Elections 2010 Lissu Aleta Tabu

Hivi Mwafrika umewahi kujiuliza hivi vibweka vyako vyenye elements za kebehi kwa imani za watu wengi humu zinasaidia ama kuathiri vipi maslahi ya chama ama mgombea wako/unayejinasabisha nae hasa wakati kama huu. Being sensitive to other people feelings and faiths is one of the most important political tool that you and some friends of yours need to learn and embrace...

omarilyas

Omar,

Hivi umewahi kujiuliza kuwa kwa nini ninakebehi tu baadhi ya watu na sio kila mtu?

Kuna waislam wangapi hapa JF? je ni wangapi ambao nimewakebehi? Umewahi kusoma majibu yangu dhidi ya watu kama Mkandara, Zitto, Mtu wa Pwani na wengineo?

Kama bado, sijawahi kutumia lugha ya kebehi kwao hata siku moja. Mimi ninajibu wale wanaoleta udini hapa kwa kebehi. Issue ya udini sikuianzisha mimi hapa. Mimi najibu moto kwa moto.

Kampeni za kistaarabu nimewaachia wengine. Umeona CCM wanavyomchafua Dr Slaa, ustaarabu wake haukusaidia chochote. CCM inabidi unawajibu kulingana na wanachokuletea. Wakikuita mdini na wewe wamwagie udini wao, wakileta mambo ya vimada, na wewe wapatie vimada vyao. Hii ndio motto yangu
 
Lisu akoroga msafara wa Slaa
Monday, 06 September 2010 20:13

Salim Said, Singida

MGOMBEA wa kiti cha ubunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, amevuruga msafara wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa, baada ya kumuamuru dereva wa gari lililokuwa limembeba mgombea urais, kuingia ghafla katika kituo cha mafuta cha Singida mjini jambo ambalo ni hatari.

Tukio hilo la aina yake na ambalo liliwashangaza na kuaacha midomo wazi watu waliokuwa katika msafara huo, lilitokea saa 7:25 mchana wa juzi, wakati msafara wa Dk Slaa ukiwa njiani kuelekea katika Kata ya Iglansoni, ukitokea Kata ya Sepuka katika Wilaya mpya ya Ikungi, mkoani humo.

Msafara huo ulikuwa na magari matano yaliyoongozana, mbele yakiongozwa na gari la polisi.

Tukio hilo lilikuja baada Lissu kugundua kuwa gari la Dk Slaa, lilikuwa na upungufu wa mafuta na hivyo akaamua lipelekewe kwenye kituo cha mafuta, lakini bila kutoa taarifa kwa polisi na viongozi wengine.

Baadhi watu, waliielezea kitendo hicho kuwa ni hatari na kwamba kilikuwa ni cha kuwadharau polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kitendo hicho, kingeweza kusababisha ajali katika msafara huo.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Sabula, alikemea kitendo hicho na kutaka kusirudiwe tena kwa kuwa kinahatarisha maisha ya mgombea na watu wengine katika msafara.

"Sasa umefanya nini Lissu, huwezi kuitoa gari ya mgombea katikati ya mwendo na kuiingiza sheli, wakati mbele tunaongozwa na polisi, ni hatari, kisijirudie tena kitu hicho," alisema Sabula kwa hasira.

Baada ya kuingia katika kituo hicho cha mafuta, Lissu alishuka katika gari la mgombea na kwenda kwenye gari lake na kulipia mafuta.

Baadaye, alipanda gari lake badala ya lile la mgombea kama ilivyokuwa kabla ya tukio hilo.

Wakati hayo yakifanyika gari la polisi lililokuwa na askari sita wakiwemo wawili wenye silaha, lilikwenda kuegesha umbali wa mita 300, ili kusubiri msafara huo, uliokuwa umekatika.

Katika tukio lingine, gari hilo la Dk Slaa lilipata pancha wakati likielekea katika mkutano uliopangwa kufanyika Iglansoni saa 9:00 alasiri.

Hata hivyo, Dk Slaa alifaulishwa katika gari la Lissu ili awahi katika eneo la mkutano na kumwacha dereva na mlinzi mmoja wakibadilisha tairi.

Source:Mwananchi

Hii nayo ni habari!? Ama kweli watu wanakifafa.....aiseee
 
Omar,

Hivi umewahi kujiuliza kuwa kwa nini ninakebehi tu baadhi ya watu na sio kila mtu?

Kuna waislam wangapi hapa JF? je ni wangapi ambao nimewakebehi? Umewahi kusoma majibu yangu dhidi ya watu kama Mkandara, Zitto, Mtu wa Pwani na wengineo?

Kama bado, sijawahi kutumia lugha ya kebehi kwao hata siku moja. Mimi ninajibu wale wanaoleta udini hapa kwa kebehi. Issue ya udini sikuianzisha mimi hapa. Mimi najibu moto kwa moto.

Kampeni za kistaarabu nimewaachia wengine. Umeona CCM wanavyomchafua Dr Slaa, ustaarabu wake haukusaidia chochote. CCM inabidi unawajibu kulingana na wanachokuletea. Wakikuita mdini na wewe wamwagie udini wao, wakileta mambo ya vimada, na wewe wapatie vimada vyao. Hii ndio motto yangu

Kuna udini,ukabila au uraia kwenye hii habari?
 
Una kumbukumbu nzuri?

Cheki Kifafa hicho!

attachment.php
 
Kikwete amefaulishwa mara ngapi katika misafara akiwa Rais Wa JMT kutokana na matatizo ya magari?

Kile kisa cha kuwekewa mafuta "yaliyochakachuliwa" kule Moshi kiliishia wapi vile?

Give me a break! That is very low from Mwananchi (if at all that is the source)

That's a convoy man! Mwananchi is right. Convoys never pull-over or turn while on track. It's dangerous.
 
Watu wanasahau kuwa:
-Juzi juzi JK kawekewa mafuta ya kuchakachuliwa, mpaka sasa kituo kimefungwa
-Gari lake lilichomoka tairi Mbagala (Nafuu ya pacha)
-Mkoani Mara, msafara ulipotea njia, Askari akatolewa Kafara
-Juzi Mkoani Kagera, mtoto wa shule amekwenda ahera - hiyo kafara au waligonga mbuzi?

Jamani watu waache kejeli kwa Dr. Slaa, he is way up in outsmarting the CCM machinery with all their resources.

Wanataka kumpunguza nguvu kwa kumwibia wagombea, kumpeleka mahakamani, kutupa pingamizi lake kwa shinikizo la Tendwa kuitwa Ikulu, n.k bado wanashangaa jamaa anapeta.
 
Khaaaaa!Kweli upofu unatuingia.Hivi kumjadili mtu ambaye anaomba dhamana ya kuliongoza taifa ni kumchafua??
 
huko madrassa mmeliongelea hili, unaweza kuifahamisha jamii hapa?

Lengo ilikuwa kufikisha ujumbe.Umefika?Stop asking such types of questions.Ur way of questioning's exposing ur thinking capacity.
 
Hivi ulitaka amendelee bila mafuta halkafu gari izime njiani kama zile zilizochomoka matairi na kuzimika, au huyu aliyezuia tatizo?

prevention is better than cure, well done Lissu
 
Back
Top Bottom