KATIBA YA CHADEMA
UANACHAMA:
5.1 Sifa za kuwa MwanaChama
5.1.1 Awe raia wa Tanzania.
5.1.2 Awe na umri wa miaka 18 au zaidi
5.1.3 Awe na akili timamu
5.1.4 Awe anakubaliana na katiba, sera, kanuni na maadili ya Chama.
5.1.5 Awe anakubaliana na Itikadi na falsafa ya Chama.
5.1.6 Asiwe mwanaChama wa Chama kingine cha siasa baada ya kujiunga na CHADEMA.
Kupinga posho lilikuwa ni wazo la Zitto au ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?
Na kama imeandikwa sehemu kwamba kupinga posho ni Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA ni kwa nini Lissu asifukuzwe uanachama: Hivi tunavyoongea hapa Lissu anakula posho ya Wabunge, kwa sababu hakuna mtu hata mmoja aliyerudisha posho, uongozi wa Bunge na Serikali walikataa ku entertain kukataa posho, kupokea back posho ya mtu. Kwa hiyo Lissu anakula posho, afukuzwe CHADEMA kwa kukiuka Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?