MADIKTETA NA UZALENDO BANDIA
Mara nyingi madikteta hujinasibu kuwa na mapenzi makubwa kwa mataifa wanayoyaongoza. Hata hivyo, ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mapenzi wanayokuwa nayo huwa ni yamejaa ubinafsi kwa kupenda kuridhisha nafsi zao pasipo kujali umuhimu wa watu wengine. Wao ndio hujigeuza kuwa taifa na kwao usalama wao ndio huwa usalama wa taifa na si usalama wa raia. Kwao uzalendo ni wananchi konyesha mapendo kwao, kuwashangilia na kuwatii. Wanaamini katika uwezo wao wa kutenda na si katika uwezo wa wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa taifa hujengwa na wananchi na hivyo mzalendo wa kweli hutanguliza mapenzi ya wananchi kuliko nafsi yake, huwaamini wananchi kuwa ndio wanajenga nchi, huamini kuwa taifa ni la wananchi na si la mtawala au kundi la watawala. Mzalendo wa kweli hufanya jitihada kuleta furaha kwa wengine kuliko kufurahisha nafsi yake. Madikteta ni mafisadi wa kimaadili (they are morally corrupt) na hawana sifa ya kuitwa wazalendo kwa kuwa uchu wao wa madaraka huleta mateso kwa wengine.
Udikteta ni dhana pana sana na pengine haina tafsiri ya moja kwa moja, nadhani maana halisi ya udikteta ni hisia.
Tukisema udikteta kwa maana ya sheria je sheria hiyo imejitosheleza kujumuisha matakwa ya kila mtu na hisia za kila mtu?
Je, sheria yenyewe haiwezi kuwa athari kwa hisia za wengine?
Lakini kama sheria ndio kipimo, je mapinduzi ya kiutawala yanawekwa upande gani? Mfano yaani mmehamua kuandamana, pasina kufuta sheria kupinga utawala dhalimu labda, je nyie mtakuwa madikteta?
Jambo la pili udikteta unanzia wapi na kuishia wapi? Ni yapi matendo ya udikteta na matendo yasiyo ya udikteta, Je ipo orodha ya mambo hayo?
Nafikiri ipo haja ya kufikiria zaidi juu ya dhana hii, "udikteta"
Ubarikiwe sana.Yote ni sahihi,
Kwa kifupi sana ni kwamba,"DIKTETA NI MTU YEYOTE ANAYETAWALA WATU KWA NGUVU BILA KUFUATA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI"
Mara nyingi mtawala huyu,siyo Kiongozi huingia au huwekwa madarakani kwa lazima iwe kwa Mapinduzi ya Kijeshi au Uchaguzi usio Huru na Haki!
Kwa sasa Tanzania ndiyo tuko hapo! Najua kuna maCCM watakataa ukweli huu lakini ndivo ilivo!
Kwa watu waliofuatilia Uchaguzi Mkuu 2015 watakubaliana na hili!
JPM hakushinda Uchaguzi Mkuu baali aliingizwa kwa nguvu za Dola( Kuchakachua kura,wizi na kuwakamata/kuvamia vituo vya Wapinzani na kuondoka na Komputa za Majumuisho ili kuvuruga hesabu au idadi halali ya kura za UKAWA!
Baada ya kuingia Ikulu JPM akijua kuwa hakushinda kura ameamua kutumia mabavu ili kuwatisha na kuwanyamazisha hao waliomshinda kwenye sanduku la Kura!
Huku akijua kuwa Katiba inawapa mwanya Wapinzani ya kujijenga na kuendelea kumkosoa na hivo kuendelea kuweka Urais wake rehani ameamua kutumia madaraka vibaya kwa KUPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA KISIASA KWA UPINZANI TU huku akijua kabisa hiyo ni kinyume cha Katiba ya Tanzania!
Udikteta ni dhana pana sana na pengine haina tafsiri ya moja kwa moja, nadhani maana halisi ya udikteta ni hisia.
Tukisema udikteta kwa maana ya sheria je sheria hiyo imejitosheleza kujumuisha matakwa ya kila mtu na hisia za kila mtu?
Je, sheria yenyewe haiwezi kuwa athari kwa hisia za wengine?
Lakini kama sheria ndio kipimo, je mapinduzi ya kiutawala yanawekwa upande gani? Mfano yaani mmehamua kuandamana, pasina kufuta sheria kupinga utawala dhalimu labda, je nyie mtakuwa madikteta?
Jambo la pili udikteta unanzia wapi na kuishia wapi? Ni yapi matendo ya udikteta na matendo yasiyo ya udikteta, Je ipo orodha ya mambo hayo?
Nafikiri ipo haja ya kufikiria zaidi juu ya dhana hii, "udikteta"
Unaota nini? Upole wake uko wapi? Waulize wakazi wa Biharamulo na Chato ndo wanamjua tangu kuzaliwa kwake!Rais wetu ni mpole sana. Ana mambo mengi ya kushughulikia zaidi ya kupambana na Lissu. Polisi wapo watamshughulikia
Baelezee!Eti udikteta ni hisia, hauna tafasiri ya moja kwa moja!. Hujui kama hii ni topic inafundishwa darasani tena elementary levels? kwa hiyo kinachofundishwa sio facts ni hisia? Umenipotezea muda wangu hata kusoma ulichoandika. Hata kama vyeti vya darasa la saba hawakagui kwako iwe special case ukaguliwe tu.
Bravo! Addition!MADIKTETA NA UZALENDO BANDIA
Mara nyingi madikteta hujinasibu kuwa na mapenzi makubwa kwa mataifa wanayoyaongoza. Hata hivyo, ukichunguza kwa undani utagundua kuwa mapenzi wanayokuwa nayo huwa ni yamejaa ubinafsi kwa kupenda kuridhisha nafsi zao pasipo kujali umuhimu wa watu wengine. Wao ndio hujigeuza kuwa taifa na kwao usalama wao ndio huwa usalama wa taifa na si usalama wa raia. Kwao uzalendo ni wananchi konyesha mapendo kwao, kuwashangilia na kuwatii. Wanaamini katika uwezo wao wa kutenda na si katika uwezo wa wananchi. Wanashindwa kuelewa kuwa taifa hujengwa na wananchi na hivyo mzalendo wa kweli hutanguliza mapenzi ya wananchi kuliko nafsi yake, huwaamini wananchi kuwa ndio wanajenga nchi, huamini kuwa taifa ni la wananchi na si la mtawala au kundi la watawala. Mzalendo wa kweli hufanya jitihada kuleta furaha kwa wengine kuliko kufurahisha nafsi yake. Madikteta ni mafisadi wa kimaadili (they are morally corrupt) na hawana sifa ya kuitwa wazalendo kwa kuwa uchu wao wa madaraka huleta mateso kwa wengine.
Hongera Ruta kwa hoja yako hiyoNonsense, woga wa kike!
Kwa nini Lissu, mwanasheria, asiende mahakamani kudai demokrasia. Maandamano ndiyo yatatoa haki hiyo au kupigwa virungu waandamanaji wakati yeye akisepa!Kwan ukikaa nyumbani haufi nyie ndio walewale ambao hamjitambui kama unaona jambo halikuhusu piga kimya uctangaze propaganda za uongo