Lissu asimama kizimbani kwa masaa 3:30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lissu asimama kizimbani kwa masaa 3:30

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 11, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Lissu apangua hoja za CCM kwa masaa 3 na nusu (3:30) : kauli ya mwisho anayosema ni kuwa katika tuhuma zote zilizoletwa mahakamani, hakuna ushahidi hata mmoja wa mawakala wa CCM, au wapiga kura wa CCM waliolalamika kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.

  Hakuna hata wakala mmoja wa CCM aliyejaza fomu namba 14 ya kutoridhika na upigaji kura. Sheria za uchaguzi zinasema wakala ajaze fomu kuonyesha kuwa ameridhika au hajaridhika na kulalamikia tuhuma iliyoletwa mahakamani.


  Jambo la pili Hakuna wakala hata moja aliyejaza fomu namba 16 ambaye hakuridhika na zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo

  Tatu: Hakuna ushahidi wowote wa nyaraka, kuonyesha kuwa CCM au mgombea wao wa Ubunge, au diwani, au wakala wao aliyelalamika kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi ya Jimbo la Singida mashariki, au kwa jambo lolote lile.

  Na hakuna ushahidi wowote uliotolewa wa malalamiko yeyote. Ushahidi uliotolewa wa Bw. Robert Kimanda, anadai kuwa aliwahi kusema kuwa alijaza. Lakini shahidi aliyefuata alisema kuwa baada yakugundua kuwa CCM wameshinda katika kituo alichosimamia, aliichana fomu hiyo. Kuna malalamiko mengi lakini mengi yanatokana na umbumbumbu wa kutojua sheria za uchaguzi.

  Kutokuwepo kwa malalamiko kunaonyesha kuwa hakukuwepo tatizo, kesi imetengenezwa baadaye na watu walioshindwa kwenye uchaguzi. Mheshimiwa jaji, Mashahidi walipingana, wengine walisema walioleta mashataka ni waongo.

  Kama mashahidi wa upande wa walalamikaji wanaitana waongo mheshimiwa jaji, kuna nini chakuongeza? Shahidi namba 16, alisema waleta maombi ni waongo.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  inshaallah lissu atashinda!kesi za kupikwa na makamba ex ccm secretary
   
 3. k

  kubenafrank Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwanini ccm wanafikiria kuwavua wabunge wote makini wa cdm ubunge?Huu ni ushahidi kuwa wanaiogopa sana nguvu ya umma.Kulazimisha kuwa Lisu ana kesi ya kujibu ni ulimbukeni na uzuzu wa ccm.Ni wakati mahakama zetu zitende haki kwa maslahi ya wananchi
   
 4. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa taarifa iliyojitosheleza
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Isango!!

  Usiwe kimya Kamanda wetu,,,,,,,,,,,,,,,,,tupe Updates ya hapo mahakamani


  Ni nini kinaendelea mpaka majira haya Kamanda?????????????????
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Atasalimika kweli
   
 7. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mdogo wangu lissu, wewe umeshamaliza sehemu yako! Kwa sasa mwachie mungu akuteteee,biblia inasema haki huinua taifa,bali dhambi ni aibu ya watu wowote(mith;14:34) haijalishi ni jaji,rais,hakimu au waziri mkuu.
   
 8. M

  Malolella JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lissu hawamuwezi. Hana rekodi ya kushindwa kesi dhidi yake au anayoisimamia.
   
 9. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Big up Lissu nakukubali sana Kamanda jinsi unavyojipanga na kutoa mashambulizi yenye kugonya bongo na n.y.e.ti za magambaz.
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hii kesi ni upuuzi mtupu!
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mtakuja kushindwa kushangaa Lissu anashindwa kesi hii.
   
 12. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa angu mmoja alishawahi nambia, huwa akimuona Lissu anazungumza huchukua kalamu na karatasi kuandika nondo zake huwenda zitamsaidia maishani mbeleni.
   
 13. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  siku zote nguvu ya uma itashinda
   
 14. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Isango..... ikipata muda tupe kwa kirefu mzee tujuze camanda Lisu alivyopangua hoja za magamba
   
 15. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  wanajua hawatashnda ila wameamua kumpotezea muda wake ili asi report mjengoni kpndi hki.
   
 16. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lissu pambana utashinda tu.
   
 17. s

  smgsmg Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na imani ndugu lisu atashinda kesi siku zote kweli huwa inashinda.God b with u
   
 18. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Najisikia kufa kufa ninaposikia hii kesi isiyo na kichwa wala miguu. Iko siku tutaingia msituni wenyewe bila kuambiwa na mtu. Magamba subirini siku yenu inakuja
   
 19. a

  ambwene_ambwene Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na pia Neno la Mungu linasema "Wamngojao Bwana Mungu hawataabika wataaibika watendao uhaini bila sababu Za. 25
   
 20. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  CCM jiangalieni sana, kila Mtanzania anawalaani hakika hamtadumu, na ninyi mliosoma kwa kodi zetu na sasa kulipwa kwa pesa za wavuja jasho, mwisho wenu utakuwa mbaya kwa kutumiwa na CCM kupindisha haki huku mkijua wazi hamkutenda haki. Majaji na polisi ole wenu kwa kwa kujifanya ninyi wajinga katika hili.
   
Loading...