Uchaguzi 2020 Lissu atolea ufafanuzi kuitwa kwenye tume ya Maadili

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,504
51,099
Akiwa huko Serengeti, Mheshimiwa Lissu ametolea ufafanuzi mzuri, wa kitaalamu na kisheria juu ya utaratibu wa kuitwa kwake kwenye tume kwa ajili ya maadili ya uchaguzi

Lissu anasema kuwa kwa mujibu wa kanuni za maadili zilizotungwa na tume yenyewe, utaratibu wa shauri la maadili uko hivi

1. Lazima upande unaolalamika, kama ni mgombea mwenyewe, au tume n. k viandae shauri husika kwa maandishi

2. Mgombea mwenye kulalamikiwa mara tu apatapo shauri husika atatakiwa kulijibu shauri hilo kwa ndani ya masaa 48 baada ya kupata taarifa hiyo.

Lissu akasema, hadi sasa hajapata taarifa rasmi ya malalamiko hayo ya tume, na hata kama akiyapata leo ana muda wa siku mbili wa kuyajibu, kwa hiyo suala la kufika kwenye tume kesho tarehe 29 siyo lazima kwa mujibu wa kanuni.

Lissu akasema hilo shauri lazima limfikie yeye mwenyewe, siyo kulipeleka kwenye chama wala nyumbani kwake, na inabidi akabidhiwe yeye mwenyewe mkononi.

Kwa taarifa zaidi, tazama video hii ya Lissu
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi huyu Mkurugenzi wa NEC anasoma Kanuni kweli???

Uchaguzi ni mchakato ambao kila hatua imeainishwa kwenye sheria, Kanuni, taratibu na miongozo.

Yaani hakuna jambo lolote linalohusiana na uchaguzi ambalo halijatajwa na sheria.

Kwa hiyo, inashangaza inakuwaje NEC inatenda baadhi ya mambo kinyume na sheria, au pengine wanafanya nakusudi au hawana hela na au hizo sheria hawana kopi zake
 
Kwani mkurugenzi wa NEC kwa mujibu wa katiba anapaswa kuwa na sifa gani? Nauliza tu,I know magu ana phD ya kuokota watu majalalani
 
Dr Mahela ni mbobezi wa masuala ya Hesabu, sasa hesabu na sheria wapi na wapi.

Labda atatumia hesabu zake kuiba kura ambazo zitamtokea puani
 
Ni aibu kwa mwanasheria nguri anayetaka kuwa kiongozi mkuu wa nchi kutumia jukwaa la kisiasa kwa matatizo yake mwenyewe.

Nimemsikia Lissu akiwasomea wananchi, kwenye kampeni yake ya Urais wa JMT, vifungu kutoka kwenye kitabu cha MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2020 (Chini ya Kifungu cha 124.A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343) kuhusu kuitwa kwake na Tume. Yeye mwenyewe, kwa mdomo wake, ameituhumu Tume na anatakiwa aende kutoa ushahidi. Je, wananchi ndio mashahidi wake au baraza la wazee wa mahakama?

Lissu asiweweseke kutaka kufanya kosa lake liwe la kiasa. Je, akifanikiwa kuwa Rais ataacha watu wafanye wanavyotaka?

Kwa jinsi alivyojipambanua ya kuwa ni jasiri wa dharau, ni dharau hiyo hiyo atawashushia walio chini yake.

Hakika atapata kura za wanachama wa CHADEMA wasiojitambua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…