajaingia clouds kabla hata ya kuzinduliwa interchange jamni mbona sielew....
 
Yaani hata mi nashangaa! Tangu adaiwe kuyakamata hayo makontena wiki haijapita na inaonyesha Ukwaju tayari alishaokotwa zaidi ya wiki mbili nyuma. Aliokotwa kwa kosa gani? Kumbe hii ya mkulu ilikuwa ni drama tu? Kwa mwendo hu wanajidharaulisha, maana watafanya tujue kila tukio wanaigiza tu! Too low for our "king"!
Acha kutufanya wajinga. Alisema ile issue alishaisikia na siku hiyo amejionea mwenyewe. Kilichompeleka ni ile michanga. Chuki imewaletea upofu.
 
Lissu azidi kumcharukia Magufuli, akerwa mtuhumiwa wa Range Rover zilizofichwa kwenye makontena ya mitumba kusota mahabusu siku 23
Mar 27, 2017 by Raia Mwema in Habari
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, amesikitishwa na hatua ya Jeshi la Polisi – kitengo cha Bandari kuendelea kumshikilia Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju, bila kumfikisha mahakamani ama kumwachia kwa dhamana.

Ramadhani ndiye anayehusishwa na tukio la kusafirisha magari matatu ya kifahari aina ya Range Rover katika makontena ambayo taarifa zake zilionyesha mzigo huo ni nguo za mitumba, tukio lililofichuliwa na Rais Dk. John Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar e s Salaam takriban wiki moja iliyopita.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na pia Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliweka bayana hayo leo, Machi 27, 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya Lissu ambayo ‘tovuti’ hii imeinasa, Ramadhani amekuwa mahabusu kwa wiki kadhaa sasa.

“Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu. Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita. Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile,” anaeleza Lissu

Anaendelea; “Suala lake limeshafika kwa DPP (Mwendesha Mashitaka) na kwa RPC Simon Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.”

Kwa mujibu wa Lissu, hayo ndiyo madhara ya rais kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Anasisitiza; “Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.”

Anasema japokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, lakini yeye si DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

“Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

“Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju. Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.”


“Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) na AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) pamoja na Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba. Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii,” anasema Lissu na kuongeza kuwa kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo hayo aliyoyaita mabaya.

Hii habari ina mapungufu ya mtiririko wa tarehe kwani tokea Raisi afike bandarini hazijaisha siku 23; ndio kusema kabla ya Raisi kufika bandarini tatizo la hizo gari lilishagundulika na hatua zilishaanza kuchukuliwa
 
Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
Siku ile tulipo oneshwa hi show ndio siku hiyo hiyo Nape alikua katumbuliwa na kutishiwa bastola pia; the following day akina mwanafyale walikua wanakula kiapo, zile hasira za mkulu za kwamba kwanini magazeti yote yaliandika habari za Nape tu na sio issues za Bandarini zilinifanya nifikirie kwamba may be there was something hidden; nimepata jibu sasa, well said Tundu.
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Soma vizuri uelewe kilicho andikwa; usisome huku umeishikilia naniliu yako. Weka akili yako kwenye maandishi, usiweke akili zako kwenye chuki ukasahau kilicho andikwa. Mstari kwa mstari ukisoma uzi haufanani na unacho kisema wewe.
 
Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
Ile ilikuwa mbinu ya kuzima hekaheka za Nape zisitoke kwenye front pages za magazeti.
 
Lo mtu anakaa mahabusu wiki tatu bila kupelekwa Mahakamani?. Hii mpya. Tunatakiwa tujitathmini.
 
Kingine jamaa kama kashahukumiwa tayari,,,maana gari zake bwana mkubwa kahamuru zitaifishwe pia,,,na kishazigawa kwa sekta tatu,,,,,iyo kesi mwisho wake utakuwa mzuri kwa upande mmoja,,,,
 
Hii habari ina mapungufu ya mtiririko wa tarehe kwani tokea Raisi afike bandarini hazijaisha siku 23; ndio kusema kabla ya Raisi kufika bandarini tatizo la hizo gari lilishagundulika na hatua zilishaanza kuchukuliwa


Ndo maana yake mkuu
 
Watu wengine hawawezi hata kujiongeza, Mbona kila kitu kilikuwa kinaelezeka, Rais alifahamishwa juu ya kontena na hakawapongeza, sasa hizi habari za kusema rais amegundua zimetoka wapi? au waandishi makanjanja na wale wapenda kukosoa?
Ukumbuke kuwa hii ishu ilisusiwa na waandishi wa habari ila magazeti yenu pendwa ndio yakaandika na kuipa kiki hiyo habari
 
Ukwaju alificha rangerover 3 kwenye mitumba? Tundu Lissu anataka tumuunge mkono? Na sisi wenye kuvaa mitumba atatuunga mkono nani? Ukwaju ni mwana CHADEMA au magari ni ya CHADEMA?
Lissu hamuungi mkono Ukwaju ila anasikitishwa na haki za ukwaju kufinyangwa. Unajua hii nchi tumeamua kuweka sheria zituongoze. Na hiyo sheria inasema mtu anapokamatwa na polisi afikishwe mahakamani ndani ya masaa 24 kama ni weekdays. Haisemi kama umefanya kosa lolote uwekwe ndani wiki au mwezi. Kwahiyo hii ni haki ya msingi ya mtuhumiwa. Kuna wakati tunaweka vyama na itikadi mbele hasa yanapowakuta wengine ila siku yakikukuta na ukose mtetezi utaomba hata namba za lissu umpigie. Kumbuka huyu ukwaju ana familia na watoto wanamtegemea sasa hata kama kafanya kosa la jinai hatua stahiki zichukuliwe ila haki yake pia apatiwe.
 
hongera sasa tunategemea na kesi za maskin mjitokeze isije kuwa mnajitokeza kesi za matajiri kwa kuwa mnajua kuna return........
 
Viwanda viwanda viwanda

Kila siku drama viwanda tutaanza kujenga lini? Kumbukeni Tanzania ya Magufuli Ni Tanzania ya viwanda
Mpaka sasa kuna viwanda elfu 5 vimejengwa na vingine vinaendelea kujengwa sehemu mbali mbali

Industrial Revolution
 
Huyu jamaa kama alikua ndani muda mrefu hivyo, haya makontena juzijuzi kumbe ilikua ni show tu? Maana walikua washamkamata tayari, wameona aitoshi wakaona wakauze headlines kidogo kwenda kuyafungua watuonyeshe.

Haya yote ni kutusahaulisha Bashite, sasa tunalianzisha tena
Inamaana hukustukia? hebu fikiria Kontena linavunjwa kufuli mbele ya Rais utadhani halijawahi kufunguliwa hata siku moja. Hizi sanaa tutashuhudia sana maana JPM siyo mzuri katika Siasa za majukwaa yeye atakijikita na style ya kutumbua mpaka apewe miaka mingine mitano na Tume ya Taifa ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom