kabamanya
Senior Member
- Jun 20, 2013
- 163
- 44
Udikteta ni dhana pana sana na pengine haina tafsiri ya moja kwa moja, nadhani maana halisi ya udikteta ni hisia.
Tukisema udikteta kwa maana ya sheria je sheria hiyo imejitosheleza kujumuisha matakwa ya kila mtu na hisia za kila mtu?
Je, sheria yenyewe haiwezi kuwa athari kwa hisia za wengine?
Lakini kama sheria ndio kipimo, je mapinduzi ya kiutawala yanawekwa upande gani? Mfano yaani mmehamua kuandamana, pasina kufuta sheria kupinga utawala dhalimu labda, je nyie mtakuwa madikteta?
Jambo la pili udikteta unanzia wapi na kuishia wapi? Ni yapi matendo ya udikteta na matendo yasiyo ya udikteta, Je ipo orodha ya mambo hayo?
Nafikiri ipo haja ya kufikiria zaidi juu ya dhana hii, "udikteta"