Lissu awasili Nairobi salama lakini Ubalozi wa Tanzania haujatoa ushirikiano

Acheni kulalamika.Kwani mlienda kuutegemea ubalozi.Fanyeni linalowezekana Lissu apone hayo mambo ya ubalozi siyo priority kwa sasa.
Kabisa maana hataivyo msaada wao hauhitajiki kabisa..... Priority matibabu.
 
Acheni kulalamika.Kwani mlienda kuutegemea ubalozi.Fanyeni linalowezekana Lissu apone hayo mambo ya ubalozi siyo priority kwa sasa.
Mkuu, hapo sikubaliani nawe. Pamoja na kuwa na itikadi tofauti za kisiasa. BADO Tundu Lissu ni Mtanzania mwenzetu.

Ndo maana hata WABUNGE wa vyama vyote ikiwemo CCM wameamua NUSU ya MSHAHARA wao UTAENDA KUGHARIMIA matibabu yake huko Nairobi.
Tutofautiane kisiasa. Lakini TUJALIANE wakati wa DHIKI!
 
Walitaka balozi afanye nini? Bora alivyokosa kosa kwenda maana ingesemakana vingine kabisa. Cdm uwa siwaelewi kabisa unamsema vibaya mtu uyo uyo then unataka msaada kwake. Tumuombe Tundu Lissu apone haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaburi112:6 kwa maana hataondoshwa kamwe mwenye haki atakumbukwa milele.
 
Sasa kama kumlipia matibabu wamegoma sembuse ubalozi hawatakanyaga hapo kikubwa tuna muomba MUNGU apone haraka
 
Nijuavyo mtanzania yeyote anapokwenda nje yeye ndiye anatakiwa Ku report ubalozini .. Hao viongozi Wã cdm waliomsindikiza inabidi ndio wakatoe taarifa ubalozi .. Ukifika pale kuna kitabu wataweka maelezo kitabu hakimfati mtu
Wanataka wao ndio wafuatwe mkuu. Ila utaratibu wanajua ila hili tukio lipo kisiasa zaidi na kuchafuana kuliko kumsaidia mgonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hakuna jambo kama hilo, balozi kashindwa kufika hospital?
Kufika kwake kusingesaidia maana alipelekwa chumba cha upasuaji punde alipofika.
Lakini UKUMBUKE pia kuwa leo WABUNGE WAMEKUBALIANA kuwa NUSU ya Mshahara wao UENDE katika kugharimia MATIBABU ya Tundu Lissu.

Nafikiri hiyo ni ISHARA njema ya KUTUUNGANISHA.
UTOFAUTI wa KIITIKADI za kisiasa kusitufanye TUKOSE huruma wakati wa DHIKI.
 
Chakushangaza hadi sasa tangu tuwasili hatujapata ushirikiano wowote wa ubalozi wa Tanzania hapa Nairobi, Si kwa balozi au maafisa wowote wale wa ubalozi.
Kwani mlitoa taarifa ubalozini kwamba mnaenda na mgonjwa?
Huko Dar mmekimbia nini halafu unataka watu wa ubalozini waje,je mgonjwa akidhurika zaidi utasema maafisa walitumwa kummaliza
 
Sasa kama kumlipia matibabu wamegoma sembuse ubalozi hawatakanyaga hapo kikubwa tuna muomba MUNGU apone haraka
Kwa kukusaidia tu. WABUNGE wa pande zote za kisiasa CHADEMA na CCM leo wameamua KUKATWA NUSU ya MSHAHARA wao ili kugharimiwa matibabu yake. Kwa hivyo HOJA yako haina msingi.
 
Kwani mlitoa taarifa ubalozini kwamba mnaenda na mgonjwa?
Huko Dar mmekimbia nini halafu unataka watu wa ubalozini waje,je mgonjwa akidhurika zaidi utasema maafisa walitumwa kummaliza
Mkuu hiyo si kauli njema. Tundu Lissu japokuwa yu chama kingine. BADO yeye ni MTANZANIA.
Hata kama wakati mwingine tunatofautiana naye katika itikadi za kisiasa. Kama Watanzania ni lazima TUMTAKIE KHERI ya AFYA na apone haraka.

Ndo maana WABUNGE wa CCM na UPINZANI LEO wameungana PAMOJA ili NUSU ya MISHAHARA yao IKATWE ili KUGHARIMIA matibabu ya Tundu Lissu.
Maana ni Mtanzania mwenzetu.
 
Habari, Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa Saba hapa Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale airport na matibabu yalianza Mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital. Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa theatre.

Tangu Jana alipofika alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio. Hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri. Nitawajuza atakapo toka theatre.

Chakushangaza hadi sasa tangu tuwasili hatujapata ushirikiano Wwa ubalozi wa Tanzania hapa Nairobi, Si kwa balozi au maafisa wowote wale wa ubalozi. Mh Freeman Mbowe amezungumza na vyombo mbali mbali vya habari pia taarifa yake itatoka punde.

Hemed Ali
Mkuu wa Idara ya Uenezi CHADEMA.
Nairobi hospital.
Wwe balozi hajipendi au hapendi kazi yake. Yule kiongozi mwenye kisasi cha mbwa atawamaliza. Kitumbua kaka
 
Kufika kwake kusingesaidia maana alipelekwa chumba cha upasuaji punde alipofika.
Lakini UKUMBUKE pia kuwa leo WABUNGE WAMEKUBALIANA kuwa NUSU ya Mshahara wao UENDE katika kugharimia MATIBABU ya Tundu Lissu.

Nafikiri hiyo ni ISHARA njema ya KUTUUNGANISHA.
UTOFAUTI wa KIITIKADI za kisiasa kusitufanye TUKOSE huruma wakati wa DHIKI.

Waliofika jana hospital walimuona? Hilo ni bunge ni makubaliano yao kama mwenzao. Lakini balozi angeonya kuguswa akafika tu.
 
Mkuu hiyo si kauli njema. Tundu Lissu japokuwa yu chama kingine. BADO yeye ni MTANZANIA.
Hata kama wakati mwingine tunatofautiana naye katika itikadi za kisiasa. Kama Watanzania ni lazima TUMTAKIE KHERI ya AFYA na apone haraka.

Ndo maana WABUNGE wa CCM na UPINZANI LEO wameungana PAMOJA ili NUSU ya MISHAHARA yao IKATWE ili KUGHARIMIA matibabu ya Tundu Lissu.
Maana ni Mtanzania mwenzetu.
Sio nusu ya mshahara mkuu ni nusu ya posho ya siku
 
Mkuu hiyo si kauli njema. Tundu Lissu japokuwa yu chama kingine. BADO yeye ni MTANZANIA.
Hata kama wakati mwingine tunatofautiana naye katika itikadi za kisiasa. Kama Watanzania ni lazima TUMTAKIE KHERI ya AFYA na apone haraka.

Ndo maana WABUNGE wa CCM na UPINZANI LEO wameungana PAMOJA ili NUSU ya MISHAHARA yao IKATWE ili KUGHARIMIA matibabu ya Tundu Lissu.
Maana ni Mtanzania mwenzetu.
hata mie makamanda wamepita ofisini nimechanga buku 5 kwenye mfuko wa chadema,ninachopinga ni kupotosha na kuweka chumvi,cha muhimu ni kumuombea Lissu apone haraka badala ya kunyoosheana vidole
 
Back
Top Bottom